Ndugu wa kweli ni kimaanisha ndugu wa damu, kila mwanadamu ana ndugu wa damu ambao kwa hao ameunganishwa nao iwe kwa kuzaliwa pamoja, ama wazawa wa walio ndugu upande wa baba na wa mama hii hudhihirishwa kwa kushabihiana kwa baadhi ya tabia zao, sura zao, kimuonekano na mifanano mingine mingi ya ndani na nje ya mwili inayoonyesha muunganiko wao kama ndugu. Sasa kwenye sayansi kuna kitu
huzungumziwa sana kinachoitwa “DNA”
ambacho ndicho kipimo kitumiwacho kutambua "vinasaba" kati ya mwana-damu mmoja na mwingine kama kweli ni ndugu yako awe mwanao, kaka, dada, binamu,
baba, mama, shangazi, mjomba na ndugu wote wa damu. Na ukisoma Torati ya
Musa kwa umakini katika Biblia kitabu cha mambo ya walawi
25: 47-52 (soma sura ya 25 yote) inasema hakika haiwezekani kabisa mtu
asiye ndugu yako kukukomboa na sisi tunakiri ya kuwa Yesu Kristo wa Nazareti
alitukomboa sisi kwa damu yake na kwa mauti ya msalaba.
Je, kwa hivyo twaweza sema Yesu
wa Nazareti ni ndugu yetu? Kwa maana ndiye aliyetukomboa utumwani wa dhambi, na
je ni ndugu yetu kweli?.
Hapo utaona inachanganya sana
lakini nikusihi hivi, ukitafakari kwa kina Neno la Mungu na kwa sala ndipo
utajua Yesu Kristo wa Nazareti ni ndugu yetu hakika, kwa kuwa biblia imethibitisha
hivyo;
v katika
kitabu cha waefeso 4:6 kuwa Yesu wa
Nazareti ni Baba yetu, Baba wa wote.
v Na
katika wagalatia 4:19 biblia
takatifu inasema Yesu wa Nazareti ni mama yetu aliyetuazaa (tulizaliwa mara ya
pili katika Yeye).
v Katika
kitabu cha mithali 7:3-4 biblia
takatifu inasema Yesu wa Nazareti ni dada yetu
v Katika
kitabu cha Waebrania 2:11 biblia
takatifu inasema Yesu wa Nazareti ni kaka yetu
v Katika
kitabu cha Mambo ya Walawi 25:49
biblia takatifu inasema Yesu wa Nazareti ni binamu yetu na mjomba wetu
Kwa hiyo sasa twatambua hakika
yakuwa yeye Yesu wa Nazareti ni vyote katika vyote, kwa namna ambayo biblia
takatifu katika waefeso sura ya 4:8-10 inasema kitu kimoja cha
kushangaza ya kwamba yeye Yesu wa Nazareti alienda juu sana kupita mbingu zote,
kwa hiyo yuko juu ya vyote, na pia biblia takatifu (1 Timotheo 2:5) inasema yeye ni mpatanishi na mwakilishi wetu kwa
hivyo yuko katikati yetu, na tena inasema (1
Wakorintho 3:11)yeye ni msingi wetu kwa hivyo yuko chini pia. Siyo hivyo tu
bali biblia kwenye kitabu cha ufunuo 1:8;
1:17 inasema kitu kimoja cha ajabu sana kuwa yeye Yesu wa Nazareti (Kristo)
ni Alfa na Omega, ndiye mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho kwa hivyo yuko
katika miisho yote. Na biblia takatifu inamalizia katika 1 Wakorintho 6:17 kwa kusema yeye yule aliyeungwa na Bwana Yesu
Kristo wa Nazareti ina maana baada ya wokovu ni roho moja naye ikimaanisha, ule
wokovu wake mkuu kama ndugu yetu unakufanya kuwa zaidi ya ndugu yaani ni roho
moja naye na hapo huwezi kutofautishwa naye.
Hivyo niwaambia ndugu zangu huyu
Yesu Kristo wa Nazareti ninayemtaja hapa hakika ni mkombozi wa dunia kwa kuwa
anakidhi na kutimiza yote yamfanyao ndugu yetu na mkombozi wetu, tambua leo,
kata shauri dakika hii, amini na amua sasa naye atakuweka huru huru kweli nawe
utaishi katika neema yake maisha yako yote hutasaritiwa naye kamwe kwa kuwa ni
baba, ni mama, ni dada, ni kaka, ni binamu na mjomba, ni wa juu sana, uu kati
yetu na chini pia na pale tu ukiamua kuokoka wawa roho moja naye yaani zaidi ya
ndugu wala huwezi kutofautishwa naye.
Okoka leo kwa uweza wa roho
mtakatifu naye atakukomboa hakika na atakutenga na dhambi zote ulizokuwa
umefungwa nazo maishani mwako, amina.