Wednesday, June 18, 2014

#THE DECLARATION OF THE ONE DEPENDING ON JESUS OF NAZARETH (OUR LORD & SAVIOUR)

The human being created by Almighty God, the one who trust in Him and depend on our Lord Jesus Christ of Nazareth, always says and declare this 23rd PSALM as his/her recognition i.e. assurance and foundation that Almighty God is everything in his/her life;
The Lord is my shepherd – THAT’S RELATIONSHIP!
I shall not want – THAT’S SUPPLY!
He maketh me to lie down in green pastures – THAT’S REST!
He leadeth me beside the still waters – THAT’S REFRESHMENT!
He restoreth my soul – THAT’S HEALING!
He leadeth me in the path of righteousness – THAT’S GUIDANCE!
For His name sake – THAT’S PURPOSE!
Yes though I walk through the valley of the shadow of death – THAT’S TESTING!
I will fear no evil – THAT’S PROTECTION!
For thou art with me – THAT’S FAITHFULNESS!
Thy rod and Thy staff they comfort me – THAT’S DISCIPLINE!
Thou preparest a table before me in the presence of mine enemies – THAT’S HOPE!
Thou annointest my head with oil – THAT’S CONSECRATION!
My cup runneth over – THAT’S ABUNDANCE!
Surely goodness and mercy shall follow me all the days of my life – THAT’S BLESSING!
And I shall dwell in the house of the Lord – THAT’S SECURITY!
Forever – THAT’S ETERNITY!

That’s why the Bible in Psalm 125:1 says; “Those who are trusting in the LORD are like Mount Zion, which cannot be overthrown. They remain forever”.

#ISHI UKIMTAZAMA YESU WA NAZARETI (NI UJUMBE WA BWANA)

      Ishi ukimtazama Yesu wa Nazareti ina maana tumuishi Yeye, Biblia inasema katika Yohana 3:14-15 kama vile Musa alivyomuinua Nyoka wa shaba kule jangwani  wanawaisraeli kwa kumutazama huyo nyoka wa shaba wakaponya na mauti ya sumu za wale nyoka waliowang’ata huko jangwani, Vivyo hivyo Mwana wa Adam (Yesu wa Nazareti) alikwishainuliwa juu na ya kwamba mwanadamu yeyote aliye na mwili amutazamaye huponya na shida, dhiki, laana, mauti na mateso yote yamukumbayo mwanadamu na kupata uzima wa milele. Kwa hiyo kama vile katika tenzi za rohoni namba 118; inavyosisitiza kuwa ni Ujumbe wa Bwana kwamba “tuishi tukimtazama yeye” yaani yeye kuwa mfano kwetu vile tupaswavyo kuishi ili tupate kuwa huru na salama kupitia yeye na ili kwamba tuishi maisha ya daima na hakika ya milele.
       Kwa maana kama ilivyoandikwa katika Yohana 8:28-29; 10:30 Yesu wa Nazareti[Adam wa pili] katika wote walio na mwili yaani Wana wa Adam ndiye pekee aliye moja ya nafsi ya Mungu[nafsi ya pili] yuna Mungu na yu Mungu hakika na siku zote anatenda yaliyo mapenzi ya Mungu. Na pia yatupasa kumtazama Yesu wa Nazareti ili kumuishi Yeye hii yote ni kutokana na sababu zifuatazo na zinginezo;-
i) Ni yeye pekee aliyesema "mimi na Baba yangu wa mbinguni tu mmoja (Yohana 10:30), naam! yeye ndiye nafsi ya pili ya Mungu.
ii) Ni yeye pekee aliyesema "sitowaacha yatima nitarudi kwenu na kukaa nanyi" (Yohana 14:18), na ni kweli yuko nasi tumuaminio na kumtumaini.
iii) Ni yeye pekee aliyesema "nitakuwa nanyi milele mpaka ukamilisho wa dahari" (Mathayo 28:20), Ndiyo! Yesu kristo wa Nazareti yu Hai ndani yetu na yeye ni wa milele hakika.
iv) Ni yeye pekee aliyesema "nakwenda mbinguni kuwaandalia makao ya milele" (Yohana 14:1-4), tumaini lipo na ni kweli hakika ametuandalia makao ya milele (Ufunuo 21:1-5, 22:1-5)
v) Ni yeye pekee aliyesema"mimi nikienda kwa Baba Mungu mwenyezi nitatuma msaidizi ambaye ni Roho mtakatifu kwenu" (Yohana 14:26, Yohana 15:26, Yohana 16:7,13), Naam nakweli siku ya pentekoste msaidizi (Roho mtakatifu) alishuka kwetu (Matendo 2:1-4)
vi) Ni yeye pekee aliyekufa msalabani (Yohana 19:30,33) na kufufuka siku ya tatu (Mathayo 28:6) na kisha kupaa mbinguni kwa Mungu mwenyezi (Matendo 1:9-11)
vii) Ni yeye pekee alivyokuwa anapaa mbinguni (Marko 16:19, Luka 24:51) alisema kuwa "Mamlaka yote nimepewa mimi mbinguni na duniani" (Mathayo 28:18)

Hivyo imba tenzi ya rohoni (118) hapo chini yamkini leo ikiwa ndiyo siku yako ya kufahamu na kutambua moyoni mwako kwamba ni nini? Bwana Yesu wa Nazareti anamaanisha anavyosema “Ishi ukinitazama mimi”: