Saturday, July 25, 2020

#IMANI NI KUSIKIA NENO LA MUNGU; KUMSIKIA KRISTO ALIYE HAI

Warumi 10:17 katika Biblia yasema; ‘Imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa Neno la Mungu (Yesu Kristo)’.  

Hivyo imani ni zao la kusikia si kuona japo kushuhudia kwa macho kunaunga juhudi kwa sehemu za kuihuisha imani iliyozalishwa na kusikia, na kusikia kwa Neno la Mungu (Yesu Kristo).

Imani huhitaji masikio zaidi kuliko macho sababu kuona kwa macho hakuimarishi imani. Awapo Kipofu asikiaye na kiziwi aonaye, imani kwa kipofu asikiaye itajengeka mara na kuimarika zaidi kuliko kiziwi, kwa maana kuona kwa macho hakufikiri bali kusikia huambatana na fikra.

Pia biblia inasema ‘Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana’ (Ebrania 11:1). 

Imani si kwa kuoneshwa bali kwa kulisikia Neno la Mungu, unaamini sio kwa sababu umeona bali umesikia, waweza ona, ukiona utakuwa umeona iliyokawaida ya macho ila usikiapo tu imani huzaliwa.

Mtu huwa na matarajio juu ya kitu ama jambo sababu ya Neno la Mungu alilolisikia na wala sio muujiza aliouona. Muujiza hautakuletea wokovu ila Neno la Mungu (Mathayo 11: 20-24).


Kwa hivyo, kule kusubiri mpaka kuona ishara na miujiza ndipo umuamini Kristo kumewapoteza wengi na kuwaponza hata watumishi wa Mungu makini kabisa, yeah! ndio, kulekutamani kuona na kuonesha hata visivyoagizo la Mungu. 

Yatosha kulisikia na kulipapasa Neno la Mungu (1 Yohana 1:1). 

Kua imani, kwa nguvu ya kusikia (masikio) maana ile mbegu iliyo Neno la Mungu ni msingi wa yote maishani, japo dunia yajali zaidi vya kuona na macho hayatosheki (Mithali 27:20) na madanganyo yake hayajengi kamwe imani. 

Sema na nafsi itulie na ijue hauiishi miujiza bali unaiishi Baraka ya Mungu.

Ubarikiwe sana ndugu, amina.