Sunday, July 14, 2024

#PRAYER SECRET (SIRI YA SALA)


Sala/prayer imetokana na neno la kigiriki "proseuche" ikimaanisha- a wish, desire, request, or vow.  Hi ni kutokana mtu anamahitaji yake au shauku maishani mwake.

Sala ni package; kuna kukiri, shukurani, kusifu Mungu, kumtukuza na kumwabudu Mungu, kuomba msaada. Yaani ni zaidi ya dua.

Sala ni mawasiliano na Mungu ktk nafasi yako ya kimamlaka uliyopewa duniani.

“The ultimate object of prayer,” says The International Standard Bible Encyclopedia, “is not merely the good of the petitioner but the honor of God’s name.”

“Lengo kuu la sala,” yasema The International Standard Bible Encyclopedia, “si kutimiza faida ya mwombi tu bali heshima ya jina la Mungu."

Bill Graham ashawahi sema; "Prayer is not just asking, it is listening for God orders". ikiwa na maana Sala sio tu kuomba omba (kuna zaidi ya hilo), kuna kusikiliza matakwa ya Mungu pia.

Na kuomba sio tu kupiga kelele; kuna kuzungumza na Mungu kwa hoja zenye mashiko (Isaya 41:21), mfano wa Mfalme Hezekia (2 Wafalme 20:1-11), pia kuna kusali kwa siri (Mathayo 6:6).

Kuna mifano ya aina nyingi ya sala ktk biblia, umewahi kuwaza Cornelio alikuwa akisalije? (Matendo 10:2-4), ama kwanini Yesu alitolea mfano wa Sala za mtozaushuru na falsayo (Luka 18:10-14)?

Yamkini hatupati sawasawa na tunavyosali sababu pengine ni kule kusali vibaya kama mtu usiyejielewa (Yakobo 4:2-3), kwani sala ni mawasiliano na mbingu juu, kuna itifaki na taratibu kumfikia Mungu kwa unavyotaka kutendewa.

Na ni sharti umuendee Mungu ukijua ni mkuu kuliko matatizo yako, imani ya matarajio yapaswa iwe kubwa. Na pia toa na sadaka madhabahuni unaposali kama Cornelio, madhabahu inajengwa na sadaka zako, na hakuna madhabahu ikiwa hakuna sadaka, kwa maana hiyo madhabahu inaweza kuanzishwa sehemu yeyote ikiwa tu sadaka imehusika, kama Yakobo ili iwe madhabahu alipoota malaika wakipanda na kushuka alisali pale na kuweka ahadi ya kumtolea sadaka Mungu pale. Kumbuka Mungu aliona, anaona na yajayo ayaona na kujua yote. Hivyo ni kwa sadaka madhabahuni, Mungu anaona moyo wako na heshima unayompa, na Marko 11:17; anasema mahali pa madhababu ya Bwana ni nyumba ya sala, napo haikumaanisha ni kuomba tu, hapana, kuna zaidi ya hayo kama kuimarisha mahusiano na Mungu.

Siri ya maombi/sala zinazojibiwa ni pamoja na kujua nini usali na nini uombe  na ni wakati gani?, mahali gani? pa kusali na kuomba, na sio kusalisali na kuombaomba ilimradi unapayuka tu. Hapana, kuna sala zingine unazungumza na Mungu kwa utulivu kabisa na kisha utake kumsikia Mungu anasemaje juu ya ombi lako, zingine unaomba hili na lile huku ukidadavua kwa nini akupe wewe, zingine ni shukurani tu, zingine za hoja za msingi unakomaa na Mungu na reference kwa nini kung'ang'ania unachong'ang'ania kiwe. Zingine za kimamlaka unatiisha, unatangaza na kuamuru ziwe kutokana na mamlaka ya neno uliyopewa, na zingine ni mapambano, sala za vita ni kama kinywa kinatema risasi mfululizo kwenye ngome za maadui, watesi wako,  kukemea pepo na roho za kichawi na uganga.

Kwa mkristo sala na maombi ni silaha pekee, ya kumthibitisha yeye ni nani ktk mbingu ya Mungu na mamlaka gani yuko nayo kuitiisha dunia na kuamuru mambo yatokee kwa matakwa yake kama Bwana mwenyewe amupavyo kutenda🙏🏾.