#EWE MFUASI, JIFUNZE KWA ANDREA MTUME WA YESU KRISTO WA NAZARETI

    Andrea, mtume wa mwanzo kuchaguliwa, mwenyekiti wa mitume wa Ufalme wa Mungu, alizaliwa Kapenaumu. Alikuwa mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watano, yaani yeye na mdogo wake Simon Petro mtume, na dada zake watatu. Baba yake Yona kabla ya kufa alikuwa mshirika wa Zebedee katika Biashara ya kukausha samaki Bethasaida, katika bandari ya uvuvi ya Capenaumu. Alipokuwa Mtume wa Yesu wa Nazareti, Andrea alikuwa hajaoa lakini aliishi na mdogo wake Simoni Petro mtume aliyekuwa amekwishaoa. Wote walikuwa wavuvi na washirika wa Yakobo na Yohana wana wa Zebedee katika Biashara hiyo.
Andrea alichaguliwa kuwa mtume wa Yesu wa Nazareti akiwa na miaka 33, akiwa amemzidi Yesu wa Nazareti kiumri na aliwazidi na mitume wengine wote kiumri, ambapo katika mitume ni Yohana tu aliyekuwa mdogo kuliko wote aliyechaguliwa kuwa mtume akiwa na miaka 24. Andrea aliibukia kuwa mwerevu na mwenye uwezo mkubwa wa kufanya jambo kimatendo katika kundi la mitume wa Yesu wa Nazareti. Japo hakuwa mzungumzaji sana, alikuwa mshapu na mfuatiliaji wa mambo katika kundi la mitume kwa karibu kwa uwezo wa juu sana. Yesu hakumpa Andrea jina jingine [a.k.a], lakini mitume wa Yesu mapema wakaanza kumuita mkurugenzi wa Yesu wa Nazareti, na wakamlinganisha kwa jina jingine kama Chief yaani mtu waliyempa nafasi ya juu ya uongozi katika kundi la mitume.
Andrea alikuwa muongozaji mzuri lakini zaidi alikuwa msimamiaji mzuri wa shughuli za huduma za kundi la mitume wa Yesu wa Nazareti. Alikuwa mmoja wa mitume wanne waliokuwa karibu sana na Yesu wa Nazareti, lakini uchaguzi wa Yesu kumfanya mkubwa wa kundi la mitume ilimfanya alazimike kubaki katika kazi hiyo ya kusimamia kundi la mitume hata wakati wale watatu yaani petro, Yohana na Yakobo wakipata nafasi ya pekee ya kukomunika na Bwana Yesu wa Nazareti mlimani ambapo wakapata kuona muujiza mkubwa wa kuwaona manabii wawili wa kale waliokuwa wakizungumza na Yesu wa Nazareti huku naye kubadilika sura na mavazi kuwa meupe pe! pale mlimani. Na mpaka mwisho Andrea alibakia kuwa mwangalizi yaani [dean] wa kundi la mitume wa Yesu wa Nazareti.
Japokuwa Andrea hakuwa mhubiri mzuri sana, lakini alikuwa mtenda kazi hodari katika kundi la mitume, akiwa mtume wa mwanzo wa ufalme kuchagulia mapema akamchukua na mdogo wake Petro akamuunganisha kwa Yesu wa Nazareti, ambapo huyo Simoni Petro akajakuwa moja kati ya wahubiri wakubwa wa Ufalme wa Mungu. Andrea alikuwa chief sapota, yaani mfuasi mzuri wa kanuni za Yesu katika kutumia njia ya kujituma kikazi katika kundi la mitume kama namna ya kuwafunza mitume 12 kuwa mamesenja wa Ufalme wa Mungu.
Iwe Yesu wa Nazareti aliwafundisha mitume wake kisiri ama alihubiri kwenye makutano, Andrea siku zote alielewa kila kitu kilichokuwa kinaendelea katika kundi la mitume; alikuwa msimamizi muelewa na hodari. Andrea alitoa maamuzi ya haraka katika kila jambo lililoletwa kwake, labda liwe lile lililojuu ya uwezo wake, ambalo katika hilo alimpelekea moja kwa moja Yesu wa Nazareti mwenyewe.
Andrea and Petro walikuwa tofauti sana kitabia na wasifu, lakini ni lazima irekodiwa milele kuwa walienda pamoja bila kukwazana pamoja na tofauti zao. Andrea hakuwahi kuwa na wivu juu ya Petro kwa kule kuwa na uwezo mkubwa wa kuhubiri, na kuongea kwa ujasiri bila kusitasita. Mara nyingi tumeona watu wa jamii ya Andrea wakiwaonea hata kuwakwaza sana wadogo zao wenye vipaji zaidi yao. Andrea na Petro hawakuonekana wakioneana wivu juu ya uwezo na mafanikio tofauti waliyo nao baina yao. Hata siku ile jioni ya Pentekoste, wakati Petro kwa uwezo wa Roho Mtakatifu akiwa amejaa Nguvu na kutoa mahubiri yenye msisimuo wa ajabu yaliyoweza kuvuta nafsi 2,000 [watu] kwenye ufalme wa Mungu, Andrea alimwambia mdogo wake Petro: “Singeweza mimi kufanya hivyo, lakini nafurahi sana nina mdogo wangu ambaye amethubutu na kufanya haya”. Ambapo Petro alimjibu akasema; “ Lakini pamoja na wewe kunileta kwa BWANA na kunihakikishia mshikamano siku zote pamoja na BWANA, hakika nisingekuwa hapa kuyafanya haya”. Andrea na Petro walitangua sheria kwa kuthihirisha kwamba hata ndugu au makaka wa familia moja wanaweza kuishi pamoja kwa amani na kufanya kazi pamoja kiuhodari kabisa bila kufarakana.
Na hata baada ya Pentekoste Petro alikuwa maarufu sana na utukufu mkuu wa Mungu ulikuwa juu yake, lakini pamoja na hayo yote haikumkwaza ama kumuumiza Kaka yake Andrea ile kuishi miaka yote akitambuliwa kama “Kaka wa Simoni Petro”.
Na katika mitume wote wa Yesu wa Nazareti, Andrea alikuwa ni mzuri katika kuwaamua wanadamu wenzake. Alijua tatizo na shida ilikuwa ikimsuka suka moyoni Yuda Iskarioti hata kabla ya mitume wengine kuhisi na kujua kwamba kuna jambo linalomsumbua Mhasibu wao yaani Yuda; lakini hakumwambia yeyote hofu zake hizo. Andrea huduma kubwa aliyoitenda kwenye kanisa la mwanzo la ufalme wa Mungu ilikuwa ni kuwashauri Petro, Yakobo na Yohana kuhusu uchaguzi wa wamisionari wa kwanza ambao walitumwa kwenda kuihubiri injili [habari njema] ya Yesu wa Nazareti, na pia katika kushauri wazee wa kwanza wa kanisa namna ya kupangilia utawala na usimamizi wa huduma ya Ufalme wa Mungu. Andrea pia alikuwa na kipaji kikubwa cha kugundua vipawa vilivyofichika na vilivyofunikwa vya vijana.
Mapema kabisa baada ya Yesu kupaa mbinguni, Andrea akaanza kuandika katika rekodi zake yale ambayo Yesu wa Nazareti alikuwa akiyasema na kuyafundisha. Lakini baada ya Andrea kufa, nakala zingine za rekodi binafsi ya Andrea zilikusanya na kusambazwa bure kati ya mwalimu wa mwanzo wa kanisa la Kristo. Haya maandiko ambayo yaliaminika kuwa ni ya Andrea yakaanza kufanyiwa marekebisho, kusahihishwa, kubadilishwa na kuongezwa mpaka yalivyoonekana kuendana kabisa na maisha ya BWANA Yesu wa Nazareti duniani. Ya mwisho kabisa kubadilishwa na kurekebishwa yalihalibiwa kwa kuchomwa na moto huko Alexandria kama miaka 100 hivi baada ya kuandikwa halisi na wale wafuasi waliochaguliwa mwanzo kabisa na mitume kumi na mbili.
Andrea alikuwa mtu mwenye mawazo chanya, fikra maanani, maamuzi yanayoshikamanisha, ambaye nguvu ya wasifu wake mkubwa ilihusisha msimamo mkubwa aliokuwanao. Udhaifu wake ilikuwa kwamba hakuwa na hamasa ya haraka; mara nyingi alishindwa kuwatia moyo mitume wenzake kwa maamuzi ya kuridhia.
Kila mmoja wa mitume wa Yesu wa Nazareti alimpenda Yesu, lakini ilibakia kweli kuwa kila mtume alivutwa kwake kwa sababu ya aina fulani ya tabia aliyokuwa nayo iliyofanya kila mtume atake kuwa nayo. Andrea alimshangaza Yesu wa Nazareti kwa sababu ya uaminifu na utu usibadilika badilika. Wakati watu walipomjua Yesu wa Nazareti, alipatwa na hamasa ya kuwajuza na wengine marafiki; na alitaka dunia nzima umjue Yesu.
Hata baada ya mateso na kuwindwa kwao baada ya ujio wa Roho mtakatifu ili wauawe hao mitume, walitawanyika kutoka Yerusalemu, Andrea alisafiri kuhubiri injili huko Armenia, Asia, Makedonia na baada ya kuwaleta maelfu kwenye ufalme wa Mungu, mwishowe akashikwa na kusulubiwa kwenye msalaba wa 'X' huko Patrae ya Achaiana kwa sababu hakuona kama ni vyema kusulubiwa kwenye msalaba kama ambavyo Yesu wa Nazareti alivyosulubiwa. Na alikaa kwenye msalaba wa mateso kwa siku mbili, na masaa yote ya siku hizo aliendelewa kuhubiri kuhusu wokovu wa ufalme wa mbinguni kwa furaha mpaka mwili ulipozima.
Anayeamini wasifu huu ni mzuri na wa baraka kuwa nao katika shamba la Bwana basi apokee kwa imani yake kwa uweza wa Roho mtakatifu, Nasema tena pokea! Upako wa Andrea sasa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, Amina.

Barikiwa na Bwana.


Maandiko:  Marko 13:3-4, Yohana 1:41, Mathayo 4:18-22, Marko 1:16-20, Yohana 12:20-22 na Yohana 6:8.

No comments:

Post a Comment