Matendo
ya Mitume 7:22-35; Neno linasema; 22 Musa alifundishwa mambo yote ya hekima ya
Wamisri akawa mashuhuri kwa maneno na matendo. 23 Alipokuwa na umri
wa miaka arobaini aliamua kwenda kuwaona ndugu zake Waisraeli. 24 Huko alimwona
mmoja wao akitendewa vibaya, akaenda kumwokoa, na kulipiza kisasi, akamuua yule
Mmisri. 25 (Alidhani kwamba
Waisraeli wenzake wangeelewa kwamba Mungu angemtumia yeye kuwakomboa, lakini
hawakuelewa hivyo.) 26 Kesho
yake, aliwaona Waisraeli wawili wakipigana, akajaribu kuwapatanisha, akisema:
Ninyi ni ndugu; kwa nini basi, kutendeana vibaya ninyi kwa ninyi? 27 Yule aliyekuwa
anampiga mwenzake alimsukuma Mose kando akisema: Ni nani aliyekuweka wewe kuwa
kiongozi na mwamuzi wa watu? 28 Je,
unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri jana? 29 Baada ya kusikia
hayo Mose alikimbia, akaenda kukaa katika nchi ya Midiani na huko akapata
watoto wawili. 30 Miaka
arobaini ilipotimia, malaika wa Bwana alimtokea Musa katika kichaka kilichokuwa
kinawaka moto kule jangwani karibu na mlima Sinai. 31 Mose alistaajabu
sana kuona jambo hilo hata akasogea karibu ili achungulie; lakini alisikia
sauti ya Bwana: 32 Mimi
ni Mungu wa baba zako, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo! Mose akatetemeka kwa
hofu na wala hakuthubutu kutazama zaidi. 33 Bwana akamwambia:
Vua viatu vyako maana hapa unaposimama ni mahali patakatifu. 34 Nimeyaona mabaya
wanayotendewa watu wangu kule Misri. Nimesikia kilio chao,nami nimekuja
kuwaokoa. Basi sasa,nitakutuma Misri. 35 Huyu Musa ndiye yule
watu wa Israeli waliyemkataa waliposema: Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi
na mwamuzi wetu? Kwa njia ya yule malaika aliyemtokea katika kichaka
kilichokuwa kinawaka moto, Mungu alimtuma Musa huyo awe kiongozi na mkombozi. 36 Ndiye
aliyewaongoza wale watu watoke Misri kwa kufanya miujiza na maajabu katika nchi
ya Misri, katika bahari ya Shamu na jangwani kwa muda wa miaka arobaini.
Sehemu A: Bwana Yesu asifiwe tumepewa ufahamu
utumie upate kufahamu na kujawa na maarifa na Hekima ya Mungu. Katika hili Neno
tunaona Musa alipofikisha miaka 40 aliazimia kuwasaidia ndugu zake kutokana na
kibali alichopewa na Mungu katikati ya waisraeli waliokuwa utumwani Misri
kilichomfanya akubalike katika familia na utawala wa farao. Ule mzigo ndani
yako juu ya ndugu ndio uliompelekea yeye kuazimia na kufanyika njia ya Mungu
kuzungumza na wana wa Israeli waliokuwa utumwani. Lakini dhidi Musa
alivyoonyesha kuugua kwake moyoni dhidi ya mateso yao na kuonewa kwao, neno la Mungu
linasema ule mistari wa 27 kwamba yule aliyekuwa anampiga mwenzake alimsukuma
Musa kando akisema: Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuzi wa
watu?. Biblia inatuambia maneno ya Yule
mtu yalimshitua sana Musa na kumfanya akimbilie nchi ya midiani. Yawezekana
aliyemtisha Musa alijua hakika Musa ndiye Kiongozi na mwamuzi wao kwani twajua
shetani wa mtu ni mtu, na shetani humtumia yoyote yule na pengine alijua Musa
anaanza kazi yake ambayo kwa hiyo aliletwa duniani, akamtisha. Hofu na woga ni
maadui wakubwa wa Imani kile ukionacho kwa macho ya rohoni au ushuhudiwacho
moyoni shikilia shetani siku zote hupinga penye anguko lake. Ukiruhusu woga au
hofu utawale maono yako hupotea na gharama ni kubwa. Yesu alipoulizwa eti wewe
ni mfalme wa Wayahudi akasema wewe wasema, kwani yesu alijua inajulikana hivyo
na alizidi kukiri hivyo. Lakini Musa alihofu baada maulizo ya vitisho kwa maana
alidhani kwamba Waisraeli wenzake wajua kwamba Mungu ameweka mzigo ndani yake
juu yao, Saa ingine yafaa kushikilia kile kilichojulikana ndani yako hata kama
utapingwa, kurudi nyuma ni ishara ya kushindwa na kutokuwa na ujasiri.
Ilimchukua Musa miaka 40 tena tangu alipokimbilia nchi ya midiani si kwa
kumtafuta Mungu bali kwa hofu ya ule utisho na akaanza kufanya mambo mengine tofauti
na ule wito uliojengeka moyoni kwa mzigo mkuu tangu alipokuwa na umri wa miaka
40, hofu na woga ilimsababishia gharama ya miaka 40 kusota ugenini pasipo
kutimiza wito wa roho ambao ulikuwepo tangu alipokusudia na kuazimia kuwa
msaada kwa wengine. Nasema ni hofu na woga kwa sababu hata Malaika wa Bwana
alipomtokea katika mwali wa moto kumtaka arudi misri kuwaokoa wana waisraeli
kutoka utumwani bado Musa alidai nitasema nimetumwa na nani?, nitafanyaje ili waniamini kwamba
nimetumwa?, kwa maana nyingine hofu ilikuwa bado ingalimo kwamba hawa ndugu
niliokusudia kuwasaidia hawakuamini wataniamini tena?. Mpaka alipopewa ishara
za Uungu za kuwaonyesha na pia akapewa na msaidizi Aaroni. Kwa hiyo ile Imani ya kwamba Mungu anataka
kumtumia yeye kuwakomboa na kuwaongoza ilikuwa dhabiti tangu alipokuwa na miaka
40, hivyo hata katika yale maulizo yao, Je ni nani amekufanya wewe kuwa mkuu na
mwamuzi juu yetu? Hekima ya Mungu ingesimama kama tu pasingekuwa na hofu na
woga, ndio maana pia Neno linasema mkisimamishwa mbele ya baraza msifikiri fikiri
mtasema nini Bwana asema nitawajaza neno kupitia Roho mtakatifu. Kutambuliwa au
kutokutambuliwa kwako sio kigezo chakutumika au kutokutumika na Mungu na pia
uwe unatambua au humtambui Mungu aliyekutuma sio kigezo kuwa wewe sio chombo
cha BWANA. Mungu humtumia yeyote amtakaye kwa wakati wake aidha anajulikana au
hajulikani au aidha anamjua Mungu au hamjui, Kizuri au kisichofaa, chema au
kibaya, cha heshima au chakudharauliwa vyote ni vyombo vyake vinavyomfaa Mungu
kwa kazi yake kwa majira yake.
Neno linasema
Imani ni kuwa na hakika juu ya mambo yatarajiwayo na ni bayana ya mambo ambayo
hayajatokea bado, twajifunza kung’ang’ana na Imani kwani mwenye haki wa Mungu
ataishi kwa imani na akisitasita neno linasema Bwana Mungu hata kuwa na haja
naye tena. Hebu fikiria kwa habari ya Musa miaka 40 kutoka nje ya mstari je,
hii si gharama?. Wajua maono na malengo uliyonayo, utafikaje kwa wakati sahihi
ulioamuliwa pasipo Imani na ujasiri wa yale uyakusudiayo kutenda?. Kwani twajua
wakatishaji tamaa wapo na wakwazao pia ili ya kwamba ushindi uwe mkuu kwa maana
utahesabiwaje ushindi hali huna mshindani? Na kipimo cha kupima yupi yupo juu
ni kuwepo na washindwaji wa chini. Hivyo komboa wakati kwa kuwa na ujasiri
katika maamuzi na imani isiyotikisika.
Na pia kaa ukijua ya kwamba ni mengi waweza kuyafanikisha pale tu Mungu
akiwa nawe kuliko ukiwa wewe kama wewe. Musa tangu utoto hadi miaka 40
alipoanza kupata mzigo wa kuwasaidia wana waisraeli hakuenenda katika wito huu baada
ya utisho, hofu na woga bali alikimbilia Midiani na huko ikamchukua miaka 40
tena, hakuna makubwa aliyoyafanikisha maishani mwake hadi alipofikisha miaka 80
zaidi ya i) kumuua Mmsiri ii) kumuoa Siphora iii) kupata mtoto wa kiume, ambayo
hayo kama mafanikio yake yameandikwa katika sura (chapters) 7 za Biblia. Lakini
pale alipoingia kikamilifu katika wito wa Mungu alifanikisha mengi zaidi ya sura
(chapters) 37 za Biblia na pia aliweza kutusaidia wakristo wa sasa kwa kuandika
Torati yenye vitabu vitano (5) ambayo kwa hiyo tumeweza kumjua Mungu na
kuzitambua njia na hukumu zake Mungu.
Kwa hivyo
hii ni uthibitisho kuwa Mtu ukiwa na Mungu na huko Roho mtakatifu akikuongoza unatenda
na kufanikisha mengi zaidi kuliko pale ukiwa wewe pasipo Roho mtakatifu.
Sehemu
B: WAWEZA SAIDIKA NA USIYEMJUA KWANI MUNGU NJIA ZAKE HAZICHUNGUZIKI
Jina la Bwana lihimidiwe!, Kwa upande
wa pili wa neno hili twajifunza usimtende mabaya mtu usiyemjua wala kumdharau
kwa maana kama neno lisemavyo wengine walifanya hivyo kumbe walifukuza malaika.
Mungu hutuma msaada na kubariki kupitia wanadamu hakuna mtu aliyepokea baraka
isipokuwa kupitia wanadamu, Mungu mwenyewe akiri kupitia kinywa chako nitanena
na kupitia mikono yako nitabariki. Usimkwaze usiyemjua usijeukapoteza muujiza
wako, Mungu hutuma msaidizi kwa wakati sahihi na uliopangwa.
Tunaona wana wa Israeli kwa miaka zaidi
ya 300 walikuwa utumwani Mungu alifunulia Musa ili kwa huyo kwa kuambatana naye
wapate wokovu lakini alipoanza kufanya yaliyokusudiwa na Mungu hawakuona kwamba
yeye ni msaada. Ikawachukua miaka 40 kupitia shida ileile utumwani kwa kukataa
msaada walikuwa wanauhitaji, swala ni kwamba hawakutambua kuwa ndiye msaada
wao. Ipo gharama katika kupinga pinga kwa maana wapo waliopinga msaada au
baraka walioihitaji pasipo kutambua. Katika unyenyekevu kuna Faida kubwa na
dhawabu pia kwani waweza karibisha Baraka au msaada nyumbani kwako. Malaika
huwaelekea wenye uhitaji na uhitaji husomeka moyoni na sio usoni au jinsi mtu
alivyo. Unajua Musa alibeba nguvu za Mungu lakini kutokana na kupinga kwao
akaenda kukaa nazo sehemu isiyosahihi (midiani) kwa miaka 40 huku akifanya mambo
mengine kabisa tofauti na wito uliotengeza mzigo ndani yake juu ya ndugu na
kuwaacha wana waisraeli wote pasipo nguvu za Mungu za kuwasaidia kutoka
kifungoni.
Wanawaisraeli wasingempinga Musa na kuambatana
naye katika imani aliyokuwa nayo kusingekuwapo nguvu za wao kushikiliwa
utumwani, Wao walilaani na kulaumu ya kwamba Musa ndiyo aliyekuwa anawataabisha
na hiyo iliwachukuwa muda mrefu kufika nchi ya ahadi. Kwa maana hata
walipotolewa misri jangwani waliendelea na lawama hiyo na pia kwa kutokusadiki kwao
matendo makuu ya Mungu iliwagharimu miaka mingine 40. Kama Mungu aliona Musa
ndiye alifaa katika ukombozi huo na kuwaongoza, wanadamu ni nani hata waseme
hapana.
Mungu anatoa msaada kupitia mwanadamu,
kwa kuzuia kwako unajizuilia Baraka zilizoelekezwa kwako kwa maana kupitia
binadamu mwenzako Mungu atashusha Baraka. Imani ya matendo ni pamoja na
kumwamini aliyetumwa na Bwana, kuna dhawabu katika kumwamini roho wa Mungu,
Mti au jiwe mara nyingi msaada hauko
katika hayo bali mwanadamu na ndio maana hata Nabii eliya alipobaki mwenyewe
wengine manabii wakiwa wameuawa Mungu alisema nimejisazia watu 7,000 wenye utii
ambao nitawatumia pamoja na yeye kupata msaada.Amina!
No comments:
Post a Comment