#SHETANI SI KITU BALI MUOGOPENI MUNGU

   Wa kuogopwa ni Mungu katika matendo yetu, utii wetu na unyenyekevu wetu. Kwa maana hata katika Mathayo inaelezea kuwa wa kuogopwa ni Mungu ambaye hata shetani mwenyewe atamuangamiza, kule kutaabisha miili yetu si kitu, tuwathamani sana mbele za Mungu, tunalindwa naye Kiroho kwa maana ikiwa mbayuwayu kwa wingi wao katika kundi lakini hawezi anguka hata mmoja akauzwe kwa nusu sarafu kama Mungu baba asipopenda, je’si zaidi kwetu sisi ambao hata nywele za vichwani zimehasabiwa.

Mathayo 10:28-31;”28 Msiwaogope wale wawezao kuua mwili lakini hawawezi kuua roho; ila mwogopeni yeye ambaye anaweza kuiangamiza roho na mwili katika moto wa Jehenamu. 29 Mbayuwayu wawili huuzwa kwa sarafu moja tu. Lakini hata mmoja wao hawezi kuanguka pasipo Baba yenu kupenda. 30 Hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa. 31 Kwa hiyo msiogope; kwa maana ninyi mna thamani kubwa zaidi kuliko mbayuwayu wengi”

Pia katika Ufunuo inasema malaika mmoja aliyeshika funguo za kuzimu na mnyororo mkubwa mkononi mwake atamfunga miaka 1000 yule Joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni ibilisi na shetani na kumtupa kuzimu,na kumtia muhuri juu yake asipate kuwadanganya mataifa tena.

Ufunuo 20:1-3;“Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena,…………………

Kwa hivyo shetani si kitu kama ni malaika mmoja amshika na kumfunga kuwapi nguvu ndani yake za kutetemesha duniani kuifanya dunia imuhofu kana kwamba yeye ni mkuu sana, Hivi ndugu usiogope kwa maana tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na ng’e na nguvu zote ndani ya yule adui (shetani) na wala hakuna chochote kitachoweza kutudhuru(Luka 10:19).

Biblia pia katika Isaya inazungumzia kuwa baada ya huzuni yako na baada ya taabu yako na baada ya utumishi mugumu uliotumikishwa Bwana (Yesu wa Nazareti) atakupa raha, mtesi wako (shetani amekushindwa) kwa kuwa Bwana Yesu wa Nazareti yuko nawe. Naam dunia itataharuki nawe ukimwona shetani utamkazia macho, utamuangalia sana ukisema, Je! huyu ndiye aliyekuwa ananitesa, ananihuzunisha na kunitaabisha katika maisha yangu, huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, na ndiye aliyetikisa falme,? Hivyo utajisikitikia sana na kujilaumu kwa woga wako wa kumhofu kwani ukishamjua Yesu wa Nazareti na kumfanya kinga yako shetani mdogo sana awezwaye hata na mtoto mdogo.

Isaya 14:3-19;”Tena itakuwa katika siku ile, ambayo Bwana atakupa raha baada ya huzuni yako, na baada ya taabu yako, na baada ya utumishi ule mgumu uliotumikishwa; utatunga mithali hii juu ya mfalme wa Babeli, na kusema, Jinsi alivyokoma mwenye kuonea; Jinsi ulivyokoma mji ule wenye jeuri! Bwana amelivunja gongo la wabaya, Fimbo ya enzi yao wenye kutawala. Yeye aliyewapiga mataifa kwa ghadhabu, Kwa mapigo yasiyokoma; Aliyewatawala mataifa kwa hasira, Ameadhibiwa asizuie mtu. Dunia yote inastarehe na kutulia; Hata huanzilisha kuimba. Naam, misunobari inakufurahia, Na mierezi ya Lebanoni, ikisema, Tokea wakati ulipolazwa chini wewe, Hapana mkata miti aliyetujia. Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi. Hao wote watajibu na kukuambia, Je! Wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi! Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika. Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo. Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme; aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao? Wafalme wote wa mataifa wamezikwa wote kwa heshima, Kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe; Bali wewe umetupwa mbali na kaburi lako, Kama chipukizi lililochukiza kabisa; Kama vazi la wale waliouawa, Wale waliochomwa kwa upanga, Wale washukao mpaka misingi ya shimo; Kama mzoga uliokanyagwa chini ya miguu.”

Sema nami hivi; kuanzia leo ewe shetani! na ufalme wako wa giza wewe si kitu kwangu nimepewa mamlaka ya kukushinda hivyo siku zote ntakukanyaga kichwa mpaka ukome, Amina.

No comments:

Post a Comment