Roho Mtakatifu (Swahili), Inumbula ja Nguluvi (Bena), Mumuyo Mwele (Chaga), Embeera z'obuntu bw'Omwoyo Omutukuvu (Luganda-Ungada), Umwuka wera (Rwanda), Mweya Mutsvene (Shona-Zimbabwe), Umoya Ongcwele (Zulu-S.Africa), Gbigbo Wiwe (Yoruba-Nigeria), Holy Spirit (English), Holy
Ghost (English), Ruach HaKo'desh (Hebrew), Allos Parakletos (Koine Greek), Paraclete(Greek), Spiritus Sanctus (Latin), Heiliger
Geist(German), esprit Saint(French), Spiorad Naomh(Irish), Svyatoy Dukh (Russian), Espíritu Santo(Spanish), vyovyote utakavyomuita kwa lugha yako.
Roho Mtakatifu ndiye aliye ndani ya Yesu Kristo yaani Mungu
Baba ndio huyo huyo mmoja hakuna watatu. Biblia (1 Yohana 5:7-9) inasema watatu
wanashuhudia mbinguni; Mungu Baba, Neno na Roho Mtakatifu nao ni mmoja (MUNGU)
na watatu duniani; Maji, Damu na Roho nao ni mmoja (Mwanadamu). Sasa kama
ambavyo mwanadamu hawezi kugawanyika na kuwa zaidi ya mmoja yaani kama Recknald
ni Baba, Mume na Mhasibu atakuwa ndiyo yuleyule Recknald mmoja daima, ndivyo
ilivyo MUNGU ni mmoja regardless His manifestations to human beings. Hivyo kama
basi ushuhuda wa mwanadamu unapokelewa kuwa ni kweli basi wa Mungu ni mkuu
zaidi, ushuhuda wa Mungu ndio huu amemshuhudia mwanawe, yaani mwana wa Roho
Mtakatifu, full stop. Amini leo kama bado.
Na hii ni hakika na kweli kwamba
Roho Mtakatifu ndiye Mwalimu wetu, Mfariji wetu, Msaidizi wetu, huyu Mungu
mmoja ndiye huyo huyo ndiye yeye kwetu na wa mfanano wetu wala si kitu, ama
njiwa ama wa ishara yeyote unayodhani wewe kumlinganisha au kumfananisha kwayo,
ni wa mfanano wetu wanadamu yaani Mungu.
Huyo ndio habari njema ya dunia
tangu kupaa kwa Yesu Kristo kwenda mbinguni na mbali, mbali zaidi ya mbingu,
hakuna habari mpya zaidi ya hiyo ya Mungu pamoja nasi daily (yaani Roho
Mtakatifu ndani yetu). Huyu yupo live duniani yupo nasi sasa hapa hapa duniani
ndani yetu anatusaidia katika udhaifu wetu hatujui kusali vyema anatuwezesha tutiwe
nguvu ya kushinda katika yote, kupitia yeye na kwa ajili yake ndani yetu
tunasali, tunaomba, tunabarikiwa na kushinda yote, tuna huo uweza kwake na
uwezo katika yote kwa maana ndiye yeye ayakamilishaye yote ndani yetu; yaani
Roho Mtakatifu ndiye Mungu baba, ndiye Mungu mwana hapo, wala huwezi kabisa
tofautisha watatu walio mmoja ndani yetu, ni ahadi na ilishatimia kwetu.
Hivyo tembea kifua mbele sio kwa
sababu ya nguvu za mwili wako, ama akili zako na utashi, ama uwezo wa kufanya
kitu, ama utajiri wako na mali, bali kwa kuwa makao makuu (HQ) ya Roho
Mtakatifu ni ndani ya wateule wake waliokombolewa kwa damu yake yaani Yesu
Kristo.
Kama umeamini katika hili na Yesu
Kristo kafanyika Bwana na mwokozi wa maisha yako, yote haya ni yako, kwa kuwa
ukombozi na uweza wa kukuunganisha katika neema hii una yeye Bwana, hivyo
nasema barikiwa na Roho Mtakatifu siku zote katika jina la Yesu Kristo, amina.
No comments:
Post a Comment