Saturday, October 2, 2021

#SON OF THE SOIL (☆☆☆MWANA - NCHI☆☆☆)

 ☆☆☆Ooh! Son of the soil.

☆☆☆Umwana uwudongo.

☆☆☆Mwana -wa-mavumbi.

☆☆☆Mwana-wa-nchi. 

☆☆☆Mwana-wa-adamu. 

☆☆☆Mwana-wa-ardhi, huh! ambayo leo tunaikanyaga hivi, kesho na kesho kutwa tutaunganayo kama waliotutangulia, nayo itatufunika milele na tutakuwa sehemu yake yaani udongo tu, tujihadhali sana tunavyoishi na tunayoyatenda. Mpende sana Mungu ishi matakwa yake ile ahadi iwe yako ya kwamba miili hii ikiexpire twawa hai zaidi ktk yeye Mungu.

Kama Biblia katika Mwanzo 3:19 inavyosema; twalitwaliwa katika ardhi/udongo na ardhini/mavumbini tutarejea. Mungu aliiamuru ardhi tuundwe/umbwe ktk hiyo kwa materials zake kwa mfanano wake Mungu. Natukapewa mamlaka ya kuiitiisha ardhi' na kuiamuru (Yeremia 22:29) na kuielekeza miili yetu yapasayo kutendeka. Yeye Bwana kama mpanzi (Mathayo 13:18-35) amepanda mbegu, neno lake ndani yetu tujitambue nafasi zetu na yaliyomapenzi ya Mungu tuyatende kwa majira yako kabla ya wakati wa kutokufaa kwetu, jukumu lako kujijua wewe ni udongo wa aina gani' je we ni ule udongo wa njiani/barabarani' ni wa mibani' ni wa miambani' ama we ndio udongo mzuri unaotakwa na Bwana Mungu basi tambua majira yako yakujiliayo sasa sababu anahaja nawe kwa ajili yake mwenyewe uyatimize mapenzi yake duniani kama ilivyo mbinguni. Na ni hakika kabisa kama alivyowahi kukiri Mtakatifu Augustino wa Hippo ya kwamba; "UMETUFANYA KWA AJILI YAKO MWENYEWE, EE! BWANA, NA MIOYO YETU HAITULII WALA HAITATULIA MPAKA ITAKAPOPATA PUMZIKO KTK WEWE". Kwa maana ktk yote tunalakujibia siku ya hukumu kwa pumzi ya uhai huu, kwa nguzu za mwili huu tusipo yatimiza mapenzi yake, hivyo sema na nafsi yako leo, ewe nafsi yangu, ewe udongo mhimidi Bwana sasa na milele. Waliotutangulia mbele ya haki aliyekutangulia mbele ya haki akupa wewe uhakika na onyo pia kwamba mapito yako yawe na Mungu, mwana udongo tusijejidau wala kujisahau sana kwa lolote iwe kwa mali, kwa vitu, kwa umaarufu, umashuhuri wala kwa uzuri heshimu kila mwana udongo mwenzio kwani njia yetu ni moja. Biblia katika Yeremia 17:7-8 inasema; "Amebarikiwa mtu yule/mwana udongo amtegemeaye Bwana, ambae Bwana ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi, wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, wala hautaacha kuzaa matunda". Barikiwa na Bwana, amina.

No comments:

Post a Comment