Saturday, June 29, 2024

#PAY ATTENTION/ KUWA MAKINI


Sikio lina shepu kama vile tumbo la uzazi, ikiashiria chochote utachosikia kizuri ama kibaya, kitakuwazisha kama kusema kukutungisha mimba, na kupelekea kuzalisha kitu au jambo kama mimba/wazo lake kwa wakati na ule muda muafaka.

Hivyo kazi ya sikio ni kupelekea kuzalisha matokeo ya kile unachokisikia na kukisikia tena na tena, hakuna makosa hapo ni kutokeza matokeo. Na ndio maana hata biblia inasisitiza kuzalishwa imani kupitia kusikia neno la Mungu (Warumi 10:17). Na sasa kama imani huja kwa kusikia, nashangaa ni yepi mengine huja kwa kusikia? je' ni vipi kama hata unavyojisikia leo, vile unavyofeel vimepitia mlango huo huo wa sikio?

Na ndio maana tunasema PAY ATTENTION yaani KUWA MAKINI, sababu hata wakati wa Covid19, ni taarifa tulizosikia mara kwa mara ndizo zilitushitusha na kutupelekea kuwa na hofu kuu hata kuogopana na wengine kujificha. Hivyo hata ATTENTION ni kama currency ktk kizazi chetu, yaani ona ukisema pay attention, ni ya thamani, ni kama vile lipia pesa, attention ndio pesa yenyewe, sio rahisi ni gharama ni sacrifice, na hivyo ukipay attention utakipata na usipopay attention hutakipata, na pia attention ikipatikana inatransact na kunakuwa na exchange sababu inaweza onekana na kuhesabika, watu wanatransact agenda zao kupitia hiyo, mipango, kurubuni watu, kufunga na kufungua watu kifikra, kunadi vitu, Mungu na biashara na hata kuwaibia, na ni namna nyingi zinatumika kuipata attention kwa watu kwa mifumo yote ya mawasiliano. Na hii ni kweli kabisa nimeona ushawishi wa madalali, wapiga debe, watumishi wa Mungu feki na wa kweli, watu wa biashara ya mtandao, wa kwenye upatu, zama za babu wa roliondo, waganga, wanasiasa ile nguvu inayotumika kupata attention za watu ni kubwa naweza sema ni uwekezaji ni mtaji sababu ya tumaini la faida inayotokana na attention hizo.

Na ndio maana social dilemma documentary inasema "kama hulipii product, basi wewe ndio product, sisi ni products sokoni,  ule umakini wetu ndio product yenyewe inayouzwa kwa advertisers. Mitandao ya kijamii sio nyenzo/chombo; ni dawa tena ya kulevya." Attention za watu ndio dhahabu ya social media.

Yesu alisema kuwa mwangalifu/makini na unachokisikia (Marko 4:24). Kwa maana matamanio yetu hayatuamulii hatima zetu bali vile tulavyo. Yaani hiyo  ni vya rohoni na mwilini; iwe kwa masikio, macho, ndimi, ngozi, pua. Unajua unaweza kuwa na shauku ya kupunguza mwili na kuwa na afya njema, na hakuna kitakacho kusaidia kama unakula kula hovyo, ndivyo ilivyo na mambo ya rohoni pia. Hivyo chunguza na kuwa mwangalifu na unacholisha roho yako, unakuta vitu vya dunia vinakutawala, miziki ya kidunia inakushika, kuangalia picha za ngono, kuangalia filamu za kutisha na hata huogopi tena, kupenda sana zana za upako unazouziwa, hivyo angalia sana shauku ya nafsi kutamani vya dunia sana isikufunge usijekengeuka na ukajipoteza. So, be selective sio kila kitu cha kupay attention, usije corrupt nafsi yako, vingine ni kuvipuuzia ili kulinda nafsi yako.

Ona kwenye miji mikubwa; chokoraa/homeless wanapenda kuokota chakula kwenye matakataka ya nyumba za watu wengine. Kwa hiyo kama unataka kugeuzwa na kukuwa kifikra we uliyeamini, acha kuwa chokoraa kiroho, ungana kanisa karibu nawe ukuwe. Kula na tafakari (feed&chew) neno la Mungu na sio ya kidunia yaani toxic worldly content. Wafuate watumishi wa Mungu, walimu watakaokufunza kweli ya Mungu na kukuvuta katika utakatifu. Kumbuka njiwa hula vya kijani na kunguru penye miozo; cheki rangi ya muonekano wao, kuwa njiwa na sio kunguru.

Mwisho soma waraka wa Paulo kwa wafilipi 4:8, ubarikiwe na Bwana, amina.🙏🏾