#KUWA MKWELI NA MUWAZI USAIDIKE

2 wafalme 6:1-7; 1 Kisha, wana wa manabii wakamwambia Elisha, Angalia basi, mahali tukaapo mbele yako ni padogo kwetu. 2Basi twende mpaka Yordani, twakuomba, tutwae huko kila mtu mti mmoja, ili tujifanyie huko mahali pa kukaa. Akajibu, Haya! Nendeni. 3Mmoja wao akasema, Uwe radhi, basi nakusihi, uende pamoja na watumishi wako. Akajibu, Nitakwenda. 4Basi, akaenda pamoja nao. Nao walipofika Yordani, wakakata miti. 5Lakini mmojawapo alipokuwa katika kukata boriti, chuma cha shoka kikaanguka majini; akalia, akasema, Ole wangu! Bwana wangu, kwani kiliazimwa kile. 6 Mtu wa Mungu akasema, Kilianguka wapi? Akamwonyesha mahali. Akakata kijiti, akakitupa pale pale, chuma kikaelea. 7Akasema, Kiokote, Basi akanyosha mkono, akakitwaa.

Sisi wanadamu hatuweki mambo yetu yote wazi na pengine kutomuuliza Mungu katika kila maamuzi tuyafanyao kama ni sahihi? Ndio! tunauhitaji wa vingi lakini kuna kanuni ya kuvipata. Fikiria hao wana wa manabii ktk 2 wafalme 6: 1-7; Unataka ufanye kitu kizuri sawa lakini huweki bayana kuwa utafanyaje kukipata?

Tumeona wengi wakinunua magari ya kifahari, wakijenga nyumba za kimataifa na kuishi maisha mazuri sana sana lakini mwisho wake kuwa mbaya kuliko ambavyo yupo yule maskini ambaye hakuwahi kuuonja utajiri. Huku kwa wengi wakisomeka ni utajiri wake! kumbe ni wa kuazima na ni mpaka vigezo vitimizwe ndipo uwe wake katika wakati fulani. Ndio! wazo lako ni zuri je’ umemshirikisha Mungu katika Maamuzi yako?, watu wanaweza kukusoma kama wewe utakavyo kusomeka kwa maana penye nia pana njia hivyo ni dhahiri kwamba waweza kung’ang’aniza usomeke vile unavyotaka hata kama si kweli. Saa nyingine mwanadamu hulazimisha asomeke kuwa anao utajiri hata kama ni wa mikopo, Ni mzuri au mrembo hata kama sio kwa sababu kuna namna nyingi za kujirembesha, n.k. Lakini kweli siku zote husimama kwa sababu ni Neno na ni Mungu. Weka mambo yako bayana na Mungu usijeaibika, kama mwana wa nabii sio mpaka upate tatizo ndio useme Kweli, inapaswa iwe kabla ya kupata tatizo. Kwa Mungu yote yanawezekana, sio mpaka mkopo wa benki ukushinde ndio useme Ukweli na kumtegemea Mungu kwamba vyote ulivyonavyo ni vya benki na wanataka kukunyang’anya au umeazima na imefika deadline ya kuvilipia au kuvirudisha. Ndio! huo mkopo umekuzalishia mali nyingi na umefanya mengi mema na mabaya pia lakini, cha kuazima hakisitiri makalio ipo siku utaaibika tu! Kumbuka mtegemea cha…… hufa masikini.

Lakini leo Yesu wa Nazareti anakata kijiti katika miti uliyokata kwa shoka ya kuazima iliyopotea ili kukurudishia hiyo shoka ukamwachia mwenye nayo na kukuzibia hiyo aibu, Upo tayari Mhusika! Chukua sehemu ya mali yako uliyoipata kwa mikopo na njia zingine zisizo halali mpe muhitaji haswaa iwe yatima, maskini, mjane, n.k,  Mungu ataipokea sadaka yako na maombi yako na katika hiyo, shoka uliyoazima itakurudia yaani atakutafutia namna ya kumaliza deni lako au mikopo yako pasipo kuaibika.Amini leo na tendea kazi neno hilo utashinda, kwani Mungu wetu ni wingi wa rehema.

No comments:

Post a Comment