Yesu wa Nazareti ni Neno la Mungu lenye mamlaka yote juu ya giza,
hivyo kupitia Neno la Mungu lililojaa mamlaka ya Mungu ndiko
ukombozi kutoka gizani uliko.
Unajua hata wakati wa Musa Nabii wa Mungu kwakusaidiana na
Haruni walivyotumwa kuwakombea wana waisraeli kutoka utumwani
misri mikononi mwa Farao, Wanawaisraeli walikuwa wakifanya kazi
ya kufyatua tofali huko Gosheni mji ulikuwa umetengwa huko Misri
kwa ajili ya waisraeli kwa kazi hiyo. Walifanya kazi hiyo katika
mazingira magumu lakini pamoja na ugumu wake Mungu alikuwa nao
ndio maana ilifika wakati ulioamuliwa wao kuachiliwa huru.
Cha ajabu Musa na Haruni walipowaomba wanaisraeli kwa Farao
naye akawa mugumu kuwaachilia na zaidi ya kuwazuilia Farao pia
aliongeza kiwango cha adhabu na mazingira magumu zaidi ya utendaji
kazi hiyo na kila Musa alivyokuwa anamkemea Farao kuwaachilia
wanawaisraeli ndivyo kazi yao ilivyoongezwa ugumu jinsi ya kuitenda.
Soma Kutoka 5:6-9 inasema; Na siku ile ile Farao akawaamuru
wasimamizi wa watu, na wanyapara wao, akisema, Msiwape watu
tena majani ya kufanyia matofali, kama mlivyofanya tangu hapo; na
waende wakatafute majani wenyewe.
Lakini hesabu ya matofali waliyokuwa wakifanya tokea hapo,
wawekeeni iyo hiyo, msiipunguze hata kidogo, kwa maana ni wavivu
hao; kwa hiyo wanapiga kelele, wakisema, Tupe ruhusa twende
kumtolea Mungu wetu dhabihu, wapeni watu hao kazi nzito zaidi,
waitaabikie; wala wasiangalie maneno ya uongo. Ona pengine
wanaisraeli wangemwamini Musa, kutii maagizo yake kutoka kwa
Mungu na kuambatana naye na kusimama katika nafasi moja toka
awali hata zile adhabu zilizoongezwa za kufyatua tofali zisingedumu
na Farao asingekuwa na nguvu kuendelea kuzuia, mng’ang’anizo wake
huyo Farao ulitokana pia na hofu ya wanawaisraeli kwamba
kunakutoka kweli hapa, na kwa kuwa ule ujumbe wa Mungu kwao
kwamba sio mateka tena hawakuuamini, hivyo ililichukua Neno la
Mungu alilotamka Musa kuwa miujiza na maajabu mengi ili
kuwaaminisha kuwa ni Mungu wa baba zao ndiye aliyemtuma na
kumdhoofisha Farao kuwa anayeshindana naye si Musa bali ni Mungu
hakika muumba wa vyote ambaye ni “Nipo ambaye Nipo” yaani
Neno.
Hivyo msaada wa mtu aliyeshikwa na ufalme wa giza u katika Neno
la Mungu ambaye ndiye Yesu wa Nazareti la siivyo unavyozidi
kung’ang’ana na ufalme wa giza kuhusu uhuru wake bila yeye kujawa
na Neno ndivyo yule muathirika anavyozidi kupata vita vikali kutoka
ufalme wa giza. Kwa hiyo sala zako za kumukomboa muathirika wa
mapepo zisikome mpaka atakavyopona hakika na kuwekwa huru,
huku Neno la Mungu likifanyika msingi kwake wa maisha, kwani
yeye akijawa na Neno litampa ujasiri ambao utamuondolea hofu hivyo
naye ataweza kumpinga shetani na ufalme huo wa giza na mwisho
atakuwa huru. Kwa kuwa uhuru hauwi uhuru kama mhusika asipojijua,
Neno la Mungu pekee litamjuza mtu juu ya uhuru hivyo ni wajibu wa
mtumwa wa kristo kusimama naye imara katika imani ileile uiaminiyo
uliyomuaminisha yeye na kumthibitisha Mungu kwake aliyemkombozi
mwenye haja naye.
Na Neno lake pekee lililo ushuhuda kwake ndilo limfanyalo awe jasiri
na kutambua nafasi na sehemu yake katika ufalme wa Mungu kwa
hapo hakika ushindi utakuwa mkuu na thabiti pasipo kupitia magumu
zaidi na kufuatwafuatwa na ufalme huo wa giza au kung’ang’aniwa na
Farao.
Ndio maana katika Luka 11:24-26 Neno linasema; ”Pepo mchafu
akimtoka mtu, anazunguka jangwani akitafuta mahali pa kupumzikia.
Asipopata anasema, ‘Kwa nini nisirudi kwenye nyumba yangu
niliyotoka? Akirudi, na kuikuta ile nyumba ni safi na imepangwa
vizuri, huenda kuwaleta pepo wengine saba wachafu kuliko yeye
wakaingia na kuishi humo. Na hali ya sasa ya mtu huyo inakuwa mbaya
kuliko ya kwanza”.
Na ndio maana saa ingine najiuliza wakati wana waisraeli jangwani
wanang’atwa na nyoka na wengine kufa, maelekezo ya Bwana kwa
Musa ilikuwa ni kutengeza nyoka wa shaba na kumuweka juu ya
wote aliyethubutu kumuangalia aliwekwa huru ambaye hakutenda
hivyo alikufa, hivyo ni Neno la Bwana na maelekezo yaliyosimamiwa
na Musa na huku matokeo ya uponyaji wao ikiwa ni Bwana ndiye
atendaye. Musa aling’ang’ana na shida zao tu kwa kulifunua na kulijuza
Neno la Bwana kwao kwa kuwa alijua jawabu na matokeo ni kazi ya
Bwana ndiye afanyaye wala si yeye, Musa jukumu lake ilikuwa ni
kulisema na kuliaminisha Neno la Bwana kwao.
Hata Yesu wa Nazareti sehemu nyingi hakuhangaika na matokeo bali
Neno la Mungu alilohubiri ndio lililopelekea matokeo; ishara, ajabu
na miujiza mingi, kwa maana ingine kiu yake kuu ilikuwa ni kuufunuo
ufalme wa Mungu duniani ya kwamba watu waijue kweli ya Mungu,
waishike na kuiishi na maarifa yake yote alitumia katika hilo. Kwa
maana ni Neno la Mungu pekee ndio limuwekalo mtu huru yaani ile
kweli anayoijua ndio uhuru wenyewe lasivyo ufalme wa giza hautaacha
kumfunga.
Tunafunzwa kuwajaza Neno la Mungu, kuwafanya waliamini na kuliishi
hilo Neno kwa maarifa yote na kuwaweka katika msingi wa Neno na
kufanya nao sala mara kwa mara wale waliotangaziwa uhuru yasije
mapepo au vifungo vyovyote vya ufalme wa giza vikawashika na
kuwafunga tena, kwani kwa Yesu ndiko ziliko njia za kutoka mautini
na gizani, Amina.
http://www.slideshare.net/Recknald/depend-on-jesus-of-nazareth-man-is-a-mere-vapour
http://www.slideshare.net/Recknald/depend-on-jesus-of-nazareth-man-is-a-mere-vapour
No comments:
Post a Comment