This is beyond doubt "Depend on JESUS of Nazareth; Man is a mere vapor"
*Surely men of low degree are vanity, and men of high degree are a lie: to be laid in the balance, they are altogether lighter than vanity [Psalm 62:9].
Also James 4:14 says that we are just a vapor that appears for a little while and then vanishes away; for we live blindly without knowing how our life will be like tomorrow.
Kwa hivyo nasema tena na hii ni uhakika kabisa “Mtegemee YESU wa Nazareti; Mwanadamu ni Ubatili” yaani mwanadamu ni kama mvuke uonekanao kwa kitambo na kisha hutoweka. Yatupasa sana kumtegemea Bwana Yesu, kumtumainia Yeye pekee ili tujifunze kwake yahusuyo Ufalme wa Mungu na hata Biblia katika Zaburi 125:1 inazungumzia kuwa wamtumainio na kumtegemea Bwana (Yesu wa Nazareti) ni kama mlima sayuni hautatikisika milele daima. Soma zaidi pia; Isaya 40:31, Zaburi 62:5-12, Zaburi 1:2-4, Yeremia 17:5-8, Mithali 4:23 na Kumb.28 kuhusu msisitizo wa kumtegemea Bwana Yesu na Baraka zitokanazo na utegemezi huo.
- Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu
6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
- Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea yeye Bwana Yesu wa Nazareti
7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, ambaye Bwana
ni tumaini lake.
8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, uenezao
mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake
litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha
kuzaa matunda.
Barikiwa na Bwana ewe kanisa la Mungu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti, Amina.
Soma pia Isaya 40:15 na mstari wa 17, utaona na kutambua kuwa Roho mtakatifu ndio kila kitu kwa mwanadamu.