Mithali 22:6 inasema; “mlee mtoto
katika njia impasayo, naye
hataiacha, hata atakapokuwa
mzee”. Hivyo ni malezi ndiyo yafanyayo
watoto kuwa wema au wabaya au
watukutu, kumbuka huwezi
kuwatenga watoto na jamii, nchi
au dunia hii iliyojaa yote mema na
mabaya isipokuwa kwa kuwajaza
nguvu ya kushinda majaribu ya
dunia ambayo imo katika Neno la
Mungu.
Kwa habari ya Ibrahimu anasemaje
basi Bwana Yesu pale alipokuwa
akijiuliza amwambie au kumficha
Ibrahimu kuhusu kusudi lake la
kuteketeza Sodoma na Gomora;
Bwana anasema nimemjua ya
kwamba atawaamuru wanawe, nyumba
yake baada yake waishike
njia ya Bwana, wafanye haki na
hukumu (Mwanzo 18:19).
Kuhusu Mfalme Yoashi wa Israeli
alianza kutawala tangu akiwa na
miaka 7 na alitawala miaka 40;
Pale bibi yake yaani Athalia ambaye
alikuwa mtoto wa Ahabu and
Yezebeli alipotaka kuwa Malkia
aliwauwa watoto wote wa Mfalme
Ahazia mwanae, ambapo ni Yoashi
tu pekee alifanikiwa kutoroshwa
na shangazi yake na kufichwa kwenye
chemba za hekalu akiwa bado mtoto
mdogo na alifundishwa njia ya
haki ya Bwana na Kuhani Yehoyada
kwa miaka 6 hekaluni alimofichwa
na akaielekea njia hiyo akafanya
yaliyomema machoni pa Bwana kama
alivyofunzwa na kuhani, akatenda
yaliyo ya haki na hukumu kipindi
chote cha ufalme wake (2 Wafalme
11:1-12; 12:1-2).
Pia Modekai aliyemulea Esta
ambaye alikuwa yatima binti wa mjomba
wake, alimfundisha na kumkuza
katika maadili mema, naye akaifuata
njia ya Bwana akawa mwanamke
mwema na mwadilifu naye akayaishi
yote, akatenda haki na hukumu na
mwishowe akaiponya Israeli na
maangamizo yaliyokuwa
yamekusudiwa kwa hila na Hamani (Esta 2:7).
Kuhani Eli hakuwaonya watoto
kuhusu kuielekea njia ya haki laana
ikaifuata familia na uzao wake
ukaangamia naye Eli pia (1 Samweli
2:12; 3:13-14).
Lutu aliishi nchi ya anasa ya
sodoma na gomora lakini kutokana na
kutowanyoosha watoto wake njia ya
haki, pamoja na kuponywa na
Bwana na kiama ya moto; bado
wanawe dhamiri na nafsi zao
zilishikamana na yale yaliyokuwa
yakitendeka sodoma na gomora,
hawakushikimana na njia ya haki
nao wakazini naye akiwa amelewa
na kuzaa watoto wa kiume na baba
yao na habari yake Lutu ikaishia
hapo (Mwanzo 19:1-38).
Hata Paulo alitambua suala la malezi ya imani lilivyo na muhimu,
pale alipomwambia Timotheo (2 Timotheo 1:5-6); "nikiikumbuka imani
uliyonayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi,
na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo. kwa
sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani
yako kwa kuwekewa mikono yangu".
Hivyo ndugu ishike njia ya haki wewe na nyumba yake yote kwa
pale alipomwambia Timotheo (2 Timotheo 1:5-6); "nikiikumbuka imani
uliyonayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi,
na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo. kwa
sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani
yako kwa kuwekewa mikono yangu".
Hivyo ndugu ishike njia ya haki wewe na nyumba yake yote kwa
maana hakika zimwi likujualo
halikuli likakwisha hivyo suluhu ni Neno
la Mungu likae kwa wingi ndani
yetu na kwa watoto wote kwani
hakuna njia ya kupingana na
shetani na ufalme wake isipokuwa kwa
kuwa karibu sana na Mungu ile imani yako.
Wazazi tujifunze na tuwe kama
Yohana mbatizaji, tuiandae njia ya
Bwana katika familia zetu ili
watoto wamuishe yeye Kristo na siyo
kuvutwa na anasa za dunia ambalo
ni pando la adui shetani, yaani
awakute wakiwa wameandaliwa
nakujua Bwana Yesu hakika ndiye
Mungu.
Kwa maana kama wana wa Lutu
wangemjua Mungu yaani njia ya
kweli na haki ile dhambi ya
sodoma na gomora isingewafutilia mpaka
kule kwenye makao mapya. Kwa
hivyo suluhu nikuwa na nguvu ya
Neno la Mungu kumshinda shetani
ili awaonapo awakimbie; kwa
maana ni kwa Neno la Mungu
lililojaa ndani yetu tunampinga shetani.
Kumbuka kushindana na shetani ni
kushindana na ufalme wa giza
tunapingana nao, kwani pepo
akitoka huyu anakuja huyu kwa hivyo
suluhu ni moja tu we jaza Neno la
Mungu ndani ambalo ndiyo Mungu
mwenyewe; yaani Mungu Baba, Mungu
Mwana na Mungu Roho
Mtakatifu na hilo ndilo
litakalomuweka shetani na ufalme wake mbali
nao. Ndiyo! Neno la maarifa,
Biblia inasema tunaangamia kwa kukosa
maarifa, na maarifa ni katika
Neno la Mungu.
Sala; Mwenyezi Mungu niongoze
mimi kama mzazi kwa neema yako
niweze kuwalea watoto wangu
katika njia iwapasayo iliyo ya Haki ya
Bwana nipe hiyo karama Bwana Yesu
ili wadumu katika kweli na
mioyo minyofu siku zote za maisha
yao katika jina la Yesu Kristo wa
Nazareti, Amina.
No comments:
Post a Comment