Somo la Yesu kwetu ni nini?
Uwana wa Mungu ni uwakilishi wa Mungu Baba aliyeketi ktk kiti cha enzi, kama yeye alivyo mbinguni ndivyo nasi tulivyo duniani (Wakolosai 2:9-10, Waebrania 1:1-10).
Na usiwe na shaka kuhusu hili kwani kuna haki hiyo (Yohana 1:12-13).
Sasa ktk Mathayo 16:13-20; pale kaisaria-filipi ndipo ilifika hatua na saa ile ya Yesu kufunuliwa kama mwana wa Mungu ambao huo ufunuo ndio mwamba wenyewe ambapo kanisa limejengwa kiroho na imani yetu ktk yeye inasimamia hapo.
Ule ufunuo kupitia Petro saa ile ( peter confession), ule uthihirisho na uthibitisho mkuu wa Yesu Kristo pale kaisaria-filipi alipokuwa amekaa na mitume chini ya miti ya miforsadi (mulberry), ndipo ulipo weka msingi na maana kuu ya huduma yake duniani.
Katika hatua zote za maisha ya Yesu duniani, wakati akisubiri kufunuliwa kwake mioyoni mwa watu ile saa iliyokusudiwa na Mungu baba, ukamilifu wake ulifikiwa kwa watu kumuelewa yeye aliye mwana wa adamu kama mwana wa Mungu, na ilimchukua muda kueleweka hivyo sababu ufahamu wa binadamu unachelewa kuchanganya (slow to wit) inapokuja kuhusu mambo ya rohoni, na hiyo ni kweli.
Yesu alipita stage ya utoto kama mwanadamu wa kawaida (conscious inakuwa dimly ktk kujitambua), then ya pili ya kujitambua, roho anaanza kujifunua ndani yake ktk ujana na mpaka ukubwa wake (pale conscious iko light-up, anakuwa aware mambo mengi ya divinity na mission yake), ya tatu ni ubatizo, kujithihirisha kwa Mungu kwake kama mwanae na kuanza huduma kama mwalimu wa ufalme wa Mungu, then mwalimu na mponyaji, hapa watu wa karibu walimjua kama mwana wa adamu na wengine wakamuita mesia, wengine wakataka hata awe mfalme wa wayahudi, na stage ya 4 na ya mwisho ilianzia pale kaisaria-filipi alipofunuliwa kama mwana wa Mungu na mpaka kusulubiwa kwake na kifo cha msalaba, na ktk stage zote hizo Yesu hakujikuza bali ulikuzwa kwa namna alivyokuwa anaishi, its stages kama ukuaji wa kipepeo kutoka buu, its marked the new start when was observed change supernaturally organically.
Can you be the son of God? Unaweza kuwa mwana wa Mungu?
Yes! nasema unaweza kuwa mwana wa Mungu leo, kupitia kumwamini kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yako.
Haya basi, nawe mwana wa Mungu mwenye haki kwa roho wake mtakatifu kupitia ile imani ktk kristo Yesu (Wagalatia 3:26), ktk kujitambua kwako hivyo pokea funguo za mamlaka kuyatenda yaliyo makuu duniani kama mbinguni, na huku sifa kuu ya umwana ya kuyatenda yaliyo mapenzi ya Mungu Baba, hata yawe magumu vipi iwe ni jadi yako, naye Mungu Baba akuwezeshe pale uyatendapo hayo mapenzi yake (Yohana 5:19; Luka 22:42-43) 🙏🏾.