1 Timotheo 3:9 inatusisitiza ya kwamba
tuishike siri ya imani katika dhamiri safi.
Dhamiri maana yake ni ule uwezo wa fikra zetu kutofautisha yale yaliyo mema na mabaya na kutenda sawia. Hivyo dhamiri ni namna ya fikra kuweza kutofautisha au kufanya maamuzi sawasawa yale mtu ayadhaniayo kuwa ni mema au mabaya. Dhamiri ina muhimu na ni msaada kwetu ikiwa na msukumo wa Roho mtakatifu kwani hututaka sisi kufanya mema na kuacha mabaya yaani yale tu mtu ayafikiriayo kuwa ni mema ambayo kweli ndiyo hivyo huyatenda hayo. Wengine hufananisha dhamiri ya mtu ni kama saa iliyosetiwa sawasawa ili
kutekeleza kusudio muhimu, lakini kama ikisetiwa vibaya (na maana kama haijulikani ndani yako lipi ni jema na lipi ni baya), dhamiri yako itakuelekeza katika mapotofu, yaani kufanya maamuzi yaliyo changanyika au yasiyofaa. Hivyo dhamiri ili iwe safi inategemea msukumo wa ndani wa Roho mtakatifu ambapo mtu kule kuweza kuutambua na kuunganishwa na fikra zake kutamuwezesha kutenda mema siku zote.

Dhamiri siku zote haiwezi kuwa mwongozo
wa kufuata pasipo kristo, Mtume Paulo anasema amemtumikia Mungu katika dhamiri
safi katika maisha yake yote (Matendo 23:1), hata alipokuwa anawaua wanaoliitia
jina la Yesu (Matendo 26:9-11) alijua anatenda mapenzi ya Mungu kwa sababu
alifikiria (dhamiri yake ilimuongoza) kwamba anatakiwa kilipinga jina la Yesu,
hivyo dhamiri yake ilifanya kazi sawasawa lakini ilisetiwa isivyo sawasawa, kwa
hiyo hata sisi tunapaswa tujiulize je’ vile tunavyodhani ni sahihi yaani yale
mema na mabaya tudhaniavyo ndivyo ilivyo kwa Mungu? Na je maamuzi yetu juu ya
mema na mabaya yanasimamia katika Kweli halisi ya Mungu?, yaani dhamiri zetu
zimesetiwa sawasawa? Jiulize ndugu.
Ni kwa namna gani dhamiri inakuwa safi,
biblia katika Warumi 3:23 inasema wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na
utukufu wa Mungu, sasa ni vipi na ni kwa namna gani dhamiri zetu zinakuwa safi
mbele za Mungu?. Katika agano la kale sadaka za kuteketeza na matoleo
havikutosheleza (Waebrania 9:9 na 10:1-4), kwa hivyo ni damu ya Yesu pekee yake
katika agano jipya ndio iwezayo kusafisha Dhamiri ya mtu (1 petro 3:21). Kwa
hiyo basi katika ubatizo tunafanywa wapya katika dhamiri zetu yaani kama ni saa
inakuwa imesetiwa sawasawa, huku tukiamini damu ya Yesu ndiyo ioshayo dhambi
zetu (Matendo 2:38 na 22:16).
Na je’ ni kwa jinsi gani dhamiri
inakuwa na mtizamo ule ule, dhamiri safi inatunzwaje na utii wetu katika
matakwa ya Mungu. Kumbuka ya kuwa tusipotenda lile tunalofahamu kuwa ni jema ni
sawa na kutenda dhambi (Yakobo 4:17) vile vile kushindwa kutokufanya yale
yaliyomabaya ni dhambi pia. Kufanya kwa utakatifu na ukweli utokao kwa Mungu
inatujengea kuwa na dhamiri safi (2 wakorintho 1:12), kule kufanya lililojema
na la haki kiukweli kunaunda ujasiri ndani yetu. Kwa hiyo vile unavyofanya
yaliyo mema zaidi na zaidi ndivyo uwezavyo kujitenga na yale yaliyo mabaya, na
ndivyo bora na safi dhamiri yako itakavyokuwa ndani yako. Kwa neema ya Mungu
hata waliokubuhu katika dhambi wanaweza kusafishwa dhamiri zao kupitia imani
katika kristo yesu wanaweza kufanywa dhamiri zao kuwa safi lakini ujue pia
kunauwezekano wa kuharibu dhamiri zetu.
Kwa namna nyingi dhamiri zetu zinaweza
kuharibiwa; (i)kwa kutokuitii dhamiri ambapo ni kutenda dhambi (Warumi
14:22-23), (ii)kwa kuichakachua dhamiri ambapo inapelekea kutokuwa na imani (1
Timotheo 1:15), na pia (iii)kwa kuichoma dhamiri, hii inapelekea
kutokukuyakubali mafundisho ya Mungu na kutoamini tena (1 Timotheo 4:1-2).
Kuiacha dhamiri au kuiharibu ni hatari sana, kwa sababu dhamiri iliyo na hatia
inapelekea mtu kuwa na dhamiri ngumu yaani kama usemi usemavyo sikio la kufa
halisikii dawa na dhamiri inakuwa hivyo kwa hiyo ule muunganiko na Mungu
hauwepo tena mfano; mtu akiwa na dhamiri ngumu haoni haja hata ya kwenda
kanisani, hudumani wala hahukumiwi moyoni mwake maana amepoteza ile signal ya
Roho mtakatifu anakuwa yupo yupo tu kule kwa kwenda haendi na kule anakopaswa asiende
yeye ndio anaenda (Waebrania 10:25). Hii inamfanya awe mgumu hata kutenda
yaliyo ya haki katika maeneo mengine pia ya maisha yake, na kama nilivyosema
dhamiri ngumu inapelekea moyo wa kutokuamini (Waebrania 3:12) kwa hiyo ule
uwongo mkuu wa dhambi na kutokutenda mema unafanya mtu kuwa na moyo mgumu, Na
moyo mgumu humfanya mtu kuanza kuuliza hata kile alichokiamini mwanzoni.
Ndugu tunaweza kuomba pamoja maandiko
yaliyo katika biblia - waebrania 13:18; ya kwamba “tuna imani kuwa tuna dhamiri
safi na katika kila kitu tunapenda kufanya yaliyosawa daima, Amina”.
Mtume Paulo anasema nakushukuru Mungu
ambaye ninakutumikia kwa dhamiri safi (2 Timotheo 1:3), kama sio na dhamiri
zetu hazijakuwa ngumu bado ya kwamba hatutasikia, hivyo tunapaswa kumwendea
mwana wa Mungu(Yesu kristo) ili asafishe dhamiri zetu kwa damu yake, na pia
turirejee neno la Mungu ili tupatekufahamu sawia kwamba yapi kweli ni mema na
mabaya mbele za Mungu. Karibu katika familia ya Mungu kupitia makutaniko ya
mara kwa mara popote wanapoliitia jina la Kristo Yesu ili kumuomba Mungu
atuwezeshaye kuwa na dhamiri safi daima, Je’ kinini kinakuzuia usimtumikie
Mungu katika dhamiri safi leo?.
http://www.slideshare.net/Recknald/depend-on-jesus-of-nazareth-man-is-a-mere-vapour
http://www.slideshare.net/Recknald/depend-on-jesus-of-nazareth-man-is-a-mere-vapour
No comments:
Post a Comment