#YESU WA NAZARETI NI MHASIBU WA WAHASIBU

     Nashuhudia!  mimi ni mhasibu bali nasema kweli ya kweli aliyemkuu wa wahasibu wote duniani ni Yesu wa Nazareti. Na ya kwamba yote katika yote si kuhusu kuchapa kazi sana, au kuhusu utalaamu sana wala kuwa na akili nyingi bali ni kuhusu NEEMA YA MUNGU (Waefeso 2:8-9 na Warumi 3:24). Tunakuwa, tunaongezeka ukuu,utashi na maarifa na kibali ni tu kutokana na neema zake, iwe unajua au haujui biblia inasema wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu maishani mwetu hivyo neema  yake ndiyo inatosheleza kutukamilisha.  Utashi, akili tulizonazo chanzo ni yeye kwani biblia inasema yeye ni chanzo cha maarifa ukimcha (Mithali 9:10) hivyo yote tuyafanyayo tuyawezayo ni kwa sababu ya roho wake hata nguvu tulizonazo katika kutenda kazi ni zake na uweza ndani yetu unatokana naye.  Saa ingine nawaza unafanya kazi wala si kwamba unaweza sana wala si kwamba umewazidi wengine ama kazi yako ni vema sana yaani ni wa kawaida tu lakini sasa kile kibali hakika ni neema ya Mungu, ndiyo inayokufanya usiwe wa kawaida. Hata wafalme wa dunia hii mpaka waamini kuwa kuna Mungu tusiyemuweza tusiyefananishwa naye aliyetuzidi wote na muumbaji wa vyote ndipo waweza tawala, yaani kule kuamini duniani kuna Mungu anayefanya mambo yote atakavyo; kuruhusu au kuzuia mamlaka ina yeye. Lakini basi kule kuamini kwetu, kumtii na kunyenyekea mbele zake tunapata kibali zaidi, mafanikio zaidi na Baraka nyingi zaidi. Biblia inasema katika Wagalatia 6:7; Mungu hadhihakiwi ndio maana yoyote aliyemkuu awe mfalme au raisi wa nchi pindi akufurupo moyoni mwake awazapo kujiinua kujifananisha Mungu mwenyezi atakapo kujifanya mungumtu anguko lake huwa hapo. Na hakuna mchawi mwenye nguvu zake mwenyewe ni nguvu za Mungu ila ni kwamba zatumika visivyo na utukufu ni wa yeye pekee yake aliyefanya vyote. Shetani alikuwa kerubi afunikaye (Malaika wa Mungu) kutenda kinyume na maadili yaliyompasa kukawa ndio sababu ya anguko lake (Ezekieli 28:13-18), hivyo si nguvu zake shetani wala nguvu za giza bali ni Nguvu za Mungu chanzo chake. Manabii au waonaji wana nguvu za Mungu ndio! Na watenda kazi kwa utukufu wake Mungu na wala sio wao, na ndivyo wawavyo na haki mbele zake walakini waangukapo na kushupaza mioyo yao pasipo kutubu kwa mwenyezi Mungu hawana tofauti na waganga na wapiga ramli kwani utukufu wa Mungu huondolewa kwao, kwa maana hata waganga saa ingine hufanya hivyo kwa sababu nguvu wazitumiazo chanzo chake ni Mungu kwani hata shetani wamtegemeaye alitoka kwa Mungu ila laana ndiyo iliyomfanya awe hivyo na wote wapokeao kutoka kwake wapokea vilivyolaaniwa, na ndio maana wao sasa hutenda kwa utukufu wao wenyewe na yeye ajitukuzaye (yaani shetani) hivyo hakuna haki ya Mungu ndani yao bali hukumu. Kumbuka Yesu wa Nazareti pekee ndiye aliyesema Yeye ni Lango la Mbinguni na wengine wote wadhaniao wanayombingu ya kuwapeleka wawafatao ni wezi na hawana sehemu katika Ufalme wa Mungu.
  Hivyo iwe unamjua au humjui, unamtii au humtii, unanyenyekea mbele zake au hunyenyekei atabaki na ataendelea kuwa Mungu tu na katika nafasi yake ataendelea kuwepo, na wala hakuna mwingine wa kulingana naye, hivyo kiburi chako, majivuno yako hayabadilishi maana wala hayatathibitisha kuwa duniani hakuna Mungu, kwa maana hata katika kutenda kazi kwako kwa sababu unaongoza watu wake Mungu, yeye ndiye anayeruhusu au kutoruhusu baadhi ya mambo uyafikiriyo kutenda kwa watu wake. Cheo chochote ulichonancho iwe katika nchi, au mashirika ya jamii au kampuni za watu kibali cha toka kwake na anayekupa ni Mungu, Nguvu zote zina yeye na yeye ni chanzo cha vyote, utasema ni nguvu za giza lakini ujue Mungu alifanya vyote matumizi ya nguvu hizo kwa haki na kwa utukufu wa Mungu ndio yanayokufanya uwe mtakatifu na upate haki mbele za Mungu na kisha uzima wa milele na ndio maana biblia inasema naweka mbele yako laana na Baraka, mauti na uzima uchaguapo vyema (nuru) utafanikiwa, utabarikiwa na kupata uzima wa milele, na uchaguapo vya giza; vyote utavyokuwa navyo ni vya muda tu huku laana, mauti na hukumu ukiwa ndio urithi wake. Chagua Mungu muumba wa vyote leo na sio miungu mingine, chagua nuru uijue kweli yake yote, chagua Yesu Kristo wa Nazareti, Amina.