#NI KWA JINSI GANI UTATHIBITIKA DUNIANI?

Hakika kuna mwanzo wa kila jambo, Mungu Baba anachagua kwa namna ya rohoni bali kuthibitika na kibali kwa wanadamu ni kupitia wanadamu.

Mungu Baba aliwachagua mitume wa Yesu wa Nazareti kwa namna ya rohoni kupitia sala alizofanya usiku kucha lakini Yesu mwenyewe aliwathibitisha asubuhi yake kwa maelekezo ya Roho wa Mungu kwa kuwachukua walewale ambao Mungu alimchagulia katika maombi yaKe ya usiku kucha (Luka 6:12-13). Na ndio maana katika Yohana 17:24 Yesu wa Nazareti anasema; "Baba, shauku yangu ni kwamba, hawa watu ulionipa wawepo mahali nilipo ili waweze kuona utukufu wangu; utukufu ambao umenipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ulimwengu haujaumbwa".

Pia tunajua hata Yesu wa Nazareti kuja duniani ilimpasa kupita kwa Bikira Maria na Yosefu (wanadamu) wanaonekana ambao hata asili zao zinajulikana kwa wengi na Yohana Mbatizaji amlitangulia ili kutengeneza njia yake na kumthibitisha kwa Waisraeli, hii yote ili dunia ipate kuisikia kwake habari njema kutoka kwa Mungu Baba lasivyo hakuna mwanadamu angemuona ndiyo mapenzi ya Mungu hayo na ndio maana imeandikwa Mungu ni pendo. Katika (Matendo 9: 10) Mtume Paulo baada ya Yesu kumfanya chombo chake Ilibidi Anania mwanafunzi wa Yesu kumfungua na kumbatiza ili ajulikane Yu katika kusudi moja na mitume na wanafunzi wengine wa Yesu. Kuna mwanzo wa kila kitu na mwisho wake ajuaye ni Mungu, kitu alichoweka Mungu ndani yako ni kupitia wanadamu kitathibitishwa katikati ya ndugu sawasawa na Neno la Bwana ili mataifa wapate kuamini ujumbe wako. Na ndio maana alikuwepo Yohana mbatizaji aliyeianda njia ya Bwana, naye anashuhudia alikuja kubatiza kwa maji ili watu wa Israeli wapate kumjua Kristo (Yohana 1:31), Pia Joshua alipata kibali na wana waisraeli walimtii baada ya Musa kumuwekea mikono na kumthibitisha kwao (Hesabu 27:18-20), hivyo hakuna mwanzo usio na mwanzilishi ila mwisho aujuaye ni Mungu pekee. Daudi alijitambua kuwa Mungu ndiye msaada wake na ndiye amuwezeshaye hata kabla ya kujulikana kwake na wakuu na wana waisraeli wote na hata kabla ya kuwa mfalme, lakini ili ajulikane kwa wanaisraeli ilimbidi Samweli ampake mafuta ili kumthibitisha rasmi sawasawa na Neno la Bwana, mengineyo kwake ilikuwa ushuhuda ingawa kwa waisraeli ilionekana kama ndiyo anaanza katika nafasi yake yaani bado hajakamilika hali yeye alijijua yuko kamili tangu kitambo ila wakati wa Bwana na kusudi lake ulikuwa bado haujafika (1 Samweli 16:13). Ni vema kumwamini aliyetumwa na Mungu na kazi azitendazo (Yohana 6:28-29) ili nawe uthibitike maana hata yeye kuna aliyemthibitisha mbele za wanadamu na ndipo utakapotumika kwa kiwango Mungu alichokusudia ndani yako. Hivyo heshimu waliokutangulia uthibitike, Nasema tena mwamini Yesu wa Nazareti utathibitika duniani hakika, Amina.