Wokovu ni pasipoti inayotufanya kuwa raia wa ufalme wa mbinguni,
Wokovu ni cheti cha uraia wa mbinguni
na nchi ile mpya ijayo, na wokovu ni kwa neema ila unathibitika katika haki ambayo i
katika matendo mema tuyatendayo zile dhamiri zetu kuwa safi (chumvi safi). Kaa ukijua ya kuwa pia Mwanadamu kama Mwanadamu kamwe hawezi kuwa mtii wala mnyenyekevu mbele za Mungu na pia hawezi kuwa mchaji wa Mungu pasipo neema ya wokovu katika maisha aishiyo, la sivyo ni ubatili tu kwani tunafanyika raia na twaishi kama raia wa ufalme wa Mungu kwa Nguvu inayotuwezesha kuwa hivyo wala usidanganyike kwamba unaweza kwa kujinyenyekeza tu pekee au kujifanyisha mtakatifu ni ngumu sana papsipo Neema ya Mungu (Yohana 1:12).
Sisi si wa ulimwengu huu (Yohana 17:14)
Yesu wa Nazareti anasema;”Nimewapa Neno lako nao ulimwengu umewachukia kwa kuwa
wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu huu.”Na pia katika Yohana
17:16 Yesu wa Nazareti anasema“Wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa
ulimwengu.”
Na ndio maana katika (Mathayo
17:24-27); Inazungumzia Swala la Yesu wa Nazareti kulipa kodi kwa maana
sio raia, ndipo Yesu akamuuliza waonaje Simoni?
Wafalme wa dunia hupokea kodi ama ushuru kwa watu
gani? Kwa wana wao au kwa wageni? Petro akajibu kwa wageni ndipo Yesu akasema
kwa hiyo wana wao huwaacha huru pasipo kulipa?, Yesu wa Nazareti akasema ili tusiwakwaze
akamtaka Petro akavue kwa ndoano samaki na yule wa kwanza kuvuliwa afumbue
mdomo wake atoe shekeli na akalipe kwa ajili yake na Yesu kwa kuwa si wa
ulimwengu huu. Hivyo baada ya wokovu, kuishi kwako duniani ni kama kwa mtu wa
kuja asiyetakiwa (chumvi), kwa maana kupingwa kwake ni kutokana na kuwa kuja
kwa kweli huleta hukumu hivyo wengi wapinga kwa sababu kwa kweli ya Mungu unawahukumu
lakini siku zote penye kweli Mungu yupo na atakupigania ndio maana hata Yesu wa
Nazareti pamoja na kumpinga kwote lakini hawakuweza kumzuia kuinena kweli mpaka
wakati ulioamriwa na Mungu.
Siku zote
asiye raia hupingwa na raia labda ampendezeshe au amlembe yaani afanye vile
raia wapendavyo (awe chumvi iliyoharibika), Ujio wa Yesu wa Nazareti ulipingwa
hata kabla ya kuzaliwa kwake kutokana na kuwa Mungu alikuja duniani kuhukumu
wenye dhambi kwa kuifunua kweli yake na yeyote aiaminiye anapata uzima wa
milele lakini kwa asiyeamini hukumu.Hata kama shetani (Mshitaki wa Ndugu, Mr.
Lawama, Mr. Kushindwa) alikuwa anataka kumuelezea Mungu kuwa sheria na amri
zake ni ngumu kuzitimiza na kuzitenda ili awe na haki katika kuasi kwake lakini
sasa kwa kuja Yesu wa Nazareti; Mungu kuishi kama mwanadamu katika aina yote ya
maisha Shetani amekwishahukumiwa kwani Yesu wa Nazareti (Adam wa pili)
alithibitisha kuwa amri na sheria za Mungu zaweza kutimizika na kutendwa kwa namna ya Roho Mtakatifu kule yeye
kufanyika mfano kama mwanadamu. Shetani hata kabla ya kuzaliwa kwa Yesu wa
Nazareti alijua kuwa huyo anakuja kutangua mashitaka yake mbele za Mungu apate
hukumu na ndio maana anaharibu wanadamu wengi kwa kuwafanya watumwa wa dhambi
zake ili asionekane kuwa ni yeye tu aliyeshindwa kutii na kutenda amri na
sheria za Mungu. Ukisoma Biblia inaonyesha kuwa kuzaliwa kwake ilikuwa muujiza
kwani watoto wote wa kiume pamoja naye, ilitolea amri na Mfalme Herode kuwa wauwawe
huku tajeti ikiwa ni Yesu wa Nazareti ndipo malaika wa Mungu akamwambia Yusufu
kuwa mtoto apelekwe Misri mpaka Mfalme Herode akifa ndipo aletwe (Mathayo
2:7-23). Ujio wa Musa pia ulipingwa na Farao wa Misri kwani waisraeli wote
walikuwa kwenye kongwa zake yaani watumwa wake hivyo kwa kuwa Musa alikuja kama
mkombozi wa waisraeli kuwapeleka nchi ya ahadi (kama sisi tulivyoahidiwa
Yerusalemu mpya) Farao aliwataka watoto wote wa kiisraeli wauawe huku tajeti
ikiwa ni Musa lakini Mungu alimponya kwenye kisafina (Kutoka 1:15-16 na 2:1-10)
akaja kuwa mkombozi wa waisraeli. Hivyo Mungu akiwa upande wako utapingwa kwa
kuwa sio raia wa dunia lakini hutashindwa utavuka tu kwani wewe ni kusudi kwa
Mungu lakini kama Biblia itusisitizavyo kuwa tushike sana tulivyonavyo asije
mwovu akatunyang’anya mataji yetu (Ufunuo 3:11). Pia tunamsoma Yusufu alikuwa
akiishi vizuri na ndugu na familia yake kwa ujumla lakini siku tu Mungu
alivyokuwa upande wake na kumfunulia mambo makubwa na kumfanya mkuu (raia wa ufalme wa mbinguni) ndugu zake na familia yote wakamchukia (Mwanzo 37:15-28) badala ya
kumfanya msaada wao lakini pamoja na chuki zao baadaye wakaja kuinama mbele
zake kama mkuu wao na kuupata msaada wake. Hivyo yote utendewayo Mungu akiwa
upande wako yatakuja kudhihirika hapa hapa duniani na itajulikana kuwa Mungu
hakuwa kwa watesi wako bali upande wake na Neno lake Mungu juu yako
litathibitika na watesi wako watahitaji uwasaidie. Na kwa kuwa wewe sio raia wa
dunia hata maongezi yako, ushauri wako, hekima zako, busara zako kwao
wasioamini huonekana kuwa vita kwa ajili ya ile kweli ya Mungu na ndimi zao kufarakanishwa
kama Yesu wa Nazareti alivyosema unadhani nimekuja kuleta amani duniani, la
hasha! Bali moto, upanga na mafarakano kwa maana ndugu watafarakana kwa ajili
ya kweli baba na mwana hwataelewana (Mathayo 10:34, Luka 12:49 na Luka 12:51).
Tunasoma pia (1 Wafalme 22:13-38) kwa habari ya Nabii Mikaya na Mfalme Ahabu
alisimama katika kweli ya Mungu kinyume na manabii 400 wa mfalme Neno lake
Mikaya Nabii lililokweli ndio lililosimama mpaka mwisho pamoja na shida na
taabu zote alizopata, Pia (1 Wafalme 17:1 mpaka 2 wafalme 2:11) kwa habari ya Nabii
Eliya na Mfalme Ahabu na Yezebeli mkewe alisimama katika kweli ufalme ukampinga
na wala hakupendwa nao lakini mpaka mwisho kwa kuwa alikuwa raia wa mbinguni na
anayo ile pasipoti alitwaliwa na Mungu, Pia Nabii Isaya shida na taabu
alizopata ni kutokana na kweli aliyoibeba ilihukumu watawala wa dunia
hawakumfurahia wakamuuwa kinyama. Naye Samsoni Mnadhiri wa Mungu kwa kupenda
kwake haki alisimama mwenyewe katika Israeli Mungu akawa pamoja naye na
wafilisti walimchukia na kutafuta kummuua kwa kuwa waliwafanya waisraeli
watumwa wao (Waamuzi 15:11). Katika Yohana 17:9 Yesu wa Nazareti anasema;”Mimi
nawaombea hao, siuombei ulimwengu bali hao ulionipa kwa kuwa hao ni wako”, tunafanywa
raia wa mbinguni kwa kuwa wana wa Mungu, ulimwengu unatuchukia kwa kuwa Bwana Mungu
kwa neema ametuchagua na anatuombea tuponywe na dhiki ya ulimwenguni. Hivyo
hatupendwi wala kufurahiwa kwa sababu sisi ni raia wa ufalme wa mbinguni na wala si
walimwengu, ukichukia uovu (shetani), uovu utakuchukia kwa sababu dunia ndiko
kuliko kitovu cha uovu kwa kuwa mkuu wa dunia hii aliyekwisha hukumiwa ni
mwanzo wa huo. Dunia hii imeshachakachuka haihitajiki mbele za Mungu (lakini
ipo neema ya Mungu kwa waaminio hupata wokovu na kuponywa na dunia) na ndio
maana siku ya mwisho dunia hii itaondolewa yote na kutupwa motoni na wote waipendayo na
vyote viijazavyo na kisha zitafanywa mbingu mpya na nchi mpya halafu itakuja Yerusalemu mpya ule mji wa Bwana wa wateule
wake wote (Ufunuo 21:1-7). Lakini kaa ukijua siku zote masihi wa Mungu haguswi
Mungu akiwa upande wake, Tunamsoma Danieli pia Meshaki, Shedraki na Abedinego,
Danieli alisimamia kweli mpaka mwisho Mfalme Nebukadineza akaamini na kumtii na
kukiri kuwa hakuna Mungu kama amwabuduye Danieli, watawala chini yake
wakafarakana na Danieli kwa ajili ya ukuu ndani yake lakini mwisho alishinda(Danieli
6:3-24). Danieli walimuita Beltashaza katika ufalme wao,jina hilo hakushikamana
nalo na halikuzoeleka isipokuwa Meshaki(aliyeitwa
awali Mishaeli), Shedraki(aliyeitwa
awali Hanania) na Abednego (aliyeitwa
awali Azaria) majina hayo
yalishikamana na huo ufalme (Daniel 1:6-7) na ndio maana hata sanamu ya mfalme
ilipotegenezwa (Danieli 3:1-27) Meshaki, Shedraki na Abedinego ndio
walilazimishwa kuiabudu na siyo Danieli, kwa hiyo pia kataa vyote visivyotokana
na Mungu vilivyo vya dunia ili dhambi zao zisishikamane nawe wakapata kukutia
hatiani. Amina