# DUTU YA KIROHO [SPIRITUAL SUBSTANCE]

 Dutu ni kiini cha kitu au mtu ambacho ndio asili yake au ndio msingi wa mwanzo wake. Kikristo ni ile imani tuliyonayo kutokana na Neno la Mungu, itupayo upako wa Mungu (Nguvu ya Mungu) wa kutuwezesha kutenda yote yasiyowezekana kwa hali ya kawaida.
       Kwa maana ya kawaida kabisa ni kile kitu ambacho kutokana nacho, au kutoka humo, mtu yoyote, kitu chochote, uhai au mwili hufanyizwa. Hata vitu halisi vimefanyizwa kutoka visivyo halisi vya rohoni, yaani kutokana na kiini au dutu ya namna fulani.
        Kwa mfano kwa Neno la Mungu (dutu) dunia iliumbwa na vyote viijavyo ikiwa ni pamoja na Mwanadamu na wanyama, Mfinyanzi anatengeneza vyungu kutokana na dutu iitwayo udongo. Seremala naye anafanyiza samani za ndani [furniture], anajenga nyumba, kutokana na dutu iitwayo mbao. Barafu nayo inaundwa na dutu iitwayo maji na maji hutokana na dutu iitwayo gesi - hii ni kisayansi.
          Hivyo mwanzo wa uumbaji wa chochote ni dutu yake au kiini. Kwa hiyo kama katika mifano hiyo, tunaishi, tunatengeneza, tunaunda na kuumba vitu mbalimbali na visivyo vya kawaida kutokana na dutu tuliyonayo yaani ile imani ktk kristo tuipatayo kutokana na Neno la Mungu nayo hutupa upako wa kutuwezesha kuumba, kuunda, kutengeneza vitu, na hiyo imani/upako yaani dutu ambayo ni kwa namna ya kiroho ndio kwa kiingereza ni “spiritual substance” kuna hatua ambayo mkristo anafikia ambayo unaihisi kuwa unayo dutu ya kiroho na kutambua kabisa kuwa ipo ndani yako na ndiyo inayokuwezesha kufanya mambo fulani fulani (maarifa ya Neno la Mungu hutuwezesha tufikie hapo). Imani kwa kweli inafaa sana kuongezeka kila iitwapo leo ndani yetu kwa mkristo yeyote, hiyo itatufanyizia upako wa Mungu ambao ndio dutu ya kiroho yakutuwezesha sisi kwa lolote na kufanya chochote kwa maana ni Nguvu ya Mungu (Wafilipi 4:13), Amina.

Tafakari;
Waebrania 11:1; “Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”. (“Now faith is the substance of things hoped for, the evidence of things not seen”).
Warumi 10:17; “Basi Imani, chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa Neno la KRISTO”. 

No comments:

Post a Comment