BIBLIA ni Agano, Ahadi, Usia wa Mungu kwa wanadamu, lakini siri kubwa ni kuwa Neno ndani ya Biblia ni zaidi ya maandishi ni pumzi ya Mungu, ni uungu wa Mungu; NENO ni Mungu. Biblia
inasema hapo mwanzo kulikuwapo Neno naye Neno alikuwapo kwa Mungu naye Neno
alikuwa ni Mungu [Yohana 1:1], na pia Biblia inasema hapo mwanzo dunia ilikuwa
utupu naye Roho alikuwa juu ya vilindi vya maji
akisubiri Neno apate kulitekeleza [Mwanzo 1:2]. Na Yohana mtakatifu
anatuhakikishia kwa habari ya Yesu wa Nazareti kwamba lile lililokuwepo toka
mwanzo, walilolisikia na kuliona kwa macho yao na kulitazama na mikono yao
ikalipapasa ndio NENO la Uzima. Isaya 9:6 anatabiri kwa habari ya ujio wa Yesu
wa Nazareti (Mungu mwana) duniani ambaye ni Neno la Mungu ya kuwa ni Mfalme wa
Amani, Mungu mwenye nguvu na Baba wa milele.
Hata pale Tomaso mtume wa Yesu wa Nazareti alipomuomba awaonyesha Baba
wa Mbinguni kuwathihirishia ili na wao wawe na uhakika zaidi pasipo shaka,
lakini Yesu ajibuje kwa swala hilo, akamwambia Tomaso umekuwa nami siku zote
hizi bado unasema nikuonyeshe Baba.
Hakika
Neno ni Mungu, Gedioni aliyekuwa kijana akiwa hana hata habari ya kuwa mtu
mkubwa, lakini Mungu akamtokea kupitia malaika wake na kumwambia “Gedioni ee!
Shujaa”, cha ajabu kwa Neno hilo ambalo ni Mungu; Gedioni akawa shujaa mara
[Waamuzi 6:11-12], hivyo Neno ni Mungu na ni nafsi ya pili ya Mungu na ni Mungu
hakika.
Neno
pia ni mzigo; ambalo ni kama ujumbe mzito ambao unapaswa kufikishwa sehemu
husika kwa wakati ulioamriwa [Malaki 1:1], kumbuka habari ya Yona nabii
alipojaribu kukimbia na uponyaji wa Ninawi, kwa sababu ni mzigo wa walengwa
wengi aliokuwa amebeba akasababisha hata meli kutaka kuzama, kwa kuwa ni watu
wengi aliowabebea uponyaji na Hatma ya maisha yao ilikuwa juu yake, kwa hivyo
ya kwake yote aliyopanga hayakuwezekana bali kutimiza tu yale yaliyokuwa ya
Bwana, (ndugu ukiwa na agizo la Bwana usitulie kwa kuwa ni mzigo utakaokukula
mpaka ukatende sawasawa na agizo hilo). Ukisoma kwa habari ya Semioni na Anna nabii
mke ule mzigo waliokuwa nao wa kusali kwa habari ya mkombozi wa dunia yaani Yesu wa Nazareti na sala zao zilimusukuma hata malaika Gabrieli kwa wakati ulioamriwa na Mungu
kuwatokea kuhani Zakaria na Bikira Maria kama uthihirisho wa sala zao juu ya kuzaliwa mkombozi.
Zaburi
82:5-7; inatusistizia ya kuwa sisi ni miungu na wana wa Mungu aliye juu sana,
hivyo tunapaswa kujitambua kuwa uungu u ndani yetu pale Neno la Mungu ambalo ni Mungu
liwapo sehemu ya maisha yetu. Tunapaswa kujitambua hakika, kwa maana mrithi
awapo kama mtoto hana tofauti na mtumwa ingawa ni Bwana wa vyote [Galatia 4:1].
Jitambue na tambua Nguvu iliyomo ndani ya NENO ambalo ni Mungu tunasoma pia
habari ya Mama Msamaria alipoonana na Yesu wa Nazareti ambaye ni Kisima cha
maji ya uzima (Yesu) akiwa amekaa juu ya kisima cha Yakobo kirefu, bado mama
Msamaria alikuwa akihangaika kutaka maji ya mbali na yasiyokata kiu hali maji
ya uzima yalikuwa karibu yake na akizungumza naye. jifunze kitu hapo kwanini wanadamu hutanguliza
dharau mbele hata pasipo kujua kwa kina uwezo ulio ndani ya wanadamu kwa sababu
unatofautiana sana, na ni heshima pekee ndio hufanya uweza ndani ya Mwanadamu kuwa
na faida kwa Mwanadamu mwenzake. Huyu Mama Msamaria alimchukulia Yesu wa
Nazareti kama Myahudi tu wa kawaida na kumbe alibeba uponyaji wake na suluhu ya
maisha yake ilikuwa juu yake kwani yeye ni Mungu, ona huyu Mama alimwita Yesu “we
Myahudi”, lakini dhidi Yesu alivyokuwa akifunuliwa kwake huyu Mama akaanza
kubadilika katika viwango vya heshima alivyokuwa akimuchukulia, unaona Yesu wa
Nazareti alivyoongea nae kwa kina yule Mama akamwita “Bwana”, jinsi alivyozidi
kufunguka akamwita tena “Bwana”, kisha baadae akamwita “Nabii” na alipofikia
kumwita na kumtambua kwamba ni “Kristo”, na NENO ndani yake ni Mungu kabisa,
historia yake yote ikageuka na kufanyika mpya kabisa na saa ile ile yule Mama
Msamaria akageuka na kuwa “Mwinjilisti na Nguvu sana” [Yohana 4:7-26].
Kijana
wa Bwana jitambue sasa kwani kwake hakuna uzee, kama vile Maombolezo 3:27-28
inavyosema ya kuwa ni vema Mwanadamu aichukue nira wakati wa ujana wake hali
ana Nguvu na akae pekee yake na kunyamaza kimya huku akiitazama njia yake tangu
awali kwa sababu ni Bwana ameweka hayo juu yake. Kijana unapaswa kuielekea njia
ya Bwana shetani anajua kwamba wnadamu hawana lolote na yoyote wanayoyafanya ni
kwa ajili ya miili yao na maisha haya ya duniani pekee na wala hawajui chochote
kuhusu baada ya hapa na ndio maana katika Ayubu 2:4 Shetani anasema 'Ngozi kwa
Ngozi' kama vile wanadamu mwisho wa kufikilia kwetu ni kuhusu vinavyoonekana sasa na
wala hatuna habari na vile tulivyoandalia rohoni, kwa maana hata Warumi 7 pia
inatufahamisha kuwa miili yetu ni ya mauti na wala haiwezi kumtii Mungu.
Mwambie
shetani najitambua na kwamba nitayaishi yale yamupendezayo Mungu kwa maana ndio
Uzima wa milele na NENO ndaliishi hilo ili niwe na Amani, huru na kweli ikae
ndani yangu daima kwani ndiye Mungu wala kuhukumiwa nafsi kusiwepo moyoni
mwangu, mwili wangu kwa uweza wa Roho mtakatifu katika jina la Yesu Kristo wa
Nazareti hautakuwa na uwezo tena wa kunivuta kwenye dhambi pasipo dhamiri yangu
kupenda hivyo na siku zote nitatenda mema, ee’ Mungu nisaidie niwe huru milele,
Amina.
No comments:
Post a Comment