# USISUMBUKIE MAISHA YESU WA NAZARETI YUPO KWA AJILI YAKO

   Katika Luka 12:22-34; Yesu kristo akawaambia wanafunzi wake, kwa sababu hiyo nawaambia, MSISUMBKIE MAISHA yenu,Mtakula nini; wala miili yenu, mtavaa nini. Kwa kuwa Maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi. Watafakiri kunguru ya kwamba hawapandi wala hawavuni hawana ghala wala uchaga na Mungu huwalisha, bora ninyi mara nyingi kuliko ndege! 29…………msifanye wasiwasi, 30 kwa maana hayo yote ndiyo watafutayo mataifa ya duniani, lakini Baba yenu anajua mna haja na hayo.31 Bali utafuteni ufalme wa Mungu na hayo mtaongezewa. 32 Msiogope enyi kundi dogo kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme 34, kwa kuwa hazina yenu ilipo ndipo itakapokuwapo na mioyo yenu. Soma pia mathayo 6:25-34 na Yakobo 4:13-15.

Mhubiri anasema ni ubatili mtupu yaliyopo na yatendekayo duniani; 
Fikiria hivi rangi ya ukweli ya dunia hii kama sayari ni Nyeusi kutoka mwanzo 1:3 dunia ilikuwa ni giza mpaka NENO alipofanya Nuru. Dunia bila nuru ni giza iwe usiku au mchana; dark is equal to blackish colour hence black real in colour.

Rangi zote zinazoonekana ni kwa sababu ya uaksi wa mwanga, pasipo mwanga ni nyeusi tu. Kwa hiyo rangi zote ni feki coz zinategemea mwanga. Rangi halisi ni zile ambazo hata gizani zinaonekana kwa rangi zake zenyewe iwe njano, nyekundu, bluu, kijani, n.k pasipo kutegemea mwanga wowote iwe wa jua, mwezi au taa au umeme ambazo hizi hazipo duniani ila mbinguni kwenye origional ya vyote hata wanavyotengeneza nakudai ni original hapa duniani bado ni feki tu. 

Siku moja nilikuwa nimewahi katika ukumbi na kushuhudia jinsi walivyokuwa wakipamba ukumbi mmoja kwa ajili ya harusi kweli mapambo yalikuwa yanang’aa rangi nzuri sana zinazovutia vitambaa vya mng’ao wa rangi tofauti tofauti na mapambo mengine ya kumetameta wakiwa katika harakati za kumalizia tayari kwa sherehe, Ghafla mwanga uletwao na umeme ukakatika nilitafakari mengi sana siku ile na bado mpaka leo natafakari tu.

Hebu fikiria masaa 12 wapambaji walikuwa wanapamba kwa masumbufu mengi hali kitu wafanyacho sio real in itself still depend on something else to shine. Ukumbi mzima ukawa giza yaani kweusi tii kiasi kwamba hata wapambaji wenyewe wakawa hawaonani na wengine kuanza kutumia mianga ya simu ambayo haikuweza kusaidia kurudisha ule mtizamo wa kupendeza, kazi yao yote ghafla ikawa meaningless haina maana kabisa kujichosha kwao kwote kukawa hakuna cha kujivunia. 

Nikajifunza kuwa haina maana mtu kusumbukia vitu visivyo na uhalisia kivyenyewe vyenyewe hali pia vikiwa ni vya muda tu, fikiria mtu kuanda mazingira ya event ya masaa kwa mabilioni ya pesa kisa tu kuweka historia. Nasema vyovyote ufanyavyo historia ambayo ni ukweli mtupu ni BIBLIA na habari ya Yesu Kristo ndiyo inayodumu yaani NENO linadumu na matukufu yake yote tangu awali generation come generation go na siku zanavyozidi kukaribia mwisho Utukufu wake wa NENO lilelile unazidi kuwa mkuu zaidi. Kwa maana walikuwapo watu maarufu matajiri wenye sifa wakapita na historia zao zimebaki pasipo matukufu yoyote na zingine hata hazijulikani wala uzao wao hautambulikani, alikuwapo Firauni zaidi ya miaka elfu mbili mwili wake ulihifadhiwa kutokana na umaarufu wake lakini hakuna cha thamani ndani yako hata ukiuona sasa, hali nafsi yake ipo katika mateso ya kuzimu. Hata hivyo Biblia inasema itakusaidia nini kama ukiupata ulimwengu wote na kupoteza nafsi yako.

Na ndio maana kama sio Mungu, uzuri wa vyote vifanywavyo na binadamu ni ubatili mtupu, ni feki, watu huunda meno bandia, bikira bandia, makalio bandia, rangi ya mwili, namna ya kuongea, kutazama na kutembea, pia watu huunda lifestyles, miziki ya kidunia, na anasa zingine za dunia. Kwa kufuata hayo tunajichelewesha kufikia tuliyoandikiwa na kuandaliwa na Mungu, Biblia inasisitiza TUSISUMBUKIE MAISHA, inazungumzia tusifuate kila kitu kitaabishacho mioyo yetu na hali utukufu wa Mungu haupatikani kwa hayo. Na ya kwamba tusienende kwa namna ya mataifa yaendavyo bali kwa kila jambo kumfuata maelekezo ya Roho wa Mungu atokaye Juu mbinguni.

-Mungu anajuwa tunahaja na utajiri na mali; anatupa ila siyo kwa namna ya dunia hii, Tafuta ufalme wa Mungu kwanza!.
-Mungu anajua tunahaja na kuwa na muonekano wa kuvutia; anatupa ila siyo kwa namna ya dunia hii, Tafuta ufalme wa Mungu kwanza!.
-Sio kwamba hautajifungua mtoto la hasha! unajifungua kwa namna kama ya waisraeli walivyofanya misri na sio kwa namna ya wamisri ilivyokuwa desturi yao, Tafuta ufalme wa Mungu kwanza!.

Ufalme wa Mungu ni katika YESU KRISTO aliye lango la mbinguni, Mhitaji leo utakuwa salama na mengine yote utajazwa ya milele kama yeye alivyo wa milele na wala si ya muda mfupi, 

Let Him controls you and not the Kingdoms of this world. Amen!!...................Glory to God.