Yale
uyatafakariyo kwa kina kutoka ndani kabisa ya kirindi cha moyo wako yaani lilo
neno la Mungu ambalo kila wakati unakuwa ukilitafakari, ukilifikiria na
kumshangaa Mungu kwa hilo jinsi alivyo wa ajabu na mkuu sana, ni kwa hilo ndipo
utamwona Mungu na atajidhihirisha kwako na hiyo ndiyo kweli itakayo kuweka huru
kabisa, na jambo hili ndilo liwafanyalo wanadamu kuwa na hofu ya Mungu na moyo
wa uchaji katika kristo. Udhihirisho wa Mungu kwako ni mpaka umtafakari na
kumfikiri yeye kwa kina, kupitia neno lake, kwa sala, kwa sifa na kwa kuabudu
na lile jawabu ulipatalo ndio udhihirisho wa Mungu kwako katika muda ule na ule
ujumbe kutoka kwa mtumwa wa Bwana.
Hebu
kwa sekunde kadhaa fikiri kwa kina sana, na najua kwa Bwana unaweza pata ufunuo
kwamba ilikuwajekuwaje;
Je
Zakaria akiwa hekaluni alikuwa anatafakari nini kwa kina ile kabla tu Malaika
Gabrieli hajamtokea? (Luka 1:5-16)
Je
Bikira Mariamu alikuwa anatafakari nini kwa kina ile kabla tu Malaika Gabrieli
hajamtokea? (Luka 1:26-35)
Je
Wachungaji walikuwa wakitafakari nini kwa kina pale walipokuwa wanachunga
mifugo kwa zamu ile kabla tu Malaika wa Bwana hajawatokea? (Luka 2:8-15)
Je Gideoni alikuwa akitafari nini kwa kina ile
kabla tu Malaika wa Bwana hajamtokea pale kwenye mti wa mwaloni? (Waamuzi
6:11-13)
Je
Mama yake Samsoni alikuwa akitafari nini kwa kina ile kabla tu Malaika wa Bwana
hajamtokea? (Waamuzi 13:2-3)
Je
Musa alikuwa akitafakari nini kwa kina ile kabla tu hajaona Malaika wa Bwana
kwa njia ya kijiti kinachowaka pasipo kuteketea na Bwana kuzungumza naye?
(Kutoka 3:1-10)
Je
Joshua alikuwa akitafakari nini kwa kina ile kabla tu hajamuona Malaika wa Bwana
na upanga alipokuwa akitaka kwenda kuushambulia mji wa Yeriko? (Joshua 5:13-15;
6:1-2)
Je
Eliya alikuwa akitafakari nini kwa kina ile kabla tu Bwana kujidhihirisha kwake
kule mapangoni? (1 Wafalme 19: 4-8)
Je
Kornelio alikuwa akitafakari nini kwa kina ile kabla tu Malaika wa Bwana
hajamtokea mchana kweupe? (Matendo 10: 1-8)
Hebu
fikiri, Je mitume walikuwa wakitafakari nini kwa kina mle ndani ile siku ya
pentekoste ile kabla tu Mungu hajajidhirisha kwao kwa kuwavuvio Roho mtakatifu
kwa nguvu? (Matendo 1: 14; 2:1-4)
Na
je hebu fikiri kwa kina mwenyewe wale watu wawili waliokuwa wanatokea
Yerusalemu walikuwa wanafikiria nini na wanatafakari nini hasa na
kushirikishana nini kuhusu Yesu kulichowapa majonzi na mzigo mkubwa moyoni mwao
kwa kiasi ambacho mpaka wakahisi kuwaka moyoni mwao pasipokujua Yesu amefufuka
na alikuwa ameambatana nao na ndiye aliyekwenda nao kula pamoja na akafanya
ishara ya meza ya Bwana mbele yao. (Luka 24:13-32)
Hebu
tu wewe mwenyewe fikiri kwa kina kuna uhusiano mkubwa kati ya yale tuyafikiriyo
na tuyatafakariyo iwe kwa Neno kulisoma au kulitafakari, kwa sala, kwa kusifu
na kwa kuabudu na yale yajidhihirishayo kwako baadaye yaani ile tu baada ya
mawazo uliyonayo katika fahamu zako yatokayo moyoni mwako. Kutokana na mifano
ya hapo juu hawa watu wa Mungu ile kabla tu Mungu hajajidhihirisha kwao,
nikwambie tu hawakuwa wanarukaruka ama kuchezacheza tu au kufikiria upuuzi bali
walikuwa katika kufikiri na kutafakari yaliyo ya Mungu na hayo ndiyo
yaliwapeleka katika uwepo mkuu uliokuwa unawapeleka ulimwengu mwingine wa
rohoni yaani walikuwa katika roho kwa mambo ya rohoni haswa na sio katika mwili
wa nyama kwa kiasi ambacho kulikuwa hakuna namna ya Mungu kutoweza kuvutika
kwao ndani ya moyo yao na hata kujidhihirisha kwao kwa njia ya malaika zake.
Unajua ni mshangao na saa nyingine inashitua sana kwa wengi pale yale
tuyafikiriyo na kuyatafakari kutokea mara yaani wakati huo huo ukiwa bado
katika tafakari, inakufanya ushuke na kububujika moyoni kwa namna ambayo uwepo
wa jawabu lako huwa ni utukufu mkuu wa Mungu kwako, na huo ndio ukawaida wa
uwepo wa Mungu tunaopaswa kuwa nao watoto wa Mungu katika Bwana kwa sala, dua
na tafakari zetu kumbuka Henoko alitembea na Mungu miaka 300.
Kwa
hiyo ni wewe ndiye unayepaswa kumvuta Mungu kwa karibu kwako kupitia jina la
Yesu Kristo kwa kumfikiri yeye, kutamani kuwa naye kila wakati, kuishi naye
akiwa ndani yako, hivyo ndivyo ukaribu ule muunganiko na Mungu uundavyo kupitia
roho mtakatifu. Yale uyafikiriayo katika fahamu zako na yale yaliyo moyoni
mwako ya wazi mbele za Mungu hakuna kinachoweza kufichika kwake siku zote yeye
hujidhihirihsa kwa wakati wake. Tamani kuwa naye, mfikiri yeye usiku na mchana
na litafakari Neno lake Mungu, Yesu kamwe hata kuangusha na hakika roho
mtakatifu atajidhihirisha katika maisha yako sio kwa asilimia fulani tu bali
mzima kabisa kwa sababu ni Mungu, Amina.
No comments:
Post a Comment