Wednesday, February 4, 2015

#USELESS IS USEFUL

Hakutakiwa MTU mashuhuri, msomi wa juu au wa heshima kuwaokoa waliotumwa kupeleleza Yeriko, Bali Rahab kahaba.

Na pia haikuhitaji MTU mkubwa sana kama raisi, au kuhani au jemadali kujenga mahali palipobomoka (kuta za yerusalem) ila Nehemia mnyweshaji wa mfalme,

Yote ktk yote ni Mungu ndiye afanikishaye mipango yetu yote kwa njia azijuazo mwenyewe kwa maana aonavyo sio kama sisi tuonavyo.

Mitazamo yetu iwe katika kumtazama yeye zaidi ya vile tujitazamavyo na kujitegemea, yeye aonaye mengi ndiye awezaye kufanya mengi kwetu kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu. Yesu ni wa Neema na Rehema na wa baraka pia.

No comments:

Post a Comment