#VAA UHUSIKA WAKO

Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo mpendwa, hebu tafakari nami neno hili hakika litakuwa la baraka kwako pia.
"Kama ni wewe basi husika kikamilifu kuwa ni wewe". 
Kama vile waigizaji kwenye filamu bila kuuvaa uhusika maudhui ya filamu hayawi na mvuto wala kugusa maisha ya wengi. Kile kinachogusa maisha ya wengi ni kule kusimamia imani yako katika kitu fulani, hiyo ni nguvu halisi na mvuto ugusao wengine. Siku zote ufanyapo kitu kisichovuta ina maana wewe mwenyewe si mhusika, hujajidhihirisha kwa wazi kuwa ndiye wewe na kuwa unaamini unachokifanya, wasiwasi wako ni kutokukubalika kwako. Hakuna namna mtu mwema na sahihi katika matendo yake kutokukubalika, kwa maana kama vile walivyo wamkataao ndivyo walivyowamukubalio. Japo kunahitajika nguvu ya Mungu, ndio! kusimamia maono si tu kuyafuata ila ni pamoja na kujihusisha kwa ujasiri wote pasipo hofu wala mashaka kwamba unachokiamini ni ndiyo na hakika na ya kwamba uko tayari kukisimamia hata kama utabaki mwenyewe katika wote, hata kama mauti ikuwinde vipi huko tayari kughairi wala kurudi nyuma, wewe unakuwa unaenda mbele kwa mbele. Huko ndio kuuvaa uhusika!! Kwa maana umekata shauri na nia yako ni dhabiti kabisa kwamba uchekwe, udharauliwe ama utengwe kamwe hauteteleki, hapo katika kipimo hicho kwa mema yako utendayo utavuta waliowengi katika watesi na adui na wote waliokinyume nawe.
Katika tafiti zangu fupi nimegundua wale waliosimama katika maono yao sio waliogopa kuanguka hapana wala sio walio ghairi maisha bali ni wale waliovaa uhusika katika maono yao haijalishi ugumu wake na kusonga mbele bila kukataa tamaa wala kuonea mtu awayeyote haya wala aibu. Hao ndio washindi hata sasa!
Ndio maana hata Biblia takatifu inatusisitiza ya kwamba tuuvae uhusika katika lile kusudi la Mungu kwa maana huko ndiko kuletako mavuno mengi, na kuyatimiza mapenzi ya Mungu. Jiulize wewe ni nani? Na ni mapenzi ya Mungu ufanye nini? Kwa sababu kila mwanadamu kuna kusudi alilokusudiwa na Mungu kulitenda, Na ukishajua kusudi lako, Vaa uhusika na yatende mapenzi yake Mungu, acha kujihangaisha kutimiza tu mapenzi ya mwanadamu mwenzako asiye na hata uwezo wa kujiongezea pumzi ya uhai pindi ikatikapo. Ukisoma Wafilipi 2:5-11NASB biblia inasema vizuri ya kwamba; Have this attitude (mind) in yourselves which was also in Christ Jesus,  who, although He existed in the form of God, did not regard equality with God a thing to be grasped,  but emptied Himself, taking the form of a bond-servant, and being made in the likeness of men.  Being found in appearance as a man, He humbled Himself by becoming obedient to the point of death, even death on a cross.  For this reason also, God highly exalted Him, and bestowed on Him the name which is above every name,  so that at the name of Jesus EVERY KNEE WILL BOW, of those who are in heaven and on earth and under the earth, and that every tongue will confess that Jesus Christ is Lord, to the glory of God the Father.
#Muwe na nia ile ile kama aliyokuwanayo Kristo, unajuwa maana yake hapo, mtu mwenye attitude fulani ni ngumu kumubadilisha na siku zote husimamia anachokiamini haijalishi mazingira na ndio maana wengine humdhania labda ni kichaa, kwa maana saa nyingine huo msimamo humfanya aende kitofauti kabisa na mawazo na matendo ya wengine ili tu kutimiza kusudi ambalo dhamiri yake inamvuta kulitenda haijalisha gharama wala mitizamo ya wengine, kwamba watamuonaje, yeye hilo haliwazi wala kuliangalia.

Siku zote mpendwa simama imara katika nia yako kwa imani yako yote na nguvu zako zote na yale unayoyatizamia yatatimia na kufanikiwa sawa sawa na kujitoa kwako katika kuyadhihirisha hayo maono. Vaa uhusika wako ili uwe sumaku, beba mzigo wa maono yako, ule utungu wa mimba ya maono yako utakufanya uyatimize malengo na kusudi kwa wakati ulioamuriwa, barikiwa na Bwana wetu Yesu Kristo, amina.

No comments:

Post a Comment