#JAWABU LA KIU YAKO YOTE NI YESU WA NAZARETI

Jibu la kiu yako yote katika maisha ni Yesu wa Nazareti (Isaya 42:1-8); unadhiki, unataabu, umasikini, unamagonjwa, umpweke, hunaamani,umjane, uyatima, mwendee Yesu wa Nazareti na kumtegemea kwa kuwa anasema mtu akiona kiu aende kwake anywe, pia anasema; ”aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyohai itabubujika ndani yake” yaani yule roho mtakatifu (Yohana 7:37-39). Hivyo ndugu kwa nini kuwa katika shida, dhiki, taabu, umsikini, upweke, kutokuwa na amani hali Yesu wa nazareti ndio jawabu la mambo yote (Ufunuo 7:17 na Ufunuo 21:6). Katika yohana 4:7-16 tunasoma habari ya Mama Msamaria, Yesu wa Nazareti alimpa maji ya uzima yaliyomfanya asione kiu milele na pia alimponya na kumtakasa na dhiki zote akawa huru na amani ikawepo ndani yake, yaani yote ndani yake yakafanyika upya na ya kale yote yakafutwa (Ufunuo 21:4-5). Sema nami Ee! Yesu wa Nazareti nipe maji ya uzima ninywe nisione kiu milele, nipate raha na amani itokanayo nawe, huku nikiamini bubujiko la maji ya uzima wa milele ndani yangu litaponya magonja, litaondoa kwangu shida, taabu, umasikini, dhiki na karaha zote ziikumbayo dunia hii, niwezeshe Bwana Yesu wa Nazareti kuulinda moyo wangu kuliko vyote kwa maana ndiko zitokako chemichemi za uzima (Mithali 4:23). Amina

No comments:

Post a Comment