Saturday, April 11, 2026
Tuesday, March 31, 2026
Tuesday, December 9, 2025
THE IMPACT OF INCLUSIVE SERVANTHOOD ON CHURCH GROWTH; A CASE STUDY OF TANZANIAN CHURCH
ABSTRACT: This study investigated the impact of inclusive servanthood on church growth, with particular reference to selected churches across Tanzania. Inclusive servanthood is understood as a Christ-centered leadership and ministry model rooted in humility, compassion, selflessness, empowerment and love-values demonstrated by Jesus Christ throughout His earthly ministry. This model aligns with Christ’s Great Commission, grounded in Matthew 28:18–20, which continues to guide the Church today. It emphasizes service to humanity rather than mere church attendance. Servanthood, therefore, forms the foundation of true discipleship and effective evangelism, reflecting the biblical mandate of Jesus Christ to “make disciples of all nations.” The research was guided by three main objectives: (1) to explore members’ and leaders’ understanding of inclusive servanthood in relation to church growth, (2) to assess the relationship between inclusive servanthood and effective evangelism, and (3) to identify the major factors influencing people to join and remain in churches. A descriptive research design was employed, combining both quantitative and qualitative approaches. Data were collected using open- and close-ended questionnaires and semi-structured interviews from 40 respondents across 24 churches in Tanzania. The participants included 18 church leaders (bishops, overseers, founders, coordinators, senior pastors, and elders), 9 church servants (secretaries, children’s teachers, project workers, intercessors, and ushers), and 13 ordinary members. Secondary data were obtained from relevant handbooks, theological and academic publications. Quantitative data were analyzed using SPSS version 27, applying Pearson’s correlation coefficient, while descriptive statistics such as frequencies, percentages, and charts summarized the findings. The results revealed a positive correlation (r = 0.181) between inclusive servanthood and church growth, signifying that while the relationship is modest, inclusive servanthood plays a key role in shaping the culture, accountability, and evangelistic effectiveness of the church. Most respondents (over 90%) agreed that inclusive servanthood promotes effective evangelism, strengthens discipleship, and enhances member retention. However, the findings also showed that many churches lack a formalized model or documented standards for inclusive servanthood, with practices often applied informally. Limited awareness, leadership resistance, and inadequate training were identified as barriers to full implementation. The study concludes that church growth is multidimensional, but inclusive servanthood remains a vital determinant of sustainable expansion, unity, and accountability. Where leaders model Christ-like service and empower all members to participate in ministry, the church experiences increased effectiveness, transparency and community engagement. Conversely, weak or authoritarian leadership undermines evangelism and contributes to stagnant growth. The research recommends that churches institutionalize inclusive servanthood by developing documented models, training programs, and evaluation committees to monitor adherence. Leaders should embody humility, transparency, and accountability while encouraging shared responsibility among members. Moreover, youth and family engagement, mentorship programs, participatory evangelism, and digital ministry expansion were identified as practical strategies for enhancing church growth. Implications of the study suggest that church growth can be significantly strengthened through contextualized leadership approaches that integrate servanthood with evangelistic practice. A values-based model of inclusive servanthood is essential for fostering unity, spiritual maturity, and sustainable ministry outcomes. Finally, the study recommends further research across a broader regional scope, including East and Central African contexts, and comparative studies between Pentecostal and non-Pentecostal traditions. Future research should also explore moderating factors such as church finances, leadership structures, and socio-economic influences on servanthood practices. In conclusion, inclusive servanthood is not merely a leadership model but a biblical mandate central to the mission of the Church.
https://www.linkedin.com/in/recknald-lucas/overlay/Education/1134096655/treasury/?profileId=ACoAAAv01qMBfjRPBqieb33hX25OGrLEwMe7B9U
Contact DR RECKNALD through E-Mail: recknald@gmail.com or +255755286021 for more details on this study.
Monday, July 14, 2025
#ARE YOU; A MARTHA OR A MARY?
Je, wewe ni Martha au Mariam?, Jiulize.......
Katika biblia, Luka 10:38-42 inaeleza vizuri wasifu wa hawa wawili namna walivyojiweka kwa Bwana na matarajio yake kwao na kisha kuwaambia la msingi kwao kulitenda ktk yote pale yeye akiwepo kama fungu lililo jema zaidi.
Biblia inatuonyesha YESU alipokuwa karibu kuingia nyumbani mwao; MARTHA alikuwa wa kwanza kumlaki na kumkaribisha.
YESU alipokuwa kati yao: ni MARIAM ndiye aliyeketi miguuni mwake Yesu kujifunza na kusikiliza maneno ya YESU.
MARTHA alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi, kusumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi uweponi wa Bwana huku akimwacha YESU na umbu lake (na kama kumuandalia chakula jibu la YESU ni Yohana 4:31-34).
YESU aliweka wazi na kufunguka msingi wa yote unaotakiwa na wote; ambao ni mmoja tu kukaa karibu naye YESU, kumkaribia yeye huku moyo umemfungulia. Fungu hilo jema ndiyo wakina MARIAM huchagua lidumu kwao.
Ndiye YESU mwenyewe aliyesema kwa lile jambo jema alitendalo kila itakapohubiriwa injili yake ulimwenguni kwote litakumbukwa vizazi hata vizazi na kutajwa kwa kumbukumbu lake, sasa sio la MARTHA bali la MIRIAM; kwa maana wakati MARTHA akitumikia (kuserve supper) karamu ile ya mwisho waliyomwandalia kama familia ya Simoni huko Bethania siku 6 kabla ya pasaka, yeye MIRIAM alitwaa ratli ya marhamu ya nardo safi ile chupa ya Alabasta yenye marashi ya thamani kubwa aliyoinunua kwa kujilimbikizia pesa aliyopata kwa mwaka mzima kama ya USD 17,000's/TZS 44M's kwa sasa, huyo alitambua thamani ya Bwana maishani mwake, akammiminia marashi hayo yote YESU kichwani pake na kumpakaa miguu na kisha kumfuta kwa nywele zake mpaka nyumba nzima ikanukia marashi hayo, naye YESU akasema kama nabii kwa waliopinga tendo hilo kuwa ametenda lililo jema wamwache alitende kuuandaa mwili wake kwa maziko (Yohana 12:1-8; Mathayo 26:6-13; Marko 14:3-9).
Hivyo huu ni msingi kwa mambo yote ya Mungu kipaumbele kuwa sio ile kazi yake Mungu uitendayo bali kuwa karibu na Bwana Mungu wa hiyo kazi ili uitende vizuri kwa wepesi na kirahisi zaidi.
Tunaona utofauti baina yao MARTHA na MARIAM pia hata wakati wa Kifo cha Lazaro kaka yao:
Yohana 11:20-27
YESU alipofika uweponi mwao karibu nao, MARTHA pekee yake kutoka msibani alikuwa wa kwanza kumlaki.
Neno alilolisema MARTHA kwa YESU "KAMA UNGALIKUWAPO HAPA NDUGU YANGU HANGALIKUFA". Kauli ile namna alivyoisema, imani yake ya kusitasita na mazoea yake kwa Bwana haikuleta matokeo mazuri bali iliprovoke/ilileta mjadala badala ya kuleta suluhisho kutoka kwa Bwana.
Yohana 11:28-44
Ni MARTHA pamoja na imani yake ya kuyumbayumba ndiye aliyeenda kumuita MARIAM umbu lake faraghani kufaidi uwepo wa Bwana akisema YESU yupo anakuita. Mahali palepale alipokutana na MARTHA ndipo YESU alikuwepo wala hakuondoka; anga lilelile, uwepo uleule, spoti ileile, mazingira yaleyale MARIAM akamwendea upesi. Lakini kwa moyo wa MARIAM ulivyokuwa alivyotoka msibani kwenda uweponi mwa Bwana si pekee bali wote waliokuwa naye walimfuata. MARIAM alipofika kwa Bwana, na kumwona YESU; ALIANGUKA MIGUUNI PAKE (Unyenyekevu wake ule ulikuwa mkuu sana na moyo uliofunguka wenye tumaini la kufungua mbingu na kumuona Mungu huku na imani thabiti kwa Bwana YESU isiyoyumbishwa na chochote), kwa huzuni na moyo ule wa imani uliofunguka kwa Bwana huku akiwa na matarajio ya matokeo mema. MARIAM akainena kauli ileile kama ya MARTHA kwa namna yake kuwa "KAMA UNGALIKUWAPO HAPA NDUGU YANGU HANGALIKUFA". YESU alipoona huzuni yake juu ya jambo lile na kulia kwake kwa uchungu kama mwenye mzigo mkuu ktk msiba ule kwa namna alivyoinena kauli ile kuliko hata MARTHA alivyojipresent/ alivyojihudhurisha kwake Bwana, kwa maana kwa kulia kwake MARIAM kwa uchungu kuliprovoke/kuliibua kilio kikuu hata kwa wale waliokuwa wamefuatana naye. Ndipo YESU ALIUGUA ROHONI, AKAFADHAIKA ROHO YAKE.
YESU ALILIA MACHOZI HUKU AKIUGUA NAFSINI MWAKE, alipoona tu kaburi alimowekwa Lazaro, AKALIA KWA SAUTI KUU Lazaro, njoo huku nje, naye akafufuka na kutoka nje huku akiwa amefungwa sanda.
Hii yote ilitokea sababu ya namna MARIAM alivyojinyenyekeza na kumheshimu YESU pasipo mazoea kwa hisia ya kweli na ya dhati moyoni mwake mbele za wote msibani kuliko MARTHA (japo naye MARTHA anasehemu yake ktk utimilifu wa jambo lile, kuachwa kwake na uwepo ule wa Mungu ktk Bwana YESU ni changamoto kuu ambayo ufalme wa mbinguni unakutana nayo hata sasa kwa wengi, wengi wapo eneo sahihi, wakati sahihi na wengine wanatumika humo ila wanakosea namna ya kuaccess vya rohoni kutoka kwake YESU kwa kutokuelewa vema namna yake ya kumpokea Roho wake Mtakatifu).
Kinamna ile MARIAM alivuta uwepo wa Mungu, aliprovoke presence ya Mungu na mbingu yake ktk Bwana Yesu kuleta matokeo yaliyoonyesha utukufu wa Mungu katika jamii yao yote. Sasa pamoja na hayo yote kutukia machoni pake MARTHA bado tunaona kutokana na mazoea yake kwa Bwana yeye alikuwa mkavu uweponi mwa Bwana YESU pasipo kuwa na imani thabiti na moyo uliofunguka; hata akaja kumwambia YESU pamoja na ufahamu aliomupa mwanzoni akasema; marehemu ananuka sasa maana amekuwa maiti kwa siku 4, kwa hatua ile Bwana YESU alimkemea kama kusema na shetani mpinzani wake (ndani ya MARTHA kwa kuwa ndiye aliyefungua mlango wa kusitasita ktk imani yake).
Jamii ya MARTHA kama wasifu wake ktk biblia ni kama Mpigadebe fulani hivi kuwaambia mwenzake ingia usafiri na gari kwa ushawishi mkubwa lakini yeye hubaki hapo hapo huku akiacha kina MARIAM wakiexperience the goodness of the journey. Ndivyo ilivyo hata katika Bwana usiwe wa jamii ya MARTHA bali kuwa kama MARIAM.
Ndipo utajua mwenyewe unao ufungua wa kuufungulia ukuu wa Mungu ndani yako utakaofurika maishani mwako na YESU yeye yupo siku zote karibu na moyo wako abisha ili ajifunue ndani yako kwa namna ya ajabu.
Kwa hivyo ni wewe kutune ile frequency ya moyo wako vizuri kwa ile mode/mood aitakayo, namna unavyojisikia ile hali yako ya ndani ya uhitaji, ile shauku kuu ya moyo wako huku ukimuelekea yeye, ukijimimina kwake, na utakapofika hali hiyo atajisikia pia ndani yake na hakutakuwa na pingamizi kwake tena kwa namna yoyote zaidi ya kujifunua kwako yaani Mungu na mbingu yake ndani yako ktk Bwana Yesu kristo unayempokea moyoni mwako kikamilifu kupitia Roho wake ayafunue yote mema maishani mwako.
Be MARYs AND NOT MARTHAs, brothers and sisters; enjoy God things easily🙏🏿.
Tuesday, January 28, 2025
#MWAKA WA KUONA _2025
KUONA KUKUPAKO KUSHINDA
Wangapi wanajivuna kwamba Naona!! Mikono juu! (Kwa maana Yesu anasema nalikuja kwa hukumu ili wanaosema wanaona wawe vipofu na vipofu waone- Yohana 9:39), safi!!, Sasa 2025 sema "Nitatazama, Nitaona"..., Nami nakuombea; nguvu ya kuona iongezeke ndani yako leo, kama mi niitajivyo.
Unajua ukisoma Luka 11:34 inasema; "Jicho lako ni nuru ya mwili wako. Macho yakiwa mazima huangaza mwili wako wote; lakini yakiwa mabovu, mwili wako pia utakuwa katika giza". This means pasipo kuona no direction!..
Jifunze kwa Bathromeo kuona kuna baraka kuu sana, tamani kuona, nasema tena tamani kuona (Marko 10:46-52).
Ng'ang'ana mpaka uone mwaka huu;
Wengi wanatazama, wanapepesa macho, wanaangalia lakini hawaoni, mtu awaye yote asikudanganye, kuna kuona, kuna kuangalia ni tofauti, kuona kunafaida sana, kunakupa maamuzi sahihi, kunakupa amani, kunakukombolea wakati, kunakupa kufikia malengo kwa muda mwafaka, kunayapa maisha maana, mtu anayeona anafocus ya maisha..
Hata ukisoma tena Marko 8:22-25 kuna kipofu yule wa Bethseida alipokuwa anawezeshwa na Yesu kuona akasema naona kama miti inatembea, kisha akamuwekea tena mikono machoni, ndipo alipotazama sana ule umakini ktk kutazama akaona vyote waziwazi!! (yaani ile live bila chenga). Unajua nini pasipo juhudi za kutaka kuona clear huwezi kuona, Roho wa Bwana yupo nasi yupo karibu yako ulipo, tamani sasa, nasema tamani sasa kuona, uone....
Kwenye Biblia, Yeremia anaulizwa na Mungu, UNAONA NINI? mara aseme nimeona hiki mara nimeona kile, na alipoona Mungu akamwambia UMEONA VYEMA. (Yeremia 1:11-12). Kule kuona kuna matokeo yake, na hata Bwana akasema ninaliangalia neno langu ili nilitimize, ni kwa namna utavyoona.
Kuna kuangalia na kuona. Na ni baada ya kuangalia huja kuona. For you can't have step by looking until you see.
Sasa, its only what you see that which you can get, than what you are looking at. The mind is not settled in looking but in seeing, yaani; ni kile tu utachokiona ndicho utaweza pata, kuliko unachoangalia hapo hata akili inakuwa haijakupata na ufahamu hauwezi kukupa chochote cha kutamkwa yaani wazo ili kiumbike kwako. Kwani ni kweli unaweza ukaangalia na usione na akilini usipate kitu, lakini ulichokiona, ulishakiangalia na mind said something on that, na hakika utakipata. Unapoona ufahamu unawajibika, unapoangalia ufahamu haujui kitu bado.
Unaona pia pamoja na kumsikia Bwana, kule kuweza kuona ile ishara ya kijiti kilichowaka moto bila kuteketea, kulimpa mungu Musa aliyekuwa zaidi ya nabii uhakika na hatua, na ndipo aliweza kuwa na ujasiri wa kumuelezea Mungu kwa taifa la Israeli kule Misri pasipo hofu na hatimaye kumshinda Farao na jeshi lake lote (Kutoka 3: 2-4).
Mwamuzi Gedioni pamoja na kuonekaniwa na malaika wa Bwana na ishara ya sadaka kulambwa na moto wa mbinguni. Lakini ili awe na hakika wa kulikabiri lile jeshi kubwa la wamidiani na waamaleki waliokuwa kama mchanga wa bahari, alitaka aone ishara zaidi (Waamuzi 6:36-40), zimupe uhakika, nguvu na ujasiri, pamoja na kwamba kusikia neno la ushindi kuliipa nguvu mkono yako kwa vita, alihitaji kuona ishara zaidi za Mungu.
Unaona pia, ujasiri wa Gehazi haukutokana na kumwamini nabii Elisha sababu alikuwa bado na shaka pale jeshi kubwa la washami la mfalme Ben-hadadi lilipowazingira Israeli yote, wala haukutokana na miujiza ama ishara nyingi za Mungu zilizofanyika kupitia mkono wa bwana wake Elisha, la hasha! bali saa zile tu alipoweza kuona jeshi la malaika wa mbinguni ndipo aliposadiki sawa sawa (2 Wafalme 6:8-23).
Hivyo nawe utachokiona sasa kikufanye kuwa jasiri zaidi na uhakika zaidi, ili hatua kuu ukaiishi, nawe ukawe mshindi, nayo ahadi ya Mungu ikafanyike halisi kwako. Nguvu ya kuona iongezeke ndani yako uyaishi hayo maono, na sio kile wanachokuambia watu kuwa ndicho bali kile utachokiona kiishi hicho, amini katika hicho mpaka kitimie.
Kunacases mbili kwenye Biblia, zinazoonyesha namna takwa la kuona linaweza timizika, and that is our prayer point now.
-> Isaya 6:1-3 anasema katika mwaka ule aliokufa Mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi,....
-> Alipotengana na Lutu tu, MUNGU akamwambia Abramu inua macho tazama/ANGALIA pande zote, nchi hii ULIYOIONA nitakupa wewe na uzao wako hata milele. Ondoka ukatembee katika nchi hii kwa marefu yake na mapana yake, maana nitakupa wewe nchi hii (Mwanzo 13:14-17).
Hitimisho:
Ahadi ni kweli ya kwamba, KWA NAMNA UTAVYOWEZA KUONA, that's means you need to strive to see crystal clear, anasema NITAKUPA WEWE NA UZAO WAKO, kuna sharti ndani ya neno so, ni lazima uyatende mapenzi ya Mungu, akipendezwa nawe hakuna kitakachozuia kukipata alichoahidi. Amina.
Sunday, December 29, 2024
Sunday, December 1, 2024
#YOUR DRESS CODE, YOUR VALUE!
When the legion was confronted, dressing code changed (Luke 8:34-35, Mark 5:1-16).
Upya, kufanikiwa rohoni kama mwilini hata kwa ishara ya vazi unalojivika pia (3 Yohana 1:2)
Ni zaidi ya kumsitiri mtu mfano Adam na Hawa, Edeni walivyositiriwa, ona pia hata kichaa akivikwa suti huweza simama sehemu ya heshima, so, jua tu mavazi yanafaida nyingi zaidi ya udhanivyo...
Changing dressing code, is the sign that you entered new season, a sign of blessing, it's a value it shows. Even Joseph was differentiated from his brothers just by being given coat of many colours, as a sign of brightright blessings of firstborn son (Genesis 37:3). A sign of new you is given also by token of new dress code (Zechariah 3:3-5). That is a sign of new beginning, a restart on you, remember prodigal son parable (Luke 15:22-24).
This is indeed that, a new dress code shows your glory in the season, utajiona pia kama umevikwa na nguvu na uweza mpya kama vazi kiroho pia just by new dress code, it shows respect and honor in you in the way you deserve, utatofautishwa, utaangaliwa na kuangaziwa kwa upya, kutakuwa na too much expectations of those seeing you anew (Mathayo 3:4, Romans 8:19) and hatred (Genesis 37:4). Look even in the mount of transfiguration - Mt. Tabor (Luke 9:29), what was observed onto Jesus; His clothes changed in front of those seeing Him, they saw Jesus different that day, He was uplifted higher in levels more than they used to see Him before, in their own sight He was changed just by sign shown there that of changed clothes.
Unaweza jiuliza kama mwana wa Mungu. Je' kuna umuhimu?
*Bwana_ pindo za vazi lake laijaza hekalu (Isaya 6:1), vazi linathihirisha ukuu wa mtu, lamtukuza mtu, laonyesha nafasi ya mamlaka ya mtu, jukumu la mtu.
*Malaika na mavazi (Ufunuo 15:6)
*Vazi la sifa (Isaya 61:3)
*(Yohana 19:23); Yesu vazi lake na thamani yake.
*Vazi la Haruni (Kutoka 31:1-10; Kutoka 39:1-31)
*Ona mfano wa maharusu, they choose the best they can because it has the sign of new beginning, it marks their significant occasion of their life. It shows new them.
Dressing code inakutofautisha sana. The way you appear matters a lot in real life, hivyo kila wakati ni vizuri ujiulize nitoke vipi? That count a lot! just for that kuna milango mingi itafunguka kwako; kama ambavyo ushetani unavutwa na machafu, pia u! nuru unavutwa na masafi na mema na thamani (fikiria thamani ya hekalu jangwani kipindi cha Musa).
*Dress code inavuta kibali cha wanadamu hata na holy ghost pia, ule utukufu among other things ni kwa ile value presented kimavazi pia.
*Vazi jipya lasababisha attention ya watu, they can suddenly stop for a second thinking about you just by a look, hata kuja kukusalimia, na kuongea na wewe.
*Vazi pia linabeba presentation ya mtu kimvuto; binti wa herodia, na mfalme herodi kuahidi kumpa hata nusu ya ufalme wake (Marko 6:22-23).
*Esta kuweza kuingia mbele za mfalme kinyume na taratibu na kupata kibali chake hata kuahidiwa nusu ya ufalme (Esta 4:16 - 5:3).
*Imagine, hata yule mwana punda aliyetakiwa kupandwa na Yesu kabla ya kutumika walimuandaa kwanza kumsafisha na kumpamba pia (Mathayo 21:7).
*Tumia dress code zako vyema kwa kupata kibali cha kupita malango ya fursa za kimafanikio na kujenga heshima yako na kuilinda.
_Yeah sure! You will be well understood by the clothes you wear, don't ignore as if it is nothing, mind how you present yourself to the world, kama ulivyotakaswa na kutengwa ndivyo ulivyotofautishwa kivyote inside out, be that way live that way and know indeed! your clothing line, that dress code you wear depicts your value, repect, honor and your glory, Hallelujah! Amen.
Monday, October 28, 2024
#KINGDOM WAY (TEMPLE, U)
Tuesday, October 15, 2024
#UFALME WAKE, UFALME WETU
Luka 12:29-32 inashangaza sana, Yesu anasema; "Msiogope! enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vyema kuwapa nyie huo Ufalme". He said; "It's your Father's good pleasure to give you the Kingdom." Hata Daniel 7:27 alitabiri kwa habari ya wana wa Mungu akisema; "Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii".
Tena katika Yohana 17:22 Yesu anasema; "Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo na umoja". ona He said; "that glory which you gave me, i have given them", this is powerful!
Sikia hii; aliteswa tupate haki ya kuwa na kuitwa wana wa Mungu.
Iliyoitwa kufuru kuwa mwana wa Mungu ikawa haki yetu.
Kwa uthubutu wake, akagharamia hata mauti yake, alitamka hivyo ikawa.
Na haki hiyo ilikuja na uweza uliotupa sisi ujasiri na nguvu katika ukiri wetu kuwa sisi ni wana wa Mungu hakika.
Ilimchukua yeye kuishi kama sisi ili tuupate ufalme wake (Wafilipi 2:6-8); yeye mwenye namna ya Mungu toka mwanzo alichukua namna ya mtumwa akawa na mfano wa wanadamu halafu alijinyenyekeza sana akawa mtii mpaka mauti, naam, mauti ya msalaba (kwani ilikuwa laana mtu kuangikwa msalabani-Wagalatia 3:13-14), Yesu anasema jina lako Baba litukuzwe duniani (Yohana 12:28, 17:4,6), kwamba kuitwa kwetu sisi wana wa Mungu ni utukufu kwa Mungu Baba.
Fikiria jina lake la heshima Yesu; imeandikwa ktk Wafilipi 2:9-11 kwa jina hilo kila goti lipigwe la vitu vyote vya mbinguni, duniani na kuzimu.
Halafu, alizaliwa nalo kikawaida kabisa, kipindi kingine alikimbizwa nalo kwenda kufichwa Misri, aliishi nalo mitaani, wakati mwingine hata hakujilipizia nalo pale watoto wenzake walipomuonea, kuna kipindi akiwa mdogo aliwachallenge nalo walimu wa sheria Yerusalemu hawakumtambua vizuri alivyo mwana wa ahadi na hatima, alicheza nalo na hakuna aliyejua, saa ilipofika akajifunua kwalo hakuna aliyemsadiki, alikataliwa nalo, akatukanwa nalo, akatengwa nalo, balaza kuu la makuhani (Sanhedrin) likamuhukumu nalo (Isaya 53), ngoja nikuambie hivi, daraja la ukuhani liliikumbatia laana ya torati, lile lililokuwa njia kumfikia Mungu kama ilivyokuwa kanuni yake Mungu likageuka kifungo, kizuizi kwa watu kumfikia, sababu Mungu alipitisha hilo alipoitoa torati kwa mkono wa Musa akamfanya Haruni kama kuhani wa kwanza kuwakilisha watu wake wanisraeli patakatifu pa patakatifu na sasa Yesu aliwaita makuhani wale walimu wa sheria; mafalsayo na masadukayo kuwa ni kama majeneza yaliyopaka chokaa nyeupe nje huku ndani imejaa mifupa mitupu kwa vile walivyowabebesha watu mzigo mzito wasiyothubutu kuibeba wao, wakiwazuia watu kuingia patakatifu pa patakatifu na huku nao wamepoteza haki ya kupafikia. Hivyo kuhani mkuu Caiaphas hata alipomnyoshea kidole cha hukumu Yesu kumuapisha kwa jina la Bwana, Mungu anayeishi alilokuwa nalo yeye pasipo wao kulijua, kama ni kweli yeye ni mkombozi na mwana wa Mungu, kwa jina hilo akajibu; Ndiyo!, na kukiri kuwa karibu anaenda kwa Baba na karibu mwana wa Mungu atavikwa nguvu na kutawala tena wenyeji wote wa mbinguni, Kuhani mkuu kwa hasira kuu akararua vazi lake na kusema ni kufuru kubwa hii wala haihitajiki ushuhuda mwingine juu ya hukumu yake na hivyo wakamtesa sana nalo, na hata Pilato aliposema sina hatia juu ya damu ya mtu huyu, naona mmekusudia afe nami sijaona kosa juu yake, lile kundi (mob) likiongozwa na kuhani mkuu na makuhani wa Sanhedrin na masadukayo na wamafalsayo wakapiga kelele asulubiwe, na kisha wakasema na damu yake iwe juu yetu sisi na vizazi (watoto) vyetu, akasulubiwa nalo, akafa nalo msalabani na kuzikwa nalo. Haki yetu ya uwana wa Mungu ilipatikana pale golgotha kwa kumwagika damu yake Yesu ktk mauti ya msalaba, na kwa hiyo alituweka huru na dhambi, na hata pazia la hekaluni lilipasuka vipande viwili ili kwa ile haki ya uwana kwa kila anayemwamini aweze ingia patakatifu pa patakatifu binafsi azungumze na Mungu kama ilivyokuwa mpango wake wa awali toka enzi za Adamu.
Unaona kwa hiyo yaliyofanyika yote hayo, kwa ajili yako wewe na mimi, kwani hakuwa tayari kuona sisi tunanyanyaswa kwa kuwa gizani kuishi isivyotusitahili asili yetu, kwa hivyo siku ya tatu akafufuka nalo, halelujah! ili tu sisi tukamilishwe kwalo, tuitwe na tuishi kama wana wa Mungu, wana wa ufalme wa mbinguni duniani. Bwana Yesu Kristo asifiwe! ni habari njema sana hii..
Hivyo chukua nafasi hiyo sasa katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti, pokea huo ufalme wa Mungu, kaa hapo ee! mwana wa Mungu, angaza nuru yake, barikiwa, occupy till when He come again. Indeed; you are the son/daughter of God, and when you are the son/daughter of God in Him you are sin-free, amen.
Saturday, October 12, 2024
#THE TRUTH CO-ORDINATED LIFE
Truth co-ordination among brethren complete the mind of christ in us. Living the truth co-ordinated life perfect our righteousness in God.
~1 Corinthians 2:16🙏
Tuesday, October 8, 2024
#HABARI NJEMA KWAKO!
Make Holy Spirit count on you,
Jesus Christ proud,
The Almighty Father smile and,
All the Heavens rejoice.
It's New Dawn now.
Thanks God 🙏🏾.
*Kukuwa katika imani ni pamoja na kutochanganyikiwa ktk semi hizi mbili👇🏾 kwa maana Kiti cha Enzi ni kimoja na Mungu aketiye juu yake ni mmoja tu, Baba wa Mbinguni*
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mfanye Roho Mtakatifu awe nawe 🫵🏾,
Yesu Kristo aone fahari,
Baba mwenye enzi yote atabasamu,
nazo mbingu zikufurahie.
Ni mwanzo mpya,
Mshukuru Mungu.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mfanye Roho Mtakatifu katika jina la Yesu Kristo aone fahari kuwa nawe,
yaani, Baba mwenye enzi yote atabasamu katika utukufu wake,
nazo mbingu zikufurahie.
Ni mwanzo mpya,
Mshukuru Mungu.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Ok!, ni kama kusema kwa mfano mzee mmoja mbobezi katika tukio la mafanikio ya mwanae katika uhasibu wake baada ya kusikia na kuona matukio yake ya kipindi chote ktk video, huku akiwa na moyo wa furaha alipopewa mic aseme neno akashusha pumzi kubwa na kusema;
"Hakika kwa roho wewe ni roho yangu kweli kweli ni ndani yako mimi, kama mhasibu mi pia, najivunia sana wewe na kama Baba nimefurahi na kufarijika sana kwa mafanikio yako, na boma yetu yote wafurahi na kuwa na shangwe kuu kwa ajili yako, ni mwanzo wako mpya tena huu nishukuru sana mimi. Ni mimi Yoshua."
Ni Habari njema?,
Ndiyo! ni njema kweli hizi🙏🏾
Thursday, October 3, 2024
#HOLY GHOST [ROHO MTAKATIFU]
God's Way not mere talk, it's an empowered life; living by God's power.
Ndio!, Ufalme wa Mungu ni nguvu ktk matendo na sio maneno sana (power in action)~1Wakorintho4:20.
Matendo 19:1-20; Neno la Mungu la ufalme (kingly word of God) lilizidi kuenea Efeso na kushinda kwa nguvu, sababu ya nini? uthihirisho wa Roho Mtakatifu.
Sasa kama ni majivuno kwa mkristo yeyote, ni kwa sababu ya kumpata Roho Mtakatifu, ambayo ni neema kubwa sana. Waliomsikia Yohana mbatizaji Neno linasema waliamini neno la toba wakatubu na kubatizwa ikaishia hapo, ila ktk Yohana 1:12 kwa waamini wote wa Yesu kristo Mnazareti, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ule uwezo ndio nguvu iletwayo na Roho Mtakatifu.
Na je' sasa we ni mwamini wa Yohana Mbatizaji ama wa Yesu Kristo wa Nazareti? Jiulize!
Mwana wa Mungu kama kweli ndiye, son/daughter of God, omba uwe na Roho Mtakatifu, hapo inaleta maana ktk imani yako, na asiwe anaheri mpagani kukuzidi, naye huyo Roho akiwemo ndani yako atajithihirisha nawe utakiri kweli sasa ninaye.
Mfano mzuri ktk kizazi chetu mwanzoni mwa miaka ya 1900s, Mwafrika mweusi William J. Seymour, mtumishi wa Mungu huyu aliyekuwa kipofu jicho moja hakupendezewa na imani butu, alitamani matendo ya mitume yaendelee na aliamini kuwa kunena kwa lugha ni ishara mojawapo ya mtu kumpokea Roho Mtakatifu (Holy Spirit Baptism), akawa na shauku sana kila akisoma Matendo 2:4, shauku hiyo ikampelekea kuwa na mzigo kutaka kupokea na hata baada ya imani kujaa aliokuwa akiwahubiria wakaanza kupokea na kisha naye akajazwa Roho Mtakatifu miaka ya 1914, na ndio ulipozaliwa uamusho wa Roho mtakatifu kwenye mitaa ya Azusa ya Marekani, mpaka mitaani watu wakawa wanajazwa wanalewa Roho Mtakatifu na kuanza kunena kwa lugha mpya, na huo ukawa mwanzo mpya tena wa upentekoste kuenea kwa kasi baada ya kanisa kupoa kwa muda na huduma nyingi zikaanza utume duniani kama Assemblies of God iliyoenea duniani kwote, nawe unajua kama hapa Tanzania huwezi zungumzia mwanzo wa upentekoste bila kutaja Tanzania Assemblies of God (TAG), lakini jua ilianza na shauku ya mtu mmoja, hii ikithibitisha kuwa Mwana wa Mungu kweli akiwa na Roho Mtakatifu ni Kuhani wa Kifalme na Taifa teule🙏🏾.
so,
#Receive Holy Spirit
#Live like King, talk like Him
#Kingly virtues.
#Serve the Almighty God
Sunday, August 25, 2024
#U MWANA WA MUNGU
Somo la Yesu kwetu ni nini?
Uwana wa Mungu ni uwakilishi wa Mungu Baba aliyeketi ktk kiti cha enzi, kama yeye alivyo mbinguni ndivyo nasi tulivyo duniani (Wakolosai 2:9-10, Waebrania 1:1-10).
Na usiwe na shaka kuhusu hili kwani kuna haki hiyo (Yohana 1:12-13).
Sasa ktk Mathayo 16:13-20; pale kaisaria-filipi ndipo ilifika hatua na saa ile ya Yesu kufunuliwa kama mwana wa Mungu ambao huo ufunuo ndio mwamba wenyewe ambapo kanisa limejengwa kiroho na imani yetu ktk yeye inasimamia hapo.
Ule ufunuo kupitia Petro saa ile ( peter confession), ule uthihirisho na uthibitisho mkuu wa Yesu Kristo pale kaisaria-filipi alipokuwa amekaa na mitume chini ya miti ya miforsadi (mulberry), ndipo ulipo weka msingi na maana kuu ya huduma yake duniani.
Katika hatua zote za maisha ya Yesu duniani, wakati akisubiri kufunuliwa kwake mioyoni mwa watu ile saa iliyokusudiwa na Mungu baba, ukamilifu wake ulifikiwa kwa watu kumuelewa yeye aliye mwana wa adamu kama mwana wa Mungu, na ilimchukua muda kueleweka hivyo sababu ufahamu wa binadamu unachelewa kuchanganya (slow to wit) inapokuja kuhusu mambo ya rohoni, na hiyo ni kweli.
Yesu alipita stage ya utoto kama mwanadamu wa kawaida (conscious inakuwa dimly ktk kujitambua), then ya pili ya kujitambua, roho anaanza kujifunua ndani yake ktk ujana na mpaka ukubwa wake (pale conscious iko light-up, anakuwa aware mambo mengi ya divinity na mission yake), ya tatu ni ubatizo, kujithihirisha kwa Mungu kwake kama mwanae na kuanza huduma kama mwalimu wa ufalme wa Mungu, then mwalimu na mponyaji, hapa watu wa karibu walimjua kama mwana wa adamu na wengine wakamuita mesia, wengine wakataka hata awe mfalme wa wayahudi, na stage ya 4 na ya mwisho ilianzia pale kaisaria-filipi alipofunuliwa kama mwana wa Mungu na mpaka kusulubiwa kwake na kifo cha msalaba, na ktk stage zote hizo Yesu hakujikuza bali ulikuzwa kwa namna alivyokuwa anaishi, its stages kama ukuaji wa kipepeo kutoka buu, its marked the new start when was observed change supernaturally organically.
Can you be the son of God? Unaweza kuwa mwana wa Mungu?
Yes! nasema unaweza kuwa mwana wa Mungu leo, kupitia kumwamini kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yako.
Haya basi, nawe mwana wa Mungu mwenye haki kwa roho wake mtakatifu kupitia ile imani ktk kristo Yesu (Wagalatia 3:26), ktk kujitambua kwako hivyo pokea funguo za mamlaka kuyatenda yaliyo makuu duniani kama mbinguni, na huku sifa kuu ya umwana ya kuyatenda yaliyo mapenzi ya Mungu Baba, hata yawe magumu vipi iwe ni jadi yako, naye Mungu Baba akuwezeshe pale uyatendapo hayo mapenzi yake (Yohana 5:19; Luka 22:42-43) 🙏🏾.
Sunday, July 14, 2024
#PRAYER SECRET (SIRI YA SALA)
Sala/prayer imetokana na neno la kigiriki "proseuche" ikimaanisha- a wish, desire, request, or vow. Hi ni kutokana mtu anamahitaji yake au shauku maishani mwake.
Sala ni package; kuna kukiri, shukurani, kusifu Mungu, kumtukuza na kumwabudu Mungu, kuomba msaada. Yaani ni zaidi ya dua.
Sala ni mawasiliano na Mungu ktk nafasi yako ya kimamlaka uliyopewa duniani.
“The ultimate object of prayer,” says The International Standard Bible Encyclopedia, “is not merely the good of the petitioner but the honor of God’s name.”
“Lengo kuu la sala,” yasema The International Standard Bible Encyclopedia, “si kutimiza faida ya mwombi tu bali heshima ya jina la Mungu."
Bill Graham ashawahi sema; "Prayer is not just asking, it is listening for God orders". ikiwa na maana Sala sio tu kuomba omba (kuna zaidi ya hilo), kuna kusikiliza matakwa ya Mungu pia.
Na kuomba sio tu kupiga kelele; kuna kuzungumza na Mungu kwa hoja zenye mashiko (Isaya 41:21), mfano wa Mfalme Hezekia (2 Wafalme 20:1-11), pia kuna kusali kwa siri (Mathayo 6:6).
Kuna mifano ya aina nyingi ya sala ktk biblia, umewahi kuwaza Cornelio alikuwa akisalije? (Matendo 10:2-4), ama kwanini Yesu alitolea mfano wa Sala za mtozaushuru na falsayo (Luka 18:10-14)?
Yamkini hatupati sawasawa na tunavyosali sababu pengine ni kule kusali vibaya kama mtu usiyejielewa (Yakobo 4:2-3), kwani sala ni mawasiliano na mbingu juu, kuna itifaki na taratibu kumfikia Mungu kwa unavyotaka kutendewa.
Na ni sharti umuendee Mungu ukijua ni mkuu kuliko matatizo yako, imani ya matarajio yapaswa iwe kubwa. Na pia toa na sadaka madhabahuni unaposali kama Cornelio, madhabahu inajengwa na sadaka zako, na hakuna madhabahu ikiwa hakuna sadaka, kwa maana hiyo madhabahu inaweza kuanzishwa sehemu yeyote ikiwa tu sadaka imehusika, kama Yakobo ili iwe madhabahu alipoota malaika wakipanda na kushuka alisali pale na kuweka ahadi ya kumtolea sadaka Mungu pale. Kumbuka Mungu aliona, anaona na yajayo ayaona na kujua yote. Hivyo ni kwa sadaka madhabahuni, Mungu anaona moyo wako na heshima unayompa, na Marko 11:17; anasema mahali pa madhababu ya Bwana ni nyumba ya sala, napo haikumaanisha ni kuomba tu, hapana, kuna zaidi ya hayo kama kuimarisha mahusiano na Mungu.
Kwa mkristo sala na maombi ni silaha pekee, ya kumthibitisha yeye ni nani ktk mbingu ya Mungu na mamlaka gani yuko nayo kuitiisha dunia na kuamuru mambo yatokee kwa matakwa yake kama Bwana mwenyewe amupavyo kutenda🙏🏾.
Saturday, June 29, 2024
#PAY ATTENTION/ KUWA MAKINI
Sikio lina shepu kama vile tumbo la uzazi, ikiashiria chochote utachosikia kizuri ama kibaya, kitakuwazisha kama kusema kukutungisha mimba, na kupelekea kuzalisha kitu au jambo kama mimba/wazo lake kwa wakati na ule muda muafaka.
Hivyo kazi ya sikio ni kupelekea kuzalisha matokeo ya kile unachokisikia na kukisikia tena na tena, hakuna makosa hapo ni kutokeza matokeo. Na ndio maana hata biblia inasisitiza kuzalishwa imani kupitia kusikia neno la Mungu (Warumi 10:17). Na sasa kama imani huja kwa kusikia, nashangaa ni yepi mengine huja kwa kusikia? je' ni vipi kama hata unavyojisikia leo, vile unavyofeel vimepitia mlango huo huo wa sikio?
Na ndio maana tunasema PAY ATTENTION yaani KUWA MAKINI, sababu hata wakati wa Covid19, ni taarifa tulizosikia mara kwa mara ndizo zilitushitusha na kutupelekea kuwa na hofu kuu hata kuogopana na wengine kujificha. Hivyo hata ATTENTION ni kama currency ktk kizazi chetu, yaani ona ukisema pay attention, ni ya thamani, ni kama vile lipia pesa, attention ndio pesa yenyewe, sio rahisi ni gharama ni sacrifice, na hivyo ukipay attention utakipata na usipopay attention hutakipata, na pia attention ikipatikana inatransact na kunakuwa na exchange sababu inaweza onekana na kuhesabika, watu wanatransact agenda zao kupitia hiyo, mipango, kurubuni watu, kufunga na kufungua watu kifikra, kunadi vitu, Mungu na biashara na hata kuwaibia, na ni namna nyingi zinatumika kuipata attention kwa watu kwa mifumo yote ya mawasiliano. Na hii ni kweli kabisa nimeona ushawishi wa madalali, wapiga debe, watumishi wa Mungu feki na wa kweli, watu wa biashara ya mtandao, wa kwenye upatu, zama za babu wa roliondo, waganga, wanasiasa ile nguvu inayotumika kupata attention za watu ni kubwa naweza sema ni uwekezaji ni mtaji sababu ya tumaini la faida inayotokana na attention hizo.
Na ndio maana social dilemma documentary inasema "kama hulipii product, basi wewe ndio product, sisi ni products sokoni, ule umakini wetu ndio product yenyewe inayouzwa kwa advertisers. Mitandao ya kijamii sio nyenzo/chombo; ni dawa tena ya kulevya." Attention za watu ndio dhahabu ya social media.
Yesu alisema kuwa mwangalifu/makini na unachokisikia (Marko 4:24). Kwa maana matamanio yetu hayatuamulii hatima zetu bali vile tulavyo. Yaani hiyo ni vya rohoni na mwilini; iwe kwa masikio, macho, ndimi, ngozi, pua. Unajua unaweza kuwa na shauku ya kupunguza mwili na kuwa na afya njema, na hakuna kitakacho kusaidia kama unakula kula hovyo, ndivyo ilivyo na mambo ya rohoni pia. Hivyo chunguza na kuwa mwangalifu na unacholisha roho yako, unakuta vitu vya dunia vinakutawala, miziki ya kidunia inakushika, kuangalia picha za ngono, kuangalia filamu za kutisha na hata huogopi tena, kupenda sana zana za upako unazouziwa, hivyo angalia sana shauku ya nafsi kutamani vya dunia sana isikufunge usijekengeuka na ukajipoteza. So, be selective sio kila kitu cha kupay attention, usije corrupt nafsi yako, vingine ni kuvipuuzia ili kulinda nafsi yako.
Ona kwenye miji mikubwa; chokoraa/homeless wanapenda kuokota chakula kwenye matakataka ya nyumba za watu wengine. Kwa hiyo kama unataka kugeuzwa na kukuwa kifikra we uliyeamini, acha kuwa chokoraa kiroho, ungana kanisa karibu nawe ukuwe. Kula na tafakari (feed&chew) neno la Mungu na sio ya kidunia yaani toxic worldly content. Wafuate watumishi wa Mungu, walimu watakaokufunza kweli ya Mungu na kukuvuta katika utakatifu. Kumbuka njiwa hula vya kijani na kunguru penye miozo; cheki rangi ya muonekano wao, kuwa njiwa na sio kunguru.
Mwisho soma waraka wa Paulo kwa wafilipi 4:8, ubarikiwe na Bwana, amina.🙏🏾
Friday, July 15, 2022
#Limit Scope of work
Always learn to limit scope of work to get maximum impact. Imagine human Jesus who as Christ was God apart from Him having super power above all, on His three years of ministry on earth at His tender age, He limited His scope of work to focus only with lost sheep of house of israel at His time on earth as commissioned by God the father even ordering His 12 disciples to focus first on that area' Israelites as nation - house of israel (Matthew 10). This He insisted even to the case of woman of cannan in Matthew 15: 21-30 about His mission on lost sheep of the house of israel. And for Him passing through the area where is not in His mission was by the way as because to reach Galilee from Judaea it was must to go through Samaria but He limited His scope as per His mission on earth on the house of Israel alone (John 4:4). Luck enough the limits like boundaries of house of Israel was well known even to Samaritans, see John 4:7-9 the conversations between Samaritan woman and Jesus... and as per His stand it means even His disciples well knew that standard of Him, in the way that asking water to drink from samaritan He did that when disciples were not around.
I pray that, maximum impact be attained at that small beginning of yours without losing focus in Jesus name, amen.
Tuesday, July 5, 2022
#God of Many and different Languages
#LET YOUR SPIRIT RISE
Always let your spirit go higher, be quickened and became life-giving like Jesus Christ.
Psalm 71:20; Thou, which hast shewed me great and sore troubles, shalt quicken me again, and shalt bring me up again from the depths of the earth.
Romans 8:11; But if the Spirit of him that raised up Jesus from the dead dwell in you, he that raised up Christ from the dead shall also quicken your mortal bodies by his Spirit that dwelleth in you.
John 6:63; It is the spirit that quickeneth; the flesh profiteth nothing: the words that I speak unto you, they are spirit, and they are life.
1 Corinthians 15:45; And so it is written, The first man Adam was made a living soul; the last Adam was made a quickening spirit.
Once your spirit is at higher declare great stuffs; as man's original function is (Genesis 1:28); to rule over all creatures, fill the earth and subdue it (tawala, jaza dunia na kutiisha vyote).
Saturday, June 25, 2022
#KUMBUKUMBU NA NGUVU ILIYOFICHWA KWENYE MWANZO NA ASILI YA JAMBO
Kumbukumbu au memory (that faculty by which mind stores and remembers information) kwa mwanadamu yeyote ndio thamani yake, kama sio tazama kichaa, tahira au yeyote ambayo kifaa cha kumbukumbu (ubongo) kina dosari ama hitilafu fulani; thamani na umuhimu wake hupunguka ama kutoweka kabisa. Kuna nguvu katika kuwa nayo hata asili ya yote ni katika kukumbuka ndivyo uhuishavyo nguvu ya nafasi yako kiuungu na kimwili, na yeyote asahauyo hana umiliki wa chochote. Mungu ni wa kumbukumbu (Kumbukumbu 15:15), huwakumbusha wanadamu na kuwataka kukumbuka, na pamoja na mikasa yote tangia mwanzo na yote yaliyojiri duniani, Mungu alitunza maneno na matendo yake kupitia watu wake aliowachagua na shuhuda zao kumhusu yeye kwa njia ya maandiko kwa kumbukumbu za umilele na yote yadumu mpaka leo...na Musa alijua bila kumbukumbu hakuna hifadhi ya asili ya kitu chochote ndio maana katika torati kuna kitabu alikidedicate kama kumbukumbu la torati. Najua ktk uandishi wake wa torati kuna kumbukumbu ya maandiko ya kale alikuwa nayo wakati Mungu anasema juu ya yapi ayaingize kwenye uandishi wa torati. Na kwake ilikuwa rahisi sababu katika ukoo wa lawi ndio ukuhani wa israeli ulidumu na hivyo walikuwa na historia yote ya mwanzo wao na mwanzo wa yote yaliyofunuliwa katika vizazi vyao toka asili ilivyokuwa na ikiwa rahisi kwao kujua Mungu huyu ni wa namna gani na ana abudiwaje. Hivyo uhodari wa taifa la israeli na nguvu yake i pia katika utunzaji wa historia na kumbukumbu zake, kama ilivyonguvu na uhodari wa malkia wa uingereza iliyokatika siri ya asili ya ufalme wake aijuaye yeye pekee mkaliaji wa kiti cha ufalme nayo i katika kumbukumbu za ufalme na pasipo yeye ufalme utayumbishwa hadi amrithishapo ufalme mmoja wa uzao wake na kumuasa kupitia kumbukumbu za kiti kile cha ufalme tangia mwanzo apate ufahamu, nguvu na hekima kuu ya utawala (na punde litajiri hili), ama kama ilivyonguvu na uhodari wa roman catholic ni vyote vyenye asili iliyodumu muda mrefu na kumbukumbu zake si rahisi kuviangusha na kuvishinda nguvu, vyenye asili ya muda mrefu vyahitaji muda mrefu kuvibatilisha kushinda nguvu zake kwanini kwa sababu kabla ya kushinda inabidi sio tu kujua asili yao bali kuifuta kwenye kumbukumbu zao na mioyoni mwao ili wasiweze tena kuwa hodari na nguvu kuu na kisha kuwashinda, mfano kwa RC likumbuke hili wenye uwezo wa kuibadilisha syllabus yake ni walioweza kuaccess asili yake walio katika level ya upapa na wafuasi watabaki kuwa wafuasi wa RC. Unajua pia hata mukuyu mkubwa miaka mia saba, mia nane nguvu yake ya miaka mingi ikatika mizizi yake roots ambazo zinahistoria kubwa ya kwamba iliwezekanaje ilishindaje na pia utaona mizizi yake ambaye ni uhai wake kuwa imara sana imeenda mbali sana na ni deep sana kwenye source of life' water na ndio juu huoni mukuyu ukitikisika kwa dhoruba yoyote sababu haujauacha uhai wake asili yake kabisa' water kule deep down ina mahusiano yadumuyo, na kwenye mizizi pekee ndio katisho la uhai wake lilipo, kwa hivyo aliyeijua mizizi yake na kuaccess deep down asili yake ana uwezo wa kukatisha uhai wake mkuyu mkubwa na fahari yake na hata kuibatilisha kwa maana ana siri kuu ya nguvu yake. Twajua nguvu ya kristo na umilele wake usioweza kufananishwa na yeyote, kutokana pia na kuweza kuestablish kudadavua asili yake kupitia kumbukumbu kuanzia adamu mpaka yeye na kisha kuithibitisha ile Yesu ni Bwana ni baada ya kuunganisha na kujua kumbe Bwana wa kutoka mwanzo ndio Yesu mwenyewe, no wonder mtume wa Yesu kristo (Mathayo 1) aliweza kuandika asili ya Yesu kutoka Adamu mpaka kufikia Yesu kupitia kumbukumbu. Siri ikiwa siri kuu kwa mwenye nayo hakuna aiwezaye nguvu yake itakuwemo mpaka pale ujulikanavyo ndipo nguvu yake ni rahisi kuififisha na kuishinda, na ndio maana Mungu hatumujui jumla ni kwa sehemu tu na hiyo ni kwa sababu anataka tuwe kama yeye japo kwa sehemu hiyo anayojifunua kwetu. Huwezi kuiteka nyara nyumba pasipo kumfunga kwanza mwenye nguvu ndani yake, na ili kumfunga lazima ujue kwanza siri zake na asili yake na hivi kama kumbukumbu hazipo na huna uwezo wa kuziaccess basi humuwezi kabisa. Na yeyote awezaye kuzipata kumbukumbu za asili yake na kuzielewa pamoja ikibidi kuzishinda huweza kufikia hatua ya kuwa na nguvu hizo kuzifuata ama kuziovertake na kuanzisha kitu kipya kipinzani juu yake. Wakati afrika inatakiwa kutawaliwa kuifanya nyara yao wakoloni walitumia njia nyingi na zote zilikuwa na maana kama ya mamisionari kabla ya kujiaminisha kuja kupambana ili kuwateka waafrika. Explorers na Wamisionari pamoja mengine walitaka kujua kwanza asili yetu ambayo ni nguvu yetu na walitumia kila falsafa ili kujua hilo walivyojua kwa sababu pamoja na kumbukumbu lakini yalikuwa mioyoni mwao na kila kabila lilihakikishwa kwenye kila kizazi kuna mtunza kumbukumbu atakaye zihamisha kwenda kizazi kingine kipya cha damu yao (kabila) na kuhakikisha yote ya kale yanaeleweka na yanatunza mioyoni mwao kwa maana ndio nguvu yao. Kuna msemo unasema mali bila daftari hupotea bila sababu, hivyo basi kabila bila kumbukumbu hufutika na kisha kupoteza asili na kuanzishwa kitu kipya, sasa kupotea kwake hakuondoi gharama ya kupotea huko, waliopotelewa na kumbukumbu ya asili lazima wagharamike sababu mwenye asili yupo naye atakuwa na kisasi na kila abezaye na kudharau kwa kusahau kabisa uwepo wake iwe kwa kusababishwa na wengine ama wenyewe. Hivyo basi hao wamisionari wakatumia nguvu kubwa baada ya kujua kuhakikisha wanazifuta kumbukumbu zetu pamoja na vile vilivyoashilia miungu yao kuviteka na kuviondoa kwao na kisha kuifuta mioyoni mwao na akilini kwa kuwapa elimu na utashi wa kibiblia wawe wapya kwa yote na zidi unavyosimama katika utashi huu mpya unafuta ule wa kale na kumbukumbu zake. Akutakaye kuwa na nguvu juu yake atakupa kujua asili yake na kumbukumbu zake utajua siri yake na hivyo utakuwa na nguvu za kuishindaniya nafasi yake hata ikibidi kumshinda ukiweza. Siri za Mungu alizomfunulia shetani ndio zilizompa lukwale' uwendawazimu wa kuitaka nafasi yake na kumbukumbu za siri hizo ndipo ilimo nguvu ya ufalme wake. Adamu wa pili alihuishwa katika Yesu' na kwa kuwa adamu alifanywa muumbaji wa dunia hii na mungu wa dunia hii na mwenyezi Mungu, hivyo Yesu alikuja kututekea nyara ufalme wa adamu uliopotezwa naye na hivyo mwana wa adamu kuishi pasipo huo. Watawala wa dunia huact kama mawakala wa mungu wa dunia hii kabla ya Yesu kufunuliwa maishani mwako, na ndivyo alimpasa kufa, sababu alikuja kumfanya kila mtu mungu wa dunia hii, muumbaji mdogo na hata aliyeko chini sana aliyedharauliwa ili litimie yeye ni Mungu wa miungu yote ya jamii yake isiyokengeuka ya ufalme wake na wote tuiishi ahadi ya neno hilo, kwa kuwa shetani baada ya kumzidi adamu akili na kutawala dunia kama mungu sehemu yake adamu, mawakala wa utawala wake hawakumruhusu Yesu kuinuka kama Mungu (baada ya kutukuzwa) na mfalme juu yao wote hivyo wakamuua na hivyo kifo chake haikuwa tu kuhusu taifa la israeli bali mamlaka ya dunia yaani shetani aliyejitukuza duniani katika sehemu na nafasi ya adamu wa kwanza (mawakala wake walitenda kazi ile kujaribu kuzima ufalme; hila za namna hiyo zimewaangusha kina ghadafi, falme za irani kwa kudai washikadau ndio wamemuua mkuu wao kumbe ni fitina za mamlaka za dunia kuangusha fahari ya mamlaka iliyopo kuwafaidia wanadaiwa na kuwa walengwa walioiangusha). When war is of gods only gods know the really course and the source and not others, vita iwapo ya miungu ni miungu pekee ijuayo kisa mkasa na kwanini na siyo washikadau au wafaidia miungu hiyo, wao hao wanaweza kujua baadae kwa sehemu kwamba kwa nini kutokea kilichotokea?.
Yote haya nayasema kuhuishwa umuhimu wa kumbukumbu na nguvu ya chanzo ama asili. Mwanadamu yeyote hawezi kuvishinda vifungo vyote alivyofungiwa pasipo kujua hivyo vifungo na pengine kama kweli vipo na vimemfunga. Kujua chanzo kunampa mtu kuwa na mkakati wa kujitoa kwenye mkwamo wa muda mrefu na miaka mingi. Kujua chanzo ni kujua siri ya kwa nini upo hapo na je ni hapo ndio unapasa kuwepo ama umefungwa nazo kumbukumbu zitakufanya ujiassess vizuri kwa kuangalia historia na mwenendo wake ndipo utapata nguvu ya kupambania hatua mpya zaidi na kutoka kwenye mkwamo huo. Vifungo vipo sana tu kwa mwanadamu na ndio maana hata Yesu mwenyewe anasema njooni kwangu nira yangu ni raini na mzigo wangu ni mwepesi hata ajae kukusaidia sharti aweze kukufunga ili uambatane naye kiroho na kimwili na hivyo basi vifungo kwa mwanadamu ni lazima dunia ilishavamiwa na mvamizi shetani awafunga wenye nayo dunia sababu alishamfunga kwa kumzidi akili mungu wa dunia hii adamu, na hivyo miili yetu ni kama imesetiwa kuangukia kwenye vifungo hivyo vyenye dhambi ya asili, na hiyo yote ili mwanadamu asijitambue kuwa yeye ni mungu wa dunia hii na shetani anainjinia vifungo hivyo kupoteza ufahamu huo ili usikumbuke ama kujitambua nafasi yako ya asili mungu wa dunia hii kwani chanzo hicho kitakujuza wewe nguvu yako juu yake hivyo haliruhusu hilo akiwa amekaa kwenye nafasi yako ya umungu wa dunia hii japo itifaki ya mwenyezi Mungu hata shetani pamoja na kukalia nafasi hawezi kuitangua ya kwamba dunia itatawaliwa na mungu adamu na wana wake na yeyote atakaye kuitawala hata kwa hila ni sharti amutumie adamu na wana wake, no wonder' Mungu kuurejesha ufalme ilimpasa aje kama adamu wa pili sasa, naye shetani anatupofusha kwamba usimamapo nafasini mwako kwamba unajitukuza kwa kukukosesha na wanadamu wengine ili ubaki chini kama walivyo wengine na yeye abaki kuwa mungu pekee wa dunia pasipo haki sababu hana mwili wa kutawala kihalali kama mungu wa dunia ya adamu na wana wake.Ee' mwana wa adamu funguka adamu baba yako asili ya damu zote alifanywa mungu wa dunia hii, baada ya kukosea Mungu mwenyezi kupitia Yesu' yeye aliyefanyika adamu wa pili alikuja kuuhuisha ule ufalme ili wana wa adamu wabaki kuwa miungu ya dunia kwa kuwa aliona mateso na kukandamizwa kwetu na shetani na kwa kudhulumiwa haki yetu ya utawala wa dunia yetu wenyewe kama miungu, ifanye leo ahadi ya Mungu juu yako mwenyewe itimie kwake (Zaburi 82:5-7) ee! mungu wa dunia hii we sio wa kawaida kama unavyojichukulia mkubali Bwana leo hii akuokoa kisha akupe roho wake akujuze zaidi uyapasayo kutenda kama mungu wa dunia, hivi kama Mungu mwenyezi ameamua mwenyewe kujimultiply kwa wana wake (sons of God) waliowashindi katika yeye, wewe ni nani hata upinge? wewe ni nani hata ukatae? Nasema wewe ni nani hata useme hapana?, jambo hili litasimama hakika na kweli yake aliyoiinua kupita jina lake lote hiyo ahadi yake itatukuzwa milele yote. Asema ili mapenzi yake Mungu wa miungu yatimizwe duniani kama vile yatimizavyo mbinguni, mwana wa adamu wewe uliyezao la damu hakika katika asili yako ifanyikavyo uumbaji tumboni mwa mama, wewe ni mungu wa dunia hii na damu yako yashuhudia haya ya kwamba ni mungu wa dunia wewe! ule uhai wake ndani yako damuni. Jua hekima hii ya kidunia chai iliyopoa ili kuhuisha joto lake inakupasa kumimina chai ya moto ya jamii ile ya mwanzo kulinda hadhi na uhalisia wake, na uhai wa damu iliyopunguka hulindwa na kumiminiwa damu mpya nyingine ya asili ya mwanzo kuhuishwa kwa upya vya asili ya mwanzo huku ikiweza kubatilishwa vimelea vya magonjwa, udhaifu na upungufu wowote uliokuwemo kwanza. Hivyo basi kukurejesha nafasini mwako kama mungu wa dunia hii ilimugharimu Mungu kumimina damu mpya kuhuisha damu ya adamu wa kwanza iliyofitinisha uungu mmoja wa mwanadamu na Mungu baba wa mbinguni ili ufalme mmoja naye udumu duniani kama ilivyo mbinguni, ni mapenzi yake hayo hiyo yatimize kwa kukubali kumpokea ili nafasi yako kwa mwana wa adamu wa pili ihuishwe ndani yako kupitia yeye Yesu' adamu wa pili aliyeshinda yote na akamnyang'anya mamlaka yako shetani aliyokuibiwa wewe na kukupa wewe tena hivyo okoka ili uishi kama mungu wa dunia hii hiyo ndio mara mia yako itakayoipata katika dunia hii na kisha uzima wa milele yaani huo ufalme wa Mungu duniani kuwa kweli mfalme. Shetani anatembelea nyota yako, namna manual ya kuwa mtawala na mumiliki wa dunia hii kama mungu wa dunia hii anatembelea shetani yaani ile baraka ya uadamu japo ameweka na mapotofu mengi ili usiifikie' amua leo mfuate Yesu atakujiza tu, naye shetani kama alivyoandikiwa na kuamuliwa kama adhabu yake ya uasi atakusujudia wewe uliyemdogo na punde kufanyika mkuu kuliko malaika, sababu shetani aliyekuwa malaika mkuu akusujudia wewe aliyemwamini Yesu na kuokoka. Jitambua leo mungu hanaga hofu wala woga ni jasiri katika njia zake, ni mungu wewe jitambue sasa Baba yako aliyeko mbinguni amekutukuza katika dunia na fahari yote ya dunia uimiliki na uitawale wala siyo shetani.
Arise and takeover the earth, oh! man as a god of this earth of which you are his/her product. i.e. created from it to be above it and not other but only you. Wewe uliyesehemu ya dunia, mwana-damu, mwana-nchi, mwana-udongo, mwana-ardhi hii tawala, tiisha vyote kwa uungu wa Mungu ndani yake ungali na nguvu, hata pale mwili utapoexpire nao utaenziwa ardhini, heshima ya mwili ni udongo na udongo ni sehemu yako uweza wa uumbaji wa vya jamii ya udongo u mikononi mwako kwa kinywa chako umba vyote navyo havitaacha kudhihirika kwa ajili ya utukufu wa Mungu wa miungu. Nasema Amka' uinuke juu uangaze kama mungu wa dunia hii, selah!!!. Ukiamini utaiona baraka hii na kuiishi, kita mizizi duniani na uitawale kama dunia kama mtawala halali wa sehemu yako. Kuna waliyojitambua hata sasa ambapo mtu aiishi ahadi ya kuwa taifa teule na mzao wa kifalme na ni wana wa adamu wenzetu ambao wanakuwa na wengine wanaenda kuwa na status ya kufanyika kama taifa katika nyakati hizi za sasa hali ni mwana wa adamu kama wewe sizungumzii nyakati za yakobo kufanyika taifa la israeli yamkini kipindi kile wakati ulicheleweshwa sana ahadi kutimia lakini katika Kristo Yesu wakati umekombolewa sana ukiwa ndani yake ni punde tu mwana wa adamu mmoja kuwa taifa teule na kuiishi ahadi ya Mungu na dunia kumutambua kama taifa ndani ya dunia ni nyakati za mwisho hizi, ni nyakati za miungu ya jamii ya Mungu mwenyezi, Mungu baba kuitawala dunia tena na sio tena mizimu iliyoimtii shetani na kuwa mawakala wa utawala wake usio na haki yoyote, hivyo funguka na ujitambue wewe sio kuku ni tai, wewe sio panzi ni jitu tena ni jitu la kutisha falme zote za ulimwenguni anazotawala shetani pasipo haki ya utawala, kwani ujionavyo wewe mbele zao ndivyo walivyopaswa wao kujiona hivyo mbele zako wewe mungu wa dunia hii. kumbuka tu hii neno la Mungu lasimama milele na ahadi yake ni kweli na amina.
Thursday, April 7, 2022
#UHALISIA WA UHALISI ama UHALISI WA UHALISIA'
Kibinadamu iko hivi, kwa mfano; Level ONE: Mbariki_blesser; ni abarikiye wengine...sio ndio!!,
Level TWO: Mbarikiwa abarikiye _ blessed blesser; anakuwa ni anayebariki wengine naye huku akibarikiwa, yaani mrithi baraka (1 Petro 3:9).
Hivyo ni sawa na yafuatayo;
Level ONE: Mvurugaji _Confuser; anayevuruga wengine na vya wengine....
Level TWO: Mvurugaji mvurugwa_ confused confuser; anayevuruga wengine avurugwaye naye.
Level ONE: Mharibu_ destroyer; aharibuye...
Level TWO: Mharibu mharibiwa_ destroyed destroyer; aharibuye aharibiwaye.
Unaweza endelea na wewe kuyadadavua mengine, mfano; mchonganishi, mfitini, mtapeli, muongo, muangushaji (m-let down), muonevu, msahaulifu, mkwamishaji, mpuuzaji, mnyimaji, mtoaji, mdharauji, mpaji, mchukiaji, msaliti, mpendaji, mropokaji, mbinafsi, mkali, mkarimu, mtaratibu, mtengaji, mdhulumaji, mchochezi, mchonganishi, mchongezi, mlalamikaji, mlalamishi, mhukumu, mzinifu, mlaaniji-cursing person, etc.
Sasa ukifika level TWO wewe ni brand, unayobanner kabisa kwa eneo lako yaani wewe ni weapon. Katika yote mtu huhusika katika kuiendeleza au kuboresha hulka ama silika ama wengine huita haiba iliyoko na wengine huiunda hata ambayo haikuwepo kwanza kutokana na mazingira walioishi.
《《LUKE 6:38》》
Kila tabia na kikombe chake, usiwe kama yule wa Zaburi 109:17-19, usipende vya giza kuliko vya nuru venye utukufu ( Yohana 3:19, Zaburi 52:3), kuwa kama Yesu Kristo, mpenda mema mtenda mema.
///Psalm 34:14///
Hata hivyo karibu kwa NEEMA na REHEMA, anayamudu haya, mwenye hiyo atakubadilisha, ataihuisha roho yako kwa upya!!....
...kutana na GOD of Grace & Mercy!...
...kisha uwe kama Warumi 8:5.....
.png)

















