#YESU WA NAZARETI NI MWAJIRI MWEMA NA MKAMILIFU

   Saa nyingine nashangaa namna Mungu alivyoweka uweza wa kufikiria ambao unatofautiana kutoka kwa mmoja hadi mwingine. Hali hiyo ipo kimungu zaidi ya uelewa wetu, leo nilikuwa nimetulia darasani ghafla ukanijia ufahamu kwa njia ya tofauti kabisa na nikashangaa sana hebu ona hii, Kiuhakika Yesu Kristo ni mwajiri mwema na mkamilifu.

HRM- Naona wengi wanasomea jinsi ya kutawala wafanya kazi na kuwa waajiri wazuri kuanzia level ya cheti, diploma, degree, master na PhD. Nafikiria hivi namna gani mtu unaweza kutawala wafanyakazi wenye upeo wao, mawazo yao, fikra zao, uelewa wao na dhamira zao, Ndio! mfanya kazi kwani kutawala uwezo wa mtu kufanya kitu fulani ni kumtawala mtu huyo. Mara nyingi nimeona na kusikia watu wakuchukua mbwa mdogo au paka mdogo au simba mdogo, n.k na kuamua kuwatunza na kuwafundisha namna ya kuwasikia, kushirikiana na kuwaheshimu mpaka wawavyo wakubwa lakini wanakuja kusalitiwa na wanyama hao na wengine kung’ata na pengine hadi kufa kwa kuumizwa vibaya na wanyama hao. Sasa si zaidi sana matukio yawapatao au kuwatukia wale wajaribuo kuwa na uwezo mkubwa katika kutawala na kusimamia wafanyakazi, hii hainiingii akilini yaani kutenda kwake ni ngumu. Wanadamu matarajio yao ndio mipango yao na siyo mipango yako; Mfanyakazi awezaye kutawalika ni yule tu aliyeamua kuwa na utii juu yako na sio yule unayetaka akutii na kutekeleza matakwa yako. Wengi hufanya kwa kukuridhisha tu lakini si kwa kutaka kama hakuridhia kuongozwa na wewe. Mfano mzuri ni Ndoa; uhusiano wa mume na mke, Mume ambaye ni kichwa amutawala mke wake na kule mke kumtamani mume wake ndiyo kunamfanya atawalike(Mwanzo 3:16), kwa hivyo ni mpaka mke mwenyewe aridhie kuwa na utii juu yake (yaani amtamani mume wake) la sivyo hatawaliki mtu hapo. Ukilazimisha kumtawala hata kumuongoza mtu pasipo yeye mwenyewe kutaka nadhani hapo itakuwa ni shida tu. Unajua saa nyingine hata ng’ombe sio rahisi kumuwekea nira pasipo mbinu fulani fulani la sivyo utakesha na hiyo ni kwa mnyama, mwanadamu je si zaidi?, Wenye hekima ya Mungu mara nyingi ndio wawezao kuwatawala na kuwaongoza wafanyakazi(watu) na ni mara chache sana kwa waliosomea nyanja hiyo pasipo hekima ya Mungu ni kama bure. Mungu tupo hekima ya kujiongoza na kujitawala sisi kwa sisi na sio useme Chuo nipe hiyo profesion ya kuongoza na kutawala wafanyakazi kwa namna nipendavyo mimi, nakuhakikishia kwa hivyo haitafaa. Unaona saa nyingine tunajidanganya wenyewe; kufanya kile wasichotarajia mawazoni mwao haimaanisha wanakutii kwa sababu wanaweza kuwa wanakudanganya pia; ufanisi kwa kufanya yatarajiwayo na wakuu pasipo hila haiwezi fanikishwa kwa kuwafanya uwaongozao kukuogopa lakini kwa wao wenyewe kuamua na kukubali kuwa na utii juu yako ndipo wanaweza kukuheshimu. Ukamilifu katika kila profesion unafanikishwa tu kupitia Yesu Kristo kwa kuwa yeye ni profesa wa maprofesa wa profesion zote ambazo watu huzipata na zile wajaribuzo kuzipata na kuzihitimu. Kwa maana ni yeye pekee aliyefanikiwa kuwatawala na kuwaongoza wanadamu wa rika tofauti, tamaduni tofauti, imani tofauti, uwezo tofauti na mataifa tofauti mpaka milele yote. Nasema hivyo kwa sababu akikuchagua anakutunza na hakupotezi na automatically unajiunganisha naye na kwa sababu ya Roho mtakatifu unamtii na kumheshimu. Ukisoma biblia Mathayo 11:28-30; hakulazimishi wala kutumia nguvu lakini anakuita kwa upole huku akikuahidi kuwa mzigo wake ni mwepesi na nira yake ni laini na wewe kwa kumkubali hautafanya jambo jingine lolote pasipo uthibitisho kutoka katika Roho mtakatifu. Mfanye leo awe mwajiri wako akuongoze kwa kuwa yeye si mkatili wala mkali bali ni Mwajiri mkamilifu, mwema, mpole na wenye ujira mpaka milele yote.

No comments:

Post a Comment