#AMOS 3:3 _PATANA KOMBOA WAKATI


Biblia inasema wawili wataendaje pamoja wasipo patana, ama wasipojuana au kufahamiana vizuri.

Mwanafalsafa wa kale wa kigiriki aliweza kutofautisha watu kulingana na hulka/silika zao za asili na haiba zao zilizojengwa kutokana na mazingira ya makuzi, uzoefu wa maisha waliyopitia. Na ni kweli hili kwa sehemu kubwa linasimama hivyo hata leo, hulka yako iliyo asili yako ama haiba yako ambayo ni matokeo ya mazingira uliyoishi inakutambulisha wewe kuwa wa aina yako kitabia na kimienendo ya maisha. Na hii ni nguzo ya msingi sana hasa pale mtu anapotafuta mwezi wa maisha, kwa maana pasipo kujua vizuri aina ya mtu unayefunga nao pingu za maisha kutakufanya wewe upoteze muda wako mwingi kufikia makusudi na majaliwa ya muumba. Kwa maana mapingano mengi ya wawili walio mwili mmoja kutokana na kutotambua kwao vizuri tofauti zao kutawafanya kukinzana kimaamuzi kila wakati, kukwamishana katika utekelezaje wa jambo, uzoloteshaji wa amani baina yao na mengine mengi yanayosababisha tofauti zao kuwa kikwazo kwao.

Sasa  tabia za watu ama hulka/silika au haiba ziko za aina nne kulingana na mwafizikia wa kigiriki Hippocrates nazo ni; sanguine, choleric, melancholic, na phlegmatic. Japo kwa sehemu fulani wapo ambao huchanganya zaidi ya moja, lakini hizo nne ndio kuu.



Kama ambavyo mchoro unafafanua;
Sanguine_kwa sehemu kubwa ni mcheshi apendaye ku-jamii-ana (sociable), muongeaji sana sio wa kuaminika sana kutokana na kukosa misimamo idumuyo kwa maana mara nyingi matukio hucontrol misimamo na focus zake za maisha, hupenda utani, masihara na mizaha mingi, anaushawishi katika jamii na tabia zijumuishazo na hizo,
Phlegmatic_ kwa sehemu kubwa ni mpole sio wa makuu, wakuaminika (reliable), diplomatic, malengo yake kusimama hutegemea aliyeambatana naye na tabia zingine zijumuishazo naye, 
Choleric_ kwa sehemu kubwa anajiamini sana, kigeugeu, king'ang'anizi, mpelekeshaji, anasimamia na kutenda analoliamini kwa gharama yoyote, optimistic na tabia zingine zijumuishazo naye (ni opposity ya sanguine in terms of stability)
Melancholic_kwa sehemu kubwa ni mtu wa misimamo na mkimya apendaye kujitenga, antisocial, pessimistic, perfectionist, anamoody sana sometimes na tabia ziendenazo na hizo.(ni opposity ya Phlegmatic in tems of stability)

Phlegmatic na Melancholic ni watu wa hulka/silika/haiba ya INTROVERT (Mkaapweke, Mtawa, Mndani), wakati Sanguine na Choleric ni watu wa hulka/silika/haiba ya EXTROVERT (Bashashi, Msondani).

Hivyo uwapo katika wasaa wa maamuzi ya mwandani wako, mshirikishe Mungu umpate aliyefungu lako, huku ukijua mwenzi mwema atoka kwa Bwana, na ujue kuwa mwenzi huja kwako kukamilishwa nawe katika gap zake, yaani yule utayemumudu.

Mwenyezi Mungu akubariki upate aliyefungu lako wa kuambatana naye mnayepatana na kama ulishampata mko wote basi Mwenyezi Mungu akujalie hekima ya kumjua vizuri muishi kwa amani na umoja pasipo kuathiriwa na tofauti zenu ili basi wakati wa Bwana upate kukombolewa, amina.

No comments:

Post a Comment