Aliposema; “IMEKWISHA”, Ilikuwa ndio mwanzo wa kufunguka kwa
majaliwa yako katika maeneo yote ya maisha yako ili kupokea miliki zako zote zilizokuwa
zimeshikwa na mwizi shetani, sio tu afya wala utajiri pekee bali pamoja na vipawa vya
roho mtakatifu vilihuishwa saa na wakati ule na roho wa BWANA; ufahamu, hekima,
shauri, maarifa, uweza, hofu ya Mungu na kumcha Mungu.
Hii ina maanisha kwa uweza wa Roho mtakatifu tunavyo vyote
ni jukumu letu kuvifanya halisi kwetu katika ulimwengu wa mwili.
Ikumbuke siku zote ile siku ya wokovu wako alioufanya Yesu
Kristo ndani yako; na maanisha ile siku ya uhuru wako katika roho ili uwe huru
katika yeye milele.
Huyo ni Yesu Kristo wa Nazareti; Akateka mateka, akawapa
wanadamu vipawa.
Yesu ananipenda sana mimi; Nina hisia hiyo kwa nguvu sana
moyoni mwangu, Ooh! YESU.
Ni vipi kuhusu wewe?
Mwalike leo moyoni mwako; Yesu atakubadilisha kwa wema na
kuyabadilisha maisha yako hakika na kukupa umiliki wako wa awali ulioibiwa
kwako.
Yatafakari maandiko haya ktk Biblia Takatifu; Yohana
19:30, Zaburi 68:18, Efeso 4:8-11, Isaya 11:2-3, Wakorintho wa Kwanza 12:8-10,
Nahumu 2:9 na Waamuzi 5:12.
~Jina la Bwana wetu
Yesu Kristo wa Nazareti libarikiwe na kuinuliwa juu sana milele yote, Amina.
No comments:
Post a Comment