Roho mtakatifu huja
kwa wana kama msaidizi ambapo kwa huyo tunalia, Baba! [Warumi 8:15]. Kwa hiyo
kama Roho mtakatifu akikujia maana yake wewe ni mwana wa Mungu, na tunajua na
kufahamu vizuri kabisa uhusiano kati ya Baba na Mwana upasavyo kuwa, kwa hivyo
acha kuishi kama yatima, usiishi kama Mwanadamu aliyepokea roho ya kitumwa
yaani roho inayomfanya kuwa mtumwa inayompelekea kuwa na hofu tena kama ya
zamani pengine na kuzidi. Biblia katika Yohana 1:12 inaeleza ya kwamba kwa wale
wote waliompokea YESU KRISTO wa Nazareti, aliwapa uwezo/Nguvu ya kufanyika kuwa
Wana wa Mungu, na hata wale walioamini katika jina lake. Nguvu za Mungu zi ndani
yenu, nyie mlio wana wa Mungu, na tulichopokea kutoka kwa mwenyezi Mungu hakika
ni roho ya kutufanya kuwa watoto wa Mungu yaani Roho itupayo haki ya uwana.
Naam!
Kuna faida zipi katika kuwa na Roho mtakatifu ndani yako;
“Akija
yule Roho wa kweli atawaongoza muijue
kweli yote. Yeye hatanena kwa uwezo wake mwenyewe bali atanena yote
atakayosikia. Atawafundisha kuhusu mambo
yote yajayo. Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo
yangu na kuwaambia ninyi. Vyote
alivyo navyo Baba ni vyangu, ndio maana nimesema kuwa atachukua yaliyo
yangu na kuwaambia ninyi.” [Yohana 16:13-15]
Uwapo mwana wa Mungu,
vyote alivyonavyo Mungu huwa na haki navyo, yaani huwapa wana wavitumie. Hii ni
kwa sababu, u-wana kwa Mungu hukupa haki ya kufanyika mrithi pamoja na Kristo,
kwa Mungu wetu. [Warumi 8:17].
Hii ni kweli; Roho
mtakatifu yu ndani ya wana wa Mungu, je’ wewe ni mwana wa Mungu? Kumbuka wote
walio katika Kristo YESU wa Nazareti wana kibali hiki katika yeye [Waebrania
1:5].
Mpokee Yesu Kristo wa
Nazareti sasa!, kumpokea Roho mtakatifu na kuwa mwana wa Mungu hakika.
No comments:
Post a Comment