High season(nyakati ya utele) kwa kila mwanadamu chini ya jua ni haki ya msingi na ya upendeleo kutoka kwa Bwana ila sharti uitambue ili iwe ya manufaa kwako na kizazi chako. Kuna majira ya kila jambo chini ya
jua, na majira ya mwanadamu hayalazimishwi wala kuzuiliwa na
yeyote, katika Luka 9:44-45 tunaona Yesu Kristo akiwaambia wanafunzi ya kuwa, “
Yashikeni maneno haya masikioni mwenu,........ Lakini biblia inasema "hawakufahamu neno lile, likafichwa kwao wasilitambue...”. Ona sasa pasipo
majira kutimia hakuna namna mwanadamu anawezapata ufahamu wa jambo, suluhisho
ama taarifa inayomuhusu na kuielewa ama kuiamini kabisa mpaka majira rasmi
ndipo huwa nguvu kwake.
Luka 19:42-44, Yesu Kristo anasisitiza na
kuhuzunishwa kuhusu wanadamu na utambuzi wa majira rasmi. Mhubiri 3:1-8, Mfalme
Sulemani anasisitiza ya kwamba ziko nyakati tofauti mwanadamu anapaswa kufahamu
ili aishi vyema na kimafanikio kabisa.
Isaya 61:1-2, Yesu Kristo mwenyewe anatoa tamko
kwamba amekuja kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, sasa hayo ni majira na
tunaona vyema kabisa baada ya tamko hilo alilolinena hekaluni mbele ya viongozi
wa dini wote, mambo ambayo alikuja kuyatenda baadaye yakaja kuwa gumzo katika
nchi yote. Lakini ukifuatilia kabla ya tamko hili utaona alikuwa akiombwa
kufanya jambo kwa uweza ndani yake alikataa na kusema saa yangu bado. Hivyo
basi hakuna mwanadamu anayeweza kufaulu, kuvuka, kushinda, kufanikiwa pasipo
kujua majira ya Bwana katika maisha yake.
Na ndio maana mhubiri 9:11 anasistiza kuwa
wakati na bahati huwapata wote, sio uwezo wako bali wakati uliopangiwa au
kuamuriwa na Bwana ndio dira ya mafanikio ili kuifikia ile hatma yako.
Siri ya majira ni kwamba pale unapoyatambua majira
ni mwanzo mpya wenye hatma yako.
Kutambua majira hutengeneza utayari ndani ya
mwanadamu.
Kutambua majira huimarisha imani ya mwanadamu.
Kutambua majira humfanyia mwanadamu focus ya
maisha sahihi.
Kutambua majira ni mwanzo wa hitimisho la jambo
lililokusudiwa na Bwana.
Hata Malaika mwenyewe hawezi zuia majira yako
isipokuwa mwanadamu mwenyewe.
A] FAIDA ZA KUTAMBUA MAJIRA KWA MIFANO YA
BIBLIA
Mfano wa watu wa
Mungu katika Biblia ambao walitambua majira ya Bwana wakabarikiwa na
kuneemeshwa na Bwana;
Ibrahimu, Mordekai/Esta (Esta 4:13-14), Mama
Mshunani ( 2 Wafalme 4:2, 8-36 (10)), Koreshi (Ezra 1:!-12, 2 Nyakati
36:22-23), Mama wa Sarepta – Mjane (1 Wafalme 17:9-24), Daniel 9:2-27, Wenye
ukoma wane (2 wafalme 7:3), Nehemia 1:1-5, Nuhu (Mwanzo 6), Henoko (Mwanzo
5:21-24), Musa (Kutoka 2:11-15), Hanna (1 Samweli 1:9-20), Elisha (1 Wafalme
19:19-21 na 2 Wafalme 2), Mamajusi (Mathayo 2:1-2), Wachunga kondoo (Luka
2:8-18), Simeoni na Anna Fanueli nabii mke (Luka 2:25-38).
B] ATHARI ZA KUTOTAMBUA MAJIRA KWA MIFANO YA
BIBLIA
Baadhi ya mifano ya watu wa Mungu ambao kwenye
biblia walipata hasara, walikosa walivyopasa kupata, walijuta ama kuathirika
vibaya baada ya kutokutambua majira rasmi ya Bwana;
Kaini, Esau, Mfalme Sauli, Akida (2 Wafalme 7:3), Zakaria (Luka
1:11-23), Samsoni (Waamuzi 14), Petro, Paulo, kaka zake Yusufu na kaka
zake Daudi.
Pasipo kutambua majira sahihi kuna uharibifu wa
nafsi ya mwanadamu, na ucheleweshwaji wa Baraka pia. Kuna usemi usemao “Ignorance
of law has no excuse, no defence”, yule asiyeyatambua majira yake hana pato bali
kukabiliana na hasara na matokeo yatokanayo na upuuzi huo, hivyo basi nami nasema kutokujua
majira sio ngao ni kwamba utakosa ulichopaswa kupata na kuishi maisha yasiyokusudiwa na Bwana i.e. utatembea jangwaani na gizani kwa kule kutokujua majira.
Wanadamu mara zingine hawatambua majira yao
rasmi kwa sababu ya kupuuza nyakati, kufungwa na nguvu za giza, laana zitokanazo na maagano ya mizimu, matambiko ya ukoo, nira za kichawi na kiganga, ibada za sanamu na miungu, kughairi pindi wapatapo misukosuko, kutochukua
hatua sahihi, kukosa washauri na baba wa kiroho ama kutowashirikisha wenye uelewa,
kutokuwa na kawaida ya kusali mara kwa mara yaani kujiweka karibu na Mungu huku
ukidumisha uhusiano imara na roho mtakatifu, au kule kutotambua saa ya
kutembelewa na wenyeji wa mbinguni (heavenly visitations).
Lakini ukweli ni kwamba kama wanyama ama mimea
ama miti hutambua majira rasmi na kujiongeza sawasawa na vile ilivyokusudiwa na
Bwana, Je? Si zaidi wanadamu wenye utashi kamili kuzidi wao. Na hii ni kweli
kabisa hata nyumbu hutambua majira rasmi na kuchukua hatua stahiki kulinda uhai
wao.
Mpendwa katika Bwana, kama vile Yesu Kristo
alivyosema katika Luka 19:42-44, ya kwamba laiti
ungalijua siku na saa ikupasayo amani wewe msomaji wangu ungalichukua hatua
muhimu sasa kumuelekea yeye atoaye uzima bure, amani bure, afya bure na tiketi
ya kuingia mbinguni bure kabisa. Chukua hatua sasa ambayo ni muhimu sana kwa
maisha yako kwa kumfanya Yesu Kristo Bwana na mwokozi wa maisha yako hakika
yaliyofichwa yatafumbuliwa kwako, na hatua yako yaani huo utayari wako na
uamuzi wako ni dhahiri kwamba hatma yako ni njema kabisa na nuru ya Bwana
imeangaza kwako sasa (Isaya 60:1) Arise Shine!!, Hallelujah!!, Amina.
Amen
ReplyDeleteAmen
ReplyDelete