#MUNGU ATAKUTUMIA HATA PASIPO WEWE KUJUA, NI WAJIBU WETU KURUDISHA UTUKUFU KWA MUNGU ILI KUTUMIKA ZAIDI

Waamuzi 15: Kwa habari ya Samsoni.
8 Basi, akawashambulia vikali na kuwaua wengi. Kisha akaenda kuishi katika pango la mwamba wa Etamu. Samsoni awashinda Wafilisti, 9 Wafilisti wakaja, wakapiga kambi yao nchini Yuda na kuushambulia mji wa Lehi. 10Watu wa Yuda wakawauliza, “Kwa nini mmekuja kutushambulia?” Nao wakawajibu, “Tumekuja ili tumfunge Samsoni na kumtendea kama alivyotutendea.” 11 Basi, watu 3,000 wa Yuda wakamwendea Samsoni pangoni mwa mwamba wa Etamu wakamwambia, “Je, hujui kwamba Wafilisti wanatawala juu yetu? Tazama basi, mkosi uliotutendea!” Samsoni akawajibu, “Kama walivyonitendea ndivyo nilivyowatendea.” 12 Wakamwambia, “Tumekuja kukufunga ili tukutie mikononi mwao.” Samsoni akawaambia, “Niapieni kwamba nyinyi wenyewe hamtaniua.” 13Nao wakamwambia, “Sisi hatutakuua ila tutakufunga tu na kukutia mikononi mwao.” Basi, wakamfunga kwa kamba mbili mpya na kumtoa humo pangoni. 14 Alipofika Lehi, Wafilisti walimwendea mbio huku wakipiga kelele. Ghafla roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Samsoni kwa nguvu na zile kamba walizomfunga mikononi mwake zikakatika kama kitani kilichoshika moto, navyo vifungo vikaanguka chini. 15Samsoni akapata utaya mbichi wa punda, akautumia kuwaua watu 1,000. 16Kisha Samsoni akasema, “Kwa utaya wa punda,nimeua watu elfu moja. Kwa utaya wa punda,nimekusanya marundo ya maiti.” 17 Alipomaliza kusema, akatupa utaya huo. Mahali hapo pakaitwa Ramath-lehi, yaani mlima wa utaya. 18 Kisha Samsoni akashikwa na kiu sana. Basi, akamwomba Mwenyezi-Mungu, akisema, “Ee Mungu, wewe ndiwe uliyeleta ukombozi huu, kwa kunitumia mimi mtumishi wako. Je, sasa utaniacha nife kwa kiu na kutekwa na Wafilisti hawa wasiotahiriwa?” 19Mungu akafungua mahali palipokuwa na shimo huko Leki, akatiririsha maji. Samsoni akanywa maji hayo na nguvu zikamrudia. Chemchemi hiyo ikaitwa En-hakore; nayo iko huko Lehi mpaka leo. 20 Samsoni alikuwa mwamuzi wa Waisraeli kwa miaka ishirini, nyakati za Wafilisti.
Kauli ya Samsoni ya ushindi haikumtukuza Mungu, aliutukuza ule utaya wa punda kwamba kwa huo amewaua wafilisti (maadui) 1,000. Mungu anataka tumtukuze ili sifa zake zivume kutoka kizazi mpaka kizazi ilimchukuwa Samsoni kushikwa na kiu kali mpaka alipomtambua Mungu kuwa ndio ulikuwa uzima wake ndio wokovu wake, na huwezi jua waweza ona ule utaya wa punda machoni kwa samsoni ulikuwa utaya kumbe katika macho ya rohoni ni upanga wa malaika kwani je’ unaweza wewe kutumia utaya wa punda kama silaha ya kivita kama usipokuwa upanga au silaha ya vita ya kiroho kushinda vita, la hasha haiwezekani. Ona Samsoni kwenye shida yake ya kiu mpaka aliposema; “Ee Mungu, wewe ndiwe uliyeleta ukombozi huu, kwa kunitumia mimi mtumishi wako’’.---ndipo Mungu akafungua maji katika shimo akanywa maji hayo na nguvu zikamrudia. Na chemchemi hiyo ikaitwa En-hakore maana yake ni Kijito cha mwombaji na kimeitwa hivyo tujue katika kumtegemea na kumuomba Mungu kuna uzima na ukombozi. Na Neno linamalizia kwa kusema baada ya hayo Mungu akamfanya Samsoni kuwa Mwamuzi wa Waisraeli kwa miaka 20 nyakati za wafilisti kwa maana yeye pekee alionekana kuwa na Imani na kwamba alimtambua Mungu asiyeshindwa na ndiyo maana hata wana waisraeli zaidi ya 3,000 walipomfuata kwa hofu kwamba msimamo wake, ujasiri wake ulikuwa unawaharibia kwani wao walikiri kuwa watumwa na watawaliwa wa wafilisti lakini si kwa Samsoni mnadhiri wa Mungu.

Uweza wako ni mkuu, Roho wa Mungu akiwa ndani yako Mungu lazima apewe utukufu kwa yote anayofanya ndani yako kwa Roho wake na utapewa hatua mpya siku hadi siku na utapandishwa na Mungu kutoka utukufu mpaka utukufu. Amina.

No comments:

Post a Comment