#KWA YESU WA NAZARETI HAUKO PEKEE YAKO HATA SIKU MOJA

      Hakika kwa Mungu hauko pekee yako Warumi 11:4-5; inazungumzia Masalia ya wana waisraeli. Neno linasema,Lakini lile jawabu ya Mungu yamwambiaje Eliya? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali, basi vivyo hivyo wakati huu wa sasa yako mabaki waliochaguliwa kwa neema. Lakini ikiwa ni kwa neema haiwi kwa matendo tena au hapo neema isingekuwa neema.

Kuwa pungufu ni kama asimilia 100 kamili kwa Mungu kuliko kule kujiona kamili, kwa sababu katika upungufu kuna ukamilifu wa kila kitu huku Mungu akitukutuzwa pasipo kujitukuza mwenyewe, huku moyo ukiwa mnyenyekevu, hofu ya Mungu na kumjua vizuri Mungu ni nani katika maisha yako. Napenda hili neno kutoka 2 wakorintho 12:9-10; linalosema”Neema yangu yakutosha maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu, basi nitajisifua udhaifu wangu kwa furaha nyingi ili uweza wa kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo nependezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba na adha na shida kwa ajili ya kristo, Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.”

Siku zote tunaangalia upande mkubwa wa tatizo litupatalo; lakini sio kwa Mungu wetu, Yeye huangalia ile sehemu kidogo ambayo kwa hiyo mavuno ni mengi na ushindi ni mkubwa. Ndiyo maana anaitwa Mungu wa yasiyowezekana; hebu jaribu fikiria sisi wanadamu tunafikiri jinsi maisha yetu ya baadaye yalivyo giza lakini yeye husema nuru kidogo uliyonayo itunze (Yohana 12:35) kwa sababu kupitia hiyo ishara, maajabu na miujiza ya kushangaza vitafanyika. Hivyo tusiangalie ule upande tuonaogiza tu katika maisha yetu na kuona kama mlima au kizuizi kipingacho mafanikio yetu tunahimizwa kuangalia nuru kidogo iliyodhihirishwa kwetu kwani kwa hiyo mambo ya ajabu yatatendeka. Ona Nabii Eliya alijiona amebaki mwenyewe anayeliitia jina la Bwana, lakini cha kushangaza Mungu akamwambia,”NIMEJISAZIA WATU ELFU SABA WASIOPIGA GOTI KWA BAALI.” kwa namna nyingine Eliya nabii alifikiri na aliona kuwa yuko mwenyewe na hakuna msaada duniani. Unajua saa nyingine uwadhaniao kuwa wako kinyume nawe Mungu anajua walio upande wako katika hao hata pasipo wewe kujua kwa sababu ya neema yake isiyoangalia matendo ya mtu. Neema ya Mungu huangalia walio wanyenyekevu wa mioyo hata walioupande wa adui na kuwabadilisha kuwa upande wako. Mungu anajua mambo kabla hayajatokea, Hebu fikiria kuhusu Sauli ambaye baadae aliitwa Mtume Paulo, alikuwa kinyume na injili ya Yesu kristo lakini kwa neema Mungu alimuona kuwa ni silaha ya nguvu ya kumpiga shetani na aliona hivyo hata kabla hajambadilisha na kumuokoa awe chombo chake kwani Mungu alijua Sauli ataibadili dunia kwa injili yake Yesu kristo.

Na Paulo mwenyewe akaja kusema nimemtumikia Mungu maisha yangu yote kwa dhamiri safi kwa sababu moyo wake ulikuwa tayari kutumika, tatizo mwanzo alitumika isivyo lakini baadaye alitumika kama mapenzi ya Mungu, lakini alijulikana na Mungu kuwa ni mtumishi wake hata kabla ya kuokoka.
Neema ya Mungu haiangalii matendo yawe mazuri au mabaya, Kama neema ingeangalia matendo hakuna mtu ambaye angeweza iona mbingu na kazi ya Yesu wa Nazareti kufa msalabani ingekuwa haina maana.

Kwa hiyo kama asilimia 0.1 ni nuru na zilizobaki asilimia 99.9 ni giza, Mungu anatusisitiza tuifikiria nuru tufanikiwe kuliko giza kubwa tulionalo mbele yetu la! Tusije ingia majaribuni na tukapotea kama shetani. Kupitia asilimia 0.1 ya nuru hiyo dunia itabadalishwa, kwa sababu kama Biblia inavyosema toka kitabu cha Mwanzo ya kwamba Dunia ilikuwa giza wala nuru haikuwepo lakini Mungu alifanyiza nuru kwa Neno ambayo kwa hiyo dunia yote ikawa na nuru ambapo giza lilitengwa nayo. Ndio maana Yesu wa Nazareti anasema masikini wataendelea kuwepo kutokana na kutokuwa fikra endelevu, na anasema amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu na kumfanya kinga yake, ni kwamba atakuwa mtumwa wa huyo na masikini milele. Fikra endelevu haina njia nyingine zaidi ya kumuangalia Yesu wa Nazareti kuwa ndiye alfa na omega, mwanzo na mwisho yaani tunapaswa kutazama mpaka tumuone Yesu wa Nazareti kuwa ni kila kitu katika maisha yetu ili ya kwamba hata tukitazama mwisho wa jambo na sio mwanzo wake tusihofu na katika ule ugumu wake, giza lake tumuone Yesu wa Nazareti akituvusha.
Jiamini mwenyewe katika Mungu utaibadili dunia unayoishi na itakumbukwa katika vizazi ya kwamba ulikuwepo, Jina la Yesu kristo wa Nazareti liinuliwe, Amina.




No comments:

Post a Comment