Kama vile ilivyokuwa kwa Kornelio; Jemedari wa Kikosi cha Italia katika Matendo
10:1-4, nasi tunapandisha na kupeleka sala zetu kuelekea juu sana pasipo kuchoka ambazo ni za
kukumbukwa na kuwa manukato mbele ya Mungu; Ili ya kwamba kwa sala zetu hizo Mungu aweze
kushuka kutuponya, kutuweka huru na kutubariki. Kwa maana katika hili
hakuna mafarakano wala matengano kama ilivyotokea walipokuwa wanajenga mnara wa
babeli ( Mwanzo 11:7-9) bali ni maelewano, kunia mamoja na kuwa na umoja katika
kristo yaani mwili mmoja unaoshirikiana kwa sauti moja ya Roho mtakatifu kupitia sala zetu (Matendo
2:1-4). Kilichotokea wakati wa ujenzi wa mnara wa babeli, walikusudia kutenda
hivyo ili wakamwone Mungu lakini kusudi lao halikuwa mpango wa Mungu naye
akawasambaratisha kwa kuwachafulia usemi wasielewane yaani wasinie mamoja,
lakini sasa tunalotumaini kupitia Yesu kristo aliyetuunganisha na Mungu kwa
upya ambapo kwa sala zetu Mungu hushuka katika yetu kwa utukufu wa jina lake.
Hivyo ijapokuwa ndimi zaweza kutofautiana; yaani zile
lugha tutumiazo katika kuwasiliana Roho Mtakatifu aliye mmoja ndiye atuwezeshaye
sote kuwa wamoja. Ujasiri upo; sala zetu na ziwe kama mnara unaelekea juu sana
kwa Mungu mwenyezi ili kupitia hizo Mungu atukuzwe na kushuka na kufanya makao
ndani yetu kwa njia ya Roho mtakatifu, katika jina la Bwana na mwokozi wetu
Yesu Kristo wa Nazareti, Amina.
No comments:
Post a Comment