Yeye aliye Nyota ya kung’aa ya asubuhi anasema kwa malaika ashindaye na kuyatunza matendo yake hata mwisho atampa mamlaka juu ya mataifa na nyota ya asubuhi.
Na kwa wana wa Mungu, anasema na wale walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga, na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele. Na nyota za asubuhi ziimbe kwa Bwana na wana wote wa Mungu wapige kelele kwa furaha na shangwe. Kumbuka ile nyota ya asubuhi, shetani ameanguka kutokana na kutenda dhambi kwa kukosa utii na unyenyekevu mbele za Mungu na kwa kile kiburi cha kutaka kujiinua na kujikweza juu kwa hiyo akaanguka mpaka chini kuzimu.
Kwa hiyo utunze ule wasifu wa Kristo ndani yako baada ya wokovu, kwa sababu ni wengi Bwana huwapa lakini ni wachache hutunza hivyo mtamani yeye zaidi kuliko vyote ili uwe na uweza wa kumiliki na kutawala, Kristo awe vyote kwako fanya mema kuwa mwema ili kuyashinda maovu yale mabaya na makwazo yote.
Furahi na kuwa na shangwe katika Bwana Yesu, aliye Shina na Mzao la Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi, nasema tena furahia katika Kristo, tumaini la utukufu; kwa kuwa tumaini ulilonalo katika Bwana ndiyo ahadi yake kwako.
Daima kuwa mshindi katika jina la Yesu kristo, Amina
Rejea katika Neno:
Luka 2:32; Mathayo 2:2; Ufunuo 22:16; Ufunuo 2:26-28; Danieli 12:3; Job 38:7; Ufunuo 1:20; Isaya 14:12.

No comments:
Post a Comment