Uvumilivu ni moja ya tunda la roho, soma Galatia 5:22.
Tunda la roho ni ile tabia ya Yesu Kristo kuumbika ndani ya
moyo wa Mwanadamu, yaani ni kule kuchukua tabia ya Yesu Kristo.
Watu wengi katika maisha hawapokei uponyaji kamili kutoka kwa
Mungu na ukombozi wao kutoka vifungo mbalimbali haukamiliki kwa sababu tu
hawavulimii mahali walipokusudiwa na Mungu, nasi twajua kuwa ukombozi una hatua
hivyo mjoli mwenzangu katika Bwana tuwe wavumilivu ndiyo tunda la roho na ndio
ukristo hata Yesu Kristo mwenyewe alivumilia mpaka mauti tena mauti ya msalaba nasi
tukapata wokovu kwa neema yake.
Waswahili husema mvumilivu hula mbivu, na pia husema subira
yavuta heri yaani kusubiri au kuvumilia kunavuta Baraka karibu nawe.
Yakobo 5:7-8; Uvumilivu ndiyo miguu ya kukufikisha kwenye
hatma au majaliwa yako. Soma zaidi Waebrania 11:37, Rumi 8:35-37 na Waebrania
6:12.
Kanuni ya kupokea majibu ni kuwa na imani na uvumilivu;
Waebrania 12:16-17
Mifano ya Roho ya uvumilivu katika Biblia;
1.
Mkulima;
2 Timotheo 2:6
2.
Mwanamke
mwenye mimba; Yohana 16:21-22
3.
Wanamichezo;
1 Korintho 9:25
Hivyo tuwe watu wa imani na uvumilivu kwa maana majibu ya
matatizo yetu yana umri mkubwa zaidi kuliko hata matatizo yenyewe. Yaani kabla
ya shida yako kuja uponyaji ulishakuwapo tayari, Tumwamini Mungu na tuvumilie
katika kristo kuyashinda yote.
Nabarikiwa na somo hili la Mwl. Peter shujaa wa UMINA na wewe
barikiwa katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti, Amina.
No comments:
Post a Comment