Isaya 58:1 Piga
kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao,
Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.
2 Walakini
wanitafuta kila siku; hupenda kujua njia zangu; kama vile taifa waliotenda
haki, wasioacha sheria ya Mungu wao, hutaka kwangu amri za haki; hufurahi
kumkaribia Mungu.
3 Husema,
Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini
huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na
kuwalemea wote watendao kazi kwenu.
4 Tazama,
ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu.
Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu.
5 Je!
Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha
nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu
chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana?
6 Je!
Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza
kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
7 Je!
Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje
nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu
mwenye damu moja nawe?
8 Ndipo
nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki
yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.
9 Ndipo
utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa
nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;
10 na
kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa;
ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.
11 Naye
Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na
kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama
chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
12 Na
watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi
vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye
kurejeza njia za kukalia.
Jua pia upendo wa kweli ni zao la upendo wa Mungu [ 1 Petro 4:8].
Hivyo kwa neema zake Mungu na akufunulia sasa siri ya saumu iliyo bora ukupayo faida katika jina la Yesu Kristo, Amina.
No comments:
Post a Comment