Ishi ukimtazama Yesu wa Nazareti ina maana tumuishi Yeye, Biblia inasema katika Yohana 3:14-15 kama vile Musa alivyomuinua Nyoka wa shaba kule jangwani wanawaisraeli kwa kumutazama huyo nyoka wa shaba wakaponya na mauti ya sumu za wale nyoka waliowang’ata huko jangwani, Vivyo hivyo Mwana wa Adam (Yesu wa Nazareti) alikwishainuliwa juu na ya kwamba mwanadamu yeyote aliye na mwili amutazamaye huponya na shida, dhiki, laana, mauti na mateso yote yamukumbayo mwanadamu na kupata uzima wa milele. Kwa hiyo kama vile katika tenzi za rohoni namba 118; inavyosisitiza kuwa ni Ujumbe wa Bwana kwamba “tuishi tukimtazama yeye” yaani yeye kuwa mfano kwetu vile tupaswavyo kuishi ili tupate kuwa huru na salama kupitia yeye na ili kwamba tuishi maisha ya daima na hakika ya milele.
Kwa maana kama ilivyoandikwa katika Yohana 8:28-29; 10:30 Yesu wa Nazareti[Adam wa pili] katika wote walio na mwili yaani Wana wa Adam ndiye pekee aliye moja ya nafsi ya Mungu[nafsi ya pili] yuna Mungu na yu Mungu hakika na siku zote anatenda yaliyo mapenzi ya Mungu. Na pia yatupasa kumtazama Yesu wa Nazareti ili kumuishi Yeye hii yote ni kutokana na sababu zifuatazo na zinginezo;-
i) Ni yeye pekee aliyesema "mimi na Baba yangu wa mbinguni tu mmoja (Yohana 10:30), naam! yeye ndiye nafsi ya pili ya Mungu.
ii) Ni yeye pekee aliyesema "sitowaacha yatima nitarudi kwenu na kukaa nanyi" (Yohana 14:18), na ni kweli yuko nasi tumuaminio na kumtumaini.
iii) Ni yeye pekee aliyesema "nitakuwa nanyi milele mpaka ukamilisho wa dahari" (Mathayo 28:20), Ndiyo! Yesu kristo wa Nazareti yu Hai ndani yetu na yeye ni wa milele hakika.
iv) Ni yeye pekee aliyesema "nakwenda mbinguni kuwaandalia makao ya milele" (Yohana 14:1-4), tumaini lipo na ni kweli hakika ametuandalia makao ya milele (Ufunuo 21:1-5, 22:1-5)
v) Ni yeye pekee aliyesema"mimi nikienda kwa Baba Mungu mwenyezi nitatuma msaidizi ambaye ni Roho mtakatifu kwenu" (Yohana 14:26, Yohana 15:26, Yohana 16:7,13), Naam nakweli siku ya pentekoste msaidizi (Roho mtakatifu) alishuka kwetu (Matendo 2:1-4)
vi) Ni yeye pekee aliyekufa msalabani (Yohana 19:30,33) na kufufuka siku ya tatu (Mathayo 28:6) na kisha kupaa mbinguni kwa Mungu mwenyezi (Matendo 1:9-11)
vii) Ni yeye pekee alivyokuwa anapaa mbinguni (Marko 16:19, Luka 24:51) alisema kuwa "Mamlaka yote nimepewa mimi mbinguni na duniani" (Mathayo 28:18)
Hivyo imba tenzi ya rohoni (118) hapo chini yamkini leo ikiwa ndiyo siku yako ya kufahamu na kutambua moyoni mwako kwamba ni nini? Bwana Yesu wa Nazareti anamaanisha anavyosema “Ishi ukinitazama mimi”:

1.Ni ujumbe wa Bwana, Aleluya!
wa maisha ya daima,
Amenena mwenyewe, Aleluya!
Utaishi ukimtazama.
wa maisha ya daima,
Amenena mwenyewe, Aleluya!
Utaishi ukimtazama.
Tazama, ishi sasa!
Kumtazama Yesu,
Amenena mwenyewe, Aleluya!
Utaishi ukimtazama.
Kumtazama Yesu,
Amenena mwenyewe, Aleluya!
Utaishi ukimtazama.
2.Ni ujumbe wa wema, Aleluya!
Nawe shika, rafiki yangu!
Ni habari ya raha Aleluya!
Mwenye kuinena ni Mungu.
Nawe shika, rafiki yangu!
Ni habari ya raha Aleluya!
Mwenye kuinena ni Mungu.
3.Uzima wa daima,Aleluya !
Kwake Yesu utauona.
ukimtazama tu, Aleluya!
Wokovu u pweke kwa Bwana.
Kwake Yesu utauona.
ukimtazama tu, Aleluya!
Wokovu u pweke kwa Bwana.
No comments:
Post a Comment