Jinsi unavyopendeza uumbaji wake, tazama milima, madini, mabonde, chemi chemi, bahari, maiwa, mito, pepo, anga, mwanga wa jua, mwanga wa mwezi, mwanga wa nyota, uoto wa asili na mimea, wanyama, ndege na wanadamu; ni kweli inashangaza sana vile alivyoumba ndani ya siku 6 kwa Neno (Mwanzo 1). Lakini kwa Mungu vyote hivi inaonekana kama sio kitu yaani kwake sio kitu kikubwa sana, kwa sababu vitu alivyoviumba anaweza kuviharibu vyote kwa sekunde na kuumba tena vitu vipya. Sasa kwa nini wanadamu kutumia uwezo wote na kwa jasho kwa vitu vya kidunia tu? Na kwa nini sio kutazama tu na kuhangaikia vitu vya ufalme wa Mungu?. Muumbaji pekee ndio wa muhimu, lakini katika dunia hii hakuna cha muhimu isipokuwa Kristo, na ndio maana Mhubiri anasema vyote ni ubatili mtupu, Kwa maana kazi zetu zote na yote tuyatendayo ni ubatili mtupu na hayana maana sana kwa Mungu ni kama mzunguko wa nyuzi 360 umbao unazunguka na kuzunguka tena na tena au kwa mshale wa saa siku zote unazunguka kuanzia saa 1 hadi saa 12 na kurudia tena na tena. Hakuna hitimisho kwa kila kitu kitendekacho chini ya jua; kwani kila tuyatendayo twayatenda tena na tena pasipo kufikia pointi ambapo utasema sasa nimeridhika au inatosha; na ndio maana ni bora kuwa mtumwa wa Yesu kwani kwake kuna uzima wa milele kuliko kuwa mtumwa wa dunia. Dunia haiwezi kukutosheleza kitu zaidi zaidi kukubebesha mizigo mabegani kila iitwapo leo bila kupumzika, hivyo tamani zaidi vile vya milele kuliko vile vilivyo vya muda kidogo tu.
Huu nao ni mshangao! Dunia/ nchi hii ambayo kiukweli iliumbwa kwa siku chache sana zisizozidi 6 kwa Neno lake; Utakuta wanadamu wanachoka nayo kwa kutafuta vitu pasipo kuridhika na kwa jasho sana kwa miaka yote tangu kuzaliwa kwao hadi uzeeni huku wakihangaika kutaka kupata vile vilokwisha umbwa na Mungu tayari wasivipate kwa wakati na vile watakavyo kufanikisha mwishowe haviwaridhishi kwa kiwango wakitakacho au kwa kulinganisha wa nguvu walizotumia kuvipata (Mhubiri 6:2). Hivyo sasa ili mambo yawe mepesi sana katika kila kitu na tufanye uhusiano wa karibu sana na Mungu muumba wetu kupitia Kristo. Biblia yasema katika Ufunuo 20:11 kuwa kwa uwepo wake tu mbingu na nchi vitakimbia na wala visionekane tena mahali pake (Ufunuo 6:14 na pia 21:1). Hiyo tu inatuhakikishia kuwa vitu vya dunia si vya kudumu bali vya kiroho ni vya milele, kwa hivyo tamani sana vitu vya kiroho viwezavyo kudumu katika ulimwengu wa kiroho na wa kimwili pia, na ni Yeye pekee aliye mwanzo na mwisho ndiye awezaye kiukweli kukubadilisha kutoka mtu wa mwilini na kuwa wa kiroho; na Jina lake ni YESU. Kwa hiyo kubali kubadlishwa leo na kujiunganisha nae kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, Amina.