Tuesday, June 3, 2014

#UJASIRI, NGUVU, KIBALI NA UKUU UNAJENGEKA NA KUONGEZEKA ZAIDI NYAKATI NGUMU NA IMANI KTK KRISTO PIA INAKUWA NA KUIMARIKA.

Kutoka 1:9-22; Kwa habari ya wanawaisraeli na kuongezeka kwao kwa idadi, kutanuka na kuenea zaidi katika nchi na kuwa wenye nguvu zaidi kuliko wengine katika nchi.
Biblia inasema hivi katika Kutoka 1 kuanzia mstari wa 9 ya kwamba; Akawaambia watu wake (yaani yule Farao mpya ambaye hakujua baraka za Yusufu kwa Wamisri), Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. 10 Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii. 11 Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi. 12 Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli. 13 Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; 14 wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali. 15 Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua; 16 akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi. 17 Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume. 18 Basi mfalme wa Misri akawaita wale wazalisha na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto waume wawe hai? 19 Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia. 20 Basi Mungu akawatendea mema wale wazalisha; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi. 21 Ilikuwa kwa sababu wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba. 22 Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai.

Waamuzi 16: Kwa habari ya Samsoni na nguvu mpya.
Mungu wetu ni mwingi wa rehema, Kwa kutambua chanzo cha nguvu zake walidhani wamemumaliza Samsoni, kumbe hawakujua kwamba kutambua chanzo cha nguvu haimaanishi unaweza kuiba au kunyang’anya au kuondoa nguvu hizo ndani yake lahasha! kwani mhusika akitengeneza na Mungu vizuri nguvu zinakuwepo tuu. Hata kwa Musa kutumia ile fimbo haikumaanisha ukimnyang’anya ile fimbo ndio mwisho wa uweza wa Mungu ndani yake, la hasha! Uweza wa Mungu unaweza kutumika katika chochote lakini haimaanishi umeanzia katika hivyo; Kwani yote ni matokeo ya nguvu za Mungu i.e. ufalme wa Mungu ukiwa ndani ya mtu inakuwa sio roho yake bali Roho mtakatifu ndiye asili ya nguvu ndani yake ambayo ndio Mungu, sasa nani awezayo kumtoa Roho mtakatifu ndani ya mtu kama si Muumba pekee yake?, kwani hata Biblia pia inatusisitiza tusimuogopa awezaye kuua mwili (shetani) bali Mungu awezaye kuua mwili na roho pia.

Na ndio maana ukisoma Waamuzi 16 kuanzia mstari wa 20; Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha, Lakini hakujua ya kuwa Bwana amemwacha. 22 Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake, 28 Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili. 29 Kisha Samsoni akazishika nguzo mbili za katikati ambazo nyumba ile ilikaa juu yake, akazitegemea, moja kwa mkono wake wa kuume na moja kwa mkono wake wa kushoto. 30 Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. Basi wale watu aliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa wengi kuliko wale aliowaua wakati wa uhai wake.
Kwa hivyo vile walivyodhania kuwa kwa kupanga na kuweka mikakati mbali mbali ya kuwatesa wana waisraeli kungewaangamiza na kuwamaliza kabisa, Haikuwa hivyo kwani ndio kwanza walikuwa wakichochea nguvu ndani yao, ujasiri, kibali na ukuu; hii inajidhihirisha katika andiko ya kuwa zidi walivyoteswa ndivyo walivyozidi katika nchi na kuwa na nguvu sana. Na pia kwa habari ya Samsoni vile walivyodhani wamemumaliza Samsoni na kusherehekea ndivyo alivyopata nguvu kubwa zaidi na ndio maana Biblia inasema watu waliokufa wakati wa kufa kwake walikuwa wengi zaidi kuliko aliowaua wakati wa kuishi kwake.

Mapito magumu yanajenga ukuu zaidi ndani yako na ujasiri unaongezeka na nguvu kwa namna ambayo huwezi kuelezea, yaani unaongezeka kila namna kila idara, kwa maana hata ukitaka kujua nguvu zilizo ndani ya paka nikatika kumpigapiga yaani wakati anahatarishiwa uhai wake ndipo uweza ndani yake ujidhihirishapo na ndipo ajulikanapo kuwa ni hatari na ananguvu yapo anaumbile dogo lakini anaweza kumuangamiza hata adui mwenye umbile kubwa zaidi yake.

Mungu hudhihirika katika udhaifu wetu yaani nyakati za kushindwa kwetu hivyo usife moyo ndugu, kwani mateso ya mwenye haki wa Bwana ni mengi na mapito yake ni magumu sana bali Bwana Mungu humponya na kumvusha na hayo yote; yeye Mungu yuko vilevile habadiliki uweza wala nguvu wala mamlaka yaani uweza wake ni ule ule, nguvu zake ni zile zile na mamlaka ni ile ile kwa kuwa yeye Mungu Baba ndiye aliyefanya vyote mbinguni na duniani. Hivyo mtegemee Yesu wa Nazareti na kumfanya kimbilio la daima, mwanadamu ni ubatili mtupu yaani ni kama mvuke; hakika! kwa Yesu utashinda kwani yeye si mwanadamu hata aseme uongo, naam! na majaribu yako na yawe mtaji leo katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareti upandishwe juu kama tai, Amina.