Biblia inasema katika
Mathayo 19:11-12; Yesu akawaambia “si watu wote wanaoweza kupokea neno hili,
isipokuwa wale tu waliojaliwa na Mungu. Kwa maana wengine ni matowashi kwa
sababu wamezaliwa hivyo, wengine wamefanywa matowashi na wanadamu na wengine
wamejifanya matowashi kwa ajili ya Ufalme wa Mbinguni. Yeye awezaye kulipokea
neno hili na alipokee.”
Muundo wa Kitowashi;
Nabii wa Zimbabwe kwenye mahubiri yake haya alisema kanisani kwake kulikuwa na
dada mmoja ambaye alifunga na kusali kwa siku 29 mlimani, ambapo kanisa
limekuwa likiutumia huo mlima kwa kufunga na sala. Sasa huyo dada baada ya siku
29 za mfungo ambao ulimuweka katika hali ya kufa kabisa, yeye alikiri kuwa
alifanya hivyo kwa ajili tu ya Nabii wake awe salama pamoja na yeye kujua jambo
lolote ambalo lingeweza kumtokea baba yake wa kiroho (Nabii).
Kuna towashi katika
neno la Mungu; towashi ni yule mtu aliyehasiwa ambapo hawezi tena kujizalisha
yeye mwenyewe, hawezi kuwa na watoto yaani hakina kizazi kitakacho fuata baada
yako. Yesu alisema kuhusu aina ya matowashi; kwamba wapo waliozaliwa matowashi
toka tumboni wa mama zao, pili wapo waliofanywa matowashi na wandamu wenzao na
pengine kwa kulazimishwa na aina ya tatu ni ile ambayo nataka kuiongelea
haswa ambayo Yesu alisema wapo waliojifanya wenyewe matowashi kwa ajili tu ya
ufalme wa Mbinguni, na Yesu mwishoni akasema yeye atakaye kupokea na apokee,
kumbuka pia maneno ya Yesu mwanzo alisema lile nalokwenda kusema yaani kuhusu
matowashi ni wachache tu watalielewa.
Sasa ukiangalia namna
vile hapo kale na taratibu zao zilivyokuwa, utagundua na kuanza kuelewa ya
kwamba matowashi walikuwa ni watu wa kuaminika sana kwa wafalme. Kila mfalme
alihakikisha ana towashi katika makazi yake ya kifalme na ni matowashi tu
waliokuwa wanaaminika na ukiwauliza wafalme kwa nini walipenda kuwa na towashi
kuliko hata walinzi au mwanadamu yeyote, atakwambia nina mabinti kwenye ufalme
wangu, vijana, wake ambapo hakuna mkorofi yeyote atakayetakiwa kuwaharibu mbele
yangu ni towashi pekee anafaa nafasi hiyo. Hii ndiyo sababu pekee iliyofanya
matowashi waaminike sana, walikuwa wanajaribu hata mvinyo wa mfalme kabla
hajanywa ili kama kuna kitu kibaya kiwapate wao, matowashi hawakuogopa kufa kwa
sababu hawakuwa na chakuishi hapa duniani isipokuwa kuwatumikia mabwana zao,
wafalme. Na hii ndio sababu pekee ya matowashi kuaminika zaidi ya wale watu ambao
walikuwa tayari kuzaa na kujizalisha wenyewe.
Siku hizi utaona mtu wa
Mungu analia sio kwa sababu anakosa washirika wa karibu wa maono yake sio! kwani
kuna watu wengi wanamzunguka karibu naye, lakini tatizo ni kwamba wakati mtu wa
Mungu anataka kujizalisha na wao wanajizalisha kisiri na hiyo inaleta mvurugano
baina yao kwani maono yanakinzana na kufitiniana. Katika biblia Mwanzo 14:14
inasema Ibrahimu alikuwa na wajakazi 318; waliofunza vyema kwa vita, jeshi
ambalo lilikuwa lake mwenyewe la nyumbani kwake, lakini katika Sura ya 15 Ibrahimu
anamlilia Mungu ya kwamba amemuacha na ya kuwa kwanini yeye hana mtoto, kwa
hivyo unaweza kuwa na watu wengi
wanakufuata na huna mtoto hapo, kwa kuwa tu wafuasi wako wako kama
watumwa na watumishi kwa hiyo kilio cha mtu wa Mungu kwa Mungu hakitaisha
kitaendelea milele mpaka tu watu wa Mungu watakavyoweza kuzalisha watoto wakike kwa wakiume makanisani, kwa sababu tu watumwa au watumishi sio wana (kwani
hawawezi kutunza maono yale yaliyo moyoni mwa mtu wa Mungu).
Sipaswi kujizalisha kwa
namna yangu, lakini baba wa kiroho anapaswa kuweka mbegu katika mfumo wangu wa
uzalishaji na mimi kuzalisha mbegu ya baba yangu wa kiroho, kwa hiyo kuna hatua
ambayo ninapaswa kuwa kama towashi wa kiroho kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Kama
tu Baba wa kiroho ataniamini ninapaswa kila siku kuangalia mfumo wangu wa
uzalishaji. Ngoja nielezee vitu vichache kwa kina hapa; Wakati Mungu amemwita
Musa, alikuwa na ufahamu kuhusu suala la wana Israeli huko Misri na usisahau kuwa
kwa Israeli kutoka Misri alitakiwa nabii, lakini Israeli walikuwa wakiomboleza
katika kazi za kitumwa huko Misri. Na ujue ni rahisi sana kuwa maskini lakini
inakuhitaji uwe na nabii kutoka katika hali hiyo, kuna vitu ambavyo unaweza
kufanya wewe mwenyewe lakini unamuhitaji nabii sahihi, mtu wa Mungu mwenye
mafunuo ya roho mtakatifu kutoka katika mambo mengine yaliyo magumu ambayo hata
pesa haiwezi kukusaidia. Kama mtu akisema kwa mtu wa Mungu, “sijui kwa nini nateseka katika maisha haya”;
pale tu utakavyosema sijui kwa nini nateseka, inamaanisha unateseka kwa sababu hajui kwa nini, na hiyo ni sababu namba moja kwa
nini unateseka. Kwa hiyo kama
unataka kutoka katika maisha yasiyofaa ya taabu, unatakiwa uanze kujua kwanza
kwa nini unateseka. Unatakiwa uanze
kutafuta namna ya kutoka; na maana ufikiriye ni namna gani nitatoka katika hayo
mateso? Kutoka katika hali mbaya,
unatakiwa ujue ni kwa namna gani! Biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa
kukosa maarifa ya Mungu, kwa hivyo ni kwa kukosa maarifa ndiko kukufanyavyo
uteseke.
Sababu ya pili; unateseka kwa sababu tu ya vile
unavyojichukulia, inashangaza sana jinsi wale wapelelezi walivyoingia nchi
ya ahadi na kupeleleza nchi na kisha walivyorudi walimtaarifu Musa ya kuwa kule
tulikuwa kama panzi mbele ya macho ya wakaaji wa huko, na hali ni Mungu ndiye
aliyewaficha kwa siri, walifichwa hakuna hata mmoja aliyeweza kuwaona,
waliingia kwa siri na kutoka kwa siri bila kuonekana na mtu, na bado walipotoka
nje eti wakasema mwachoni mwetu wenyewe tulijiona kama panzi kwao na wachoni
mwao pia walituona sisi kama panzi, kwenye macho ya nani?, Hali Mungu alikuwa
pamoja nao. Unajua saa nyingine u maskini, kwa sababu ya vile unavyojichukulia
wewe mwenyewe, hao walikuwa wapelelezi waliofuzu kabisa kwa kazi hiyo, watu
ambao walikuwa wanaweza kuingia sehemu na kutoka bila kuonekana na yeyote, na
bado eti wakasema tulikuwa kama panzi mwachoni mwao, je ni nani aliwaona?, Usipende
kujichukulia mwenyewe vibaya.
Sasa biblia
inasema kwa nabii, wana Israeli
walikombolewa utumwani na kwa nabii, taifa la Israeli lilihifadhiwa jangwaani,
kwa hiyo yote yalikuwa kwa sababu ya uwepo wa nabii na lile wingu lilikuwepo
kumlinda nabii na watu wote waliokuwa naye walinufaika na wingu hilo kwa uwepo
wake nabii kwao. Na kama ukisoma biblia kwa uangalifu utaona hata Gehazi
alipotoka nje na kuona ukubwa wa jeshi la maadui limewazunguka alirudi na
kumwambia nabii Elisha kuwa hata tumekwisha, lakini cha kushangaza nabii Elisha
akamwambia’ “walio pamoja nasi ni wengi kuliko wao” na akasali ili Mungu
amufungue na macho ya mfanyakazi wake yakafunguliwa naye akaona jeshi kutoka
mbinguni likiwa limemzunguka nabii na ndipo mfanyakazi Gehazi naye
akajiunganisha na ulinzi huo uliokuwa kwa nabii akahifadhiwa. Kwa hiyo Israeli
kama taifa lilikombolewa kutoka Misri na kuhifadhiwa jangwani kwa sababu
lilikuwa ni kusanyiko la kinabii chini ya Musa, nabii.
Wakati Musa alivyopewa
jukumu na Mungu la kuhakikisha anakwenda na kuongea Farao juu ya wana wa
Israeli, Musa akatoa sababu kwa Mungu ya kuwa ana kigugumizi hivyo hawezi
kuongea vizuri, pamoja na kuwa Mungu alimshawishi na miujiza mingi kule mlimani Sinai, hivyo
Mungu kwa hasira yale maono makubwa yaliyompasa Musa pekee, Mungu akaamua
kumuunganisha Haruni kaka yake Musa kwenye hayo maono ambaye kwa wakati huo
alikuwa anakuja kumtafuta huko hali yuna furaha alipomuona, japokuwa ni Musa
ndiye aliyekuwa kuribu na Mungu na sio Haruni na Musa alifanyika na Mungu kuwa
mungu kwa Farao na kwa Haruni, hali Haruni akawa nabii wa Musa kwa Farao. Hii ilifanyika hivi kwa namna ambayo wakati
Musa alipokuwa anagugumia kuongea Haruni aweze kupakamilisha. Kwa hiyo Musa
aliporudi Misri, Farao alitakiwa hata ingebidi kubadilisha dini yake kwa sababu
mungu Musa alikuwa kwake sio tu kuwa kwake alikuwa akiongea na yeye Farao. Sasa
ona Musa alikuwa kwanza nabii wa Mungu halafu akafanyizwa na Mwenyezi Mungu
kuwa mungu kwa Farao pale tu alipokutana na Mwenyezi Mungu mlimani Sinai. Na
ukumbuke pale Ibrahimu na yule Lazaro maskini kifuani mwake (Luka 16:29),
Ibrahim akamwambia yule tajiri aliyekufa, ndugu zako wanaye Musa na manabii;
wawasikilize hao. Kwa hiyo akina nani hao Musa na manabii, inachanganya hapo!
Mungu alimfanya Musa mungu kwa Farao na kwa Haruni na Haruni kaka yake, nabii
wake Musa kwa Farao (Kutoka 7:1). Hii inanihakikishia kuwa kama Musa
asingejiona mwenyewe kuwa ana kigugumizi mbele ya uso wa Mungu, inamaanisha
Haruni asingepaswa kuwa sehemu ya maono yale makubwa. Hata hivyo mwanzo Haruni
hakuwa sehemu ya maono hayo makubwa mpaka pale Musa alipokiri ule udhaifu.
Katika maisha haya,
kama Mungu ni kila kitu kwako usijichukulie kama vile huwezi jambo lolote,
usipende kukiri udhaifu mbele ya uso wa Mungu ambaye ni nguvu zako (Yehova
Tsori), na pia usijichukulie mwenyewe ya kuwa huwezi kufanya yaliyo mapenzi ya
Mungu na kutekeleza kusudi lake kwako.
Wakati Mungu
alipomfanya Musa mungu kwa Farao na kwa Haruni kaka yake na Haruni kuwa nabii
wake Musa kwa Farao; Haruni alijua yakuwa alipaswa kutabiri kwa Farao na wana
wa Israeli pale tu na yale tu ambayo Musa alikusudia kuyasema, kama vile neno
kutoka kwa mwenyezi Mungu lilivyomjia Musa na wala sio kumjia Haruni kwa sababu
katika kipindi chote hicho cha maono hayo Musa alibakia kuwa mungu kwa kaka
yake Haruni (Kutoka 4:16).
Tukirejea kwa habari ya
mfumo wa kitowashi; kama unataka kibali ndani ya jumba la mfalme usiharibu wala
kuchakachua mbegu ya mfalme, Ukiunganishwa kwenye maono ya mtu wa Mungu
unatakiwa siku zote uelewe ni mbegu ya mtu wa Mungu tu (yaani yale maono yake
kama alivyopewa na Mungu) inayopaswa kujizalisha. Ni mtu wa Mungu pekee
anayezalisha na sio wengine kwa niaba yake, kwa sababu maono yanayodumu milele
ni yale yasiyojifitinisha yenyewe, na wala hakuna maono mengine ya tofauti
katika maono yale yale yaliyo halisi aliyopokea mwanzo. Kumbuka katika huduma
za kikristo; kuna walioletwa kwenye maono ya watu wa Mungu ili kusaidia katika
kuyathibitisha lisianguke hata moja na kuyaendeleza, haijalishi hata kama
wasaidizi hao watakuwa wanauwezo wa kuhubiri vizuri kuliko mbeba maono.
Kumbuka tena Yesu anasema kuna wengine waliojifanya matowashi kwa ajili tu ya
ufalme wa Mbinguni, kwa hivyo inakupasa ujitoe sadaka wewe mwenyewe na kujihasi
kiroho dhidi ya mvuto wa dunia ili uwe tayari kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
Hebu tafakari hili; mtu
wa Mungu E. Makndiwa alisema baada ya kuwajulishwa waumini wake kuhusu maono ya
ujenzi wa kanisa kubwa na kuwaonesha michoro kwa sinema, ndipo akamjulisha na
Baba yake wa kiroho lakini baba yake huyo alivyoona akamwambia mwanangu huu ni
upuuzi mtupu na kumshauri impasavyo kufanya, kwa hivyo baada ya ushauri huo wa
kiroho kutoka kwa baba yake wa kiroho ikambidi kurudi tena kwa waumini walewale
aliowajulisha mwanzo maono yake na kusema michoro ya ujenzi wa kanisa
imebadilika kwa sababu tu kuna mtu wa Mungu
(baba yake wa kiroho) anayeona vyema zaidi yangu, mfumo wa kitowashi.
Tafakari hili tena;
Mungu, japokuwa yeye ni Mungu lakini alikuja chini na kuacha vyote mbinguni na
akazaliwa na mwanadamu na akanyonya maziwa ya mwandamu ili akue sio tu
kunyonya, akahudhuria huduma za wanadamu, sio tu kuhudhuria huduma,
alijinyenyekeza chini ya mwanadamu na kumbe yeye ni Mungu, na sio tu
kujinyenyekeza, alimuruhusu mwanadamu amubatize, na hapo ndipo biblia inasema
mbingu zikafunguka kwa ajili yake, nakuambia, utateseka milele kama hutajifunza
kunyenyekea na kama hutatafuta mwanadamu ambaye utakwenda kwake na kujishusha chini yake na kunyenyekea, mtu
ambaye atakushika mkono na kabla hajakuinua juu atakukandamiza chini, na watu
wengi wanasali na kutenda kazi chini ya mbingu zilizofungwa, mambo yao ni shida
na magumu, wanasumbuliwa na pepo nyingi ziwapingazo kwa sababu tu hawako chini
ya mamlaka wala hawajajinyenyekeza chini ya mtu wa Mungu, kama vile Yesu
anavyomuelezea mtu mwenye imani kuu katika biblia, yule mtu aliyesema “hata mimi ni mtu chini ya mamlaka…….”.
Je’ umeshawahi kuwaza
kwa kina ni nini kinatokea unapotoa fungu la kumi kwa mtu wa Mungu au kanisa
ambalo halitoi fungu la kumi kwa kanisa lolote au mtu wa Mungu yeyote yule, au
unajinyenyekeza kwa mtu wa Mungu ambaye hanyenyekei kwa mtu wa Mungu yeyote
yaani asiye na baba wa kiroho, yeye ndio mkubwa hakuna mkubwa juu yake (baba wa
kiroho) yaani ni Yesu tu au kwa yule
asiyejua chochote kuhusu kuwa chini ya mwavuli wa baba wa kiroho, kweli hapo
wewe na kanisa kunakuwa na ugumu katika kuyatenda mapenzi ya Mungu na pengine
kuwa chini ya mbingu zilizofungwa na hali unaweza kuwa umejitoa kabisa kwa
Yesu, kumbuka watoto wa Skeva watoto wa kuhani katika biblia hawakuwa chini ya
mwavuli wa kiroho wa Paulo bali chini ya mwavuli wa kiroho wa baba yao,
wakataka mamlaka ndani ya Paulo imefanye kazi kwao wakati wakifanya huduma ya
ukombozi, hata kama ukitaka kutumia mwavuli wa kiroho wa mtu tofauti ndani ya
huduma ya baba yako jua kuwa kuna gharama ya kulipia, kwa hivyo inaaibisha sana
ukiwa na baba wa kiroho ambaye hawezi kuwakomboa watu. Saa nyingine haufanikiwi
kwa sababu tu hautaki kuchukua na kuifikisha mbali zaidi mbegu ya baba yake (yale
maono ndani yake).
Kuna matowashi katika
falme za wanadamu, unaona raisi ana mlinzi ambaye yuko tayari kufa kwa ajili
yake, yuko tayari kupokea risasi zote zilizokusudiwa kumpata raisi asiye hata
na roho mtakatifu, na wala si mtakatifu lakini kwa sababu tu ana mamlaka. Je si
zaidi sana ilivyotakiwa kuwa kwa watu wa Mungu walio na roho mtakatifu wa Mungu?
Mfumo wa kitowashi ni mzuri hata Ufalme wa Mungu unatambua hilo, na ndio maana
hata Filipo alitakiwa asimamishe kusanyiko lililokuwapo kwa ajili ya uamusho wa
roho mtakatifu ili tu kumfuata towashi; ambaye alikuwa na mamlaka chini ya
Kentuki malkia wa Ethiopia aliaminiwa juu ya mali na utajiri wake wote (Matendo
8:38-39). Tafakari uzuri wa muundo huo
katika kitabu cha Esta ; wakati Mfalme alivyotaka kuoa wanamke mwingine,
walikusanya mabikira wote katika nchi na kuwaacha chini ya usimamizi wa towashi
haggi kwa miezi kumi na mbili kabla ya kukutana na Mfalme, wakatunzwa naye na
kuwa wazuri zaidi bila kuchakachuliwa. Kanisa la leo linahitaji matowashi wa
kiroho ambao watakuwa tayari kutunza maono ya watu wa Mungu bila kuyaharibu au
kuyapotosha, bila kuzalisha aina nyingine ya maono lakini kuyatunza na
kuhakikisha yanadumu milele.
Kwa hiyo vitu vikiwa
haviendi sawa unatakiwa ucheki ule muungano wako na mtu wa Mungu; je' ni kweli
unaheshimu na kuitambua mamlaka? Kwa sababu kuna kitu katika maisha ambacho
hata pesa haiwezi kukufanyia, unahitaji upako wa Mungu ulio ndani ya baba yako
wa kiroho ili kuweka mambo sawa kwa ajili yako. Biblia inasema wapo
waliojifanya wenyewe matowashi kwa ajili ya ufalme wa Mungu; je uko tayari
kuacha kila kitu katika maisha yako pamoja na mke, watoto, ndugu, hata kuikataa
mbegu yako kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Mephibosheth (mwana wa Jonathan)
alidanganywa na mtumishi wa mfalme Daudi, wakati mfalme alipokuwa mafichoni
baada ya mwanae kukaa sehemu ya kiti chake cha ufalme, na hapo Mfalme Daudi
aliporudi na kumwona Mephiboshesh ya kuwa alibaki katika jumba la mfalme wala
hakuambatana nae, Mfalme akamuuliza kwa nini hukuenda pamoja nami naye akasema
alidanganywa na akaongeza kuwa kwa yeye Mephibosheth
yakuwa alishakufa miaka mingi iliyopita na hata hivyo akamwambia mfalme kwa
nini kunitunza mpaka sasa, unaweza kuutoa uhai hata sasa kama itakufanya wewe
ufurahi, wakati akiongea hayo alikuwa wakushangaza mbele ya mfalme kwa kuwa
alikuwa mchafu, ananuka, nywele zimevurugika, na kama ukimuuliza kwanini alikuwa
vile atakwambia kuwa aliona hakuna haja ya kuwa na raha nyumbani kwa mfalme
hali mwenye jumba yuko msituni hivyo hakuwa na amani ya kula, kunywa, kuoga wala
kuvaa (2 Samweli 19:24-28), Vipi kuhusu wewe?
Kwa hivyo kuwa towashi
wa kiroho kwa ajili ya Ufalme wa Mbinguni. Wana wa Mungu ishi maono ya Kristo
Yesu ndani yenu na heshimu watu wa Mungu (watumishi wake waaminifu) na pia
utunze maono ambaye Mungu ameweka ndani yao, utahifadhiwa na kufanikiwa hakika
katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti, Ameni.
Asante mtumishi wa Mungu, ufafanuzi wako umenifungua ufahamu zaidi na nimepokea. MUNGU akubariki
ReplyDelete