#MUNGU HUCHUKIA WAJIKWEZAO

       Kujikweza ni dhambi mbaya sana kwa sababu inamuongoza mwanadamu kumuasi mwenyezi Mungu. Dhambi ya kujikwezwa ndio iliyomsababisha shetani ajiinue na kumuasi Mungu, na hiyo ndiyo iliyopelekea anguko lake kutoka mbinguni mpaka kuzimu. Mtu yeyote ajiinuaye na kujikweza huamini anaweza kujitegemeza maisha yake mwenyewe vizuri kabisa pasipo Mungu. Na upande mwingine Mnyenyekevu anatambua kuwa kila kitu akihitajicho duniani kinatoka kwa Bwana. Na ndio hao tu wanaojua kuwa wamuhitaji Mungu ili wapate ufalme wa Mungu.

Yesu alisema; kuwa mkuu katika ufalme wa Mungu unatakiwa uwatumikie wengine (Luka 22:26) kwa kusema yeyote atakaye kuwa mkubwa wa wengine kati yenu anatakiwa kuwa mdogo kuliko wote na kiongozi sharti awe kama mtumwa, hiyo yote inahitaji uvumulivu.

Biblia inasema katika (Yakobo 4:6) lakini ametupa neema sana, na ya kwamba Mungu huwapinga wajikuzao bali huwapa neema wanyenyekevu. Katika Mathayo 5:3 inasema, Heri masikini wa roho kwa kuwa ufalme wa mbinguni ni wao. Hivyo Mungu hawakubali wala kuwapaka mafuta watu kutokana na kujulikana kwao au kusemwa vizuri na watu bali wasifu wa ndani ya mtu ndio anaouangalia. Na Isaya 40:29 inasema huwapa nguvu wazimiao, humwongezea yeye asiyekuwa na uwezo. Kumbuka kujinyenyekeza kwa Mungu na sio kwa mwanadamu kama neno lisemalo heri walio masikini wa roho yaani yeye yule ambaye siku zote anauhitaji rohoni mwenye upungufu maana ufalme wa mbinguni ni wao, Sema nanyenyekea kwako Bwana sasa.

No comments:

Post a Comment