#WA WAPI WASHITAKI WAKO? [WHERE ARE YOUR ACCUSERS?]

Yesu kristo akamwambia wako wapi washitaki wako? Je hakuna aliyekuhumu kuwa na hatua?, kisha akasema wala mimi sikuhumu. Na akasema Enenda zako wala usitende dhambi tena.

Na hii ni kwa sababu yeye (Yesu) alikuwepo hapo.

Hili linanifikirisha sana, unajua nini ipo siri hapo,.. Uwapo kwa Yesu kristo upo katika mikono salama, alipo Yesu kristo uzima ni tele kwa kuwa ni Mungu, kwa maana hakuna aliyekutana na Mungu akawa kama alivyokuwa, hakuna mashitaka uwapo kwa Kristo. Kumshinda adui hivyo ni kwa wewe kujisogeza na kuwa karibu na Yesu kristo. Ukaribu na utii wako kwake unatengua mashitaka, mahukumu, mauti, magonjwa na dhambi zako zote. (Yohana 8:10).

Shetani ni mshitaki wa ndugu kama simba aungurumaye (1 Petro 5:8, Zekaria 3:1, Ufunuo 12:10). Hivyo basi mtiini Mungu. Mpingeni shetani naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribieni ninyi. (Yakobo 4:7-8, 1 Petro 5:9). Ukaribu wako na utii wako kwa Mungu ni fimbo tosha kwa shetani, hatakusogelea kabisa bali kukimbia na kukaa mbali nawe. Nguvu ya wewe dhabiti kabisa ni hii, wewe kuwa karibu tu na Yesu kristo ni hakika kwamba hakuna hukumu ya dhambi wala watesi wala maadui kuwa na nguvu juu yako (Yohana 8:6-11).

Ukiwa karibu, yaani ule ukaribu wako na Yesu kristo, Neno utalolisikia kwake ni kwamba "Usitende dhambi tena". Kwa maana kuna uhuru, uzima, msamaha wa dhambi, uchaguapo vyema, yaani kwa wewe kuchagua kuwa karibu na Yesu kristo. Chagua sasa! Bwana yupo malangoni pa moyo wako akisubiri maamuzi yako, mfanye awe Bwana na mwokozi wa maisha yako hutatahayarika kamwe na amani itatawala kwako, Amini Amua, Bwana Yu Mwema, Hatakutupa kamwe katika jina la Yesu Kristo, Amina.

No comments:

Post a Comment