#ALICHOANZISHA YESU WA NAZARETI NDANI YAKO ATAKIKAMILISHA

       Uumbaji ni karama ambayo Mungu ameweka kwa kila mwanadamu aliyemuumba kwa sura na mfano wake.
Mwanzo 1:1-5 inazungumzia kuhusu Mungu kuumba mbingu na dunia, na ya kwamba dunia ilikuwa pasipo na umbo la kueleweka na ikawa ni giza tu ambalo lilitanda uso wote wa dunia yaani ni kweusi tii na roho wa Mungu alikuwa juu ya maji, ndipo Mungu akasema kuwe na Nuru ikawa Nuru, na Mungu alipoona ya kuwa Nuru ni nzuri akatenganisha nuru na giza kwa kuita nuru mchana na giza usiku, na ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza.

Biblia inasema dunia ilikuwa haina umbo la kueleweka na ikiwa na giza tu….. na roho wa Mungu alikuwa juu ya maji akisubiri neno kutamkwa apate kulitekeleza na vyote vilivyotamkwa ikawa hivyo. Mungu alisema na kusema vitu vikawa. Sasa dunia ina maana ilikuwa iko hovyo hovyo haina kitu na imepungukiwa vitu fulani fulani ni kama vile injinia ambaye Mungu kampa ufahamu wa kumuwezesha kuunda vitu ambavyo hata mioyo yetu inakiri kuwa ni vizuri na wengine kushangazwa navyo. Pointi yangu ni kwamba, Mungu anaanza na kitu kutoka katika ubaya wake jinsi kilivyo kuwa kitu kizuri, kutoka kutokuwepo mpaka kuwepo, kutoka katika upungufu wake hadi kukamilika kwake, kutoka hakuna mpaka kuwa nacho na hashirikiani utukufu na wengine iwe miungu au yeyote au chochote chenye jina lolote lile isipokuwa jina la YESU. Hatua aliyoanza nawe katika maisha yako inaashiria kuwepo hatua zingine mbele yako mpaka ukamilifu wako hadi atakavyoona kuwa ni nzuri na kumbuka siku zote mtu ambaye Mungu amemchagua na kumuokoa atathibitisha uchaguzi wake ambao Bwana ameufanya. Katika yeye hakuna mpango unaoisha pasipo kukamilika lakini kumwamini yeye ndiyo msingi mkuu, akianza nawe chini atakufikisha Juu na kwake hakuna kurudi nyuma, labda wewe mwenyewe kwa kutokujua kwako ulivyojulishwa na kwa kukosa maarifa kwako iwe sababu. Hatua kwa hatua maana yeye ni Mungu mwenyezi ambaye yupo siku zote hajawahi kusahau au kufutilia mbali mpango wake wala kutokuwapa hatua mpya kila iitwavyo leo kwao wamnyenyekeao na kumtii kama ilivyokuwa kwa kristo aliyefanyika mfano kwetu, Amina.

No comments:

Post a Comment