#YESU NINAYEMUABUDU NA KUMWAMINI

  

       Biblia imeandika Neno la Mungu lenyeuhai kwa kila kiumbe, na kutupa njia sahihi kwa mifano elekevu itujuzayo kweli ya Mungu na kwa namna ya kufunua na kuthibitisha uhusiano wa mwanadamu na Mungu ulivyozaidi ya mahusiano mengine. Ona katika kitabu cha Mwanzo 3:9 neno linasema; "Bwana Mungu akamwita Adam, akamwambia uko wapi?", sasa kwa hali ya kawaida tunajua Mungu yupo popote na anaona kwote na hivyo mlengo wa swali ulihusiana na nafasi. Kama mzazi wa kawaida kuna tofauti kubwa kumuwajibisha mtoto; 1) yule aliepata shida au kutenda kosa lakini yu katika nafasi yake 2) na yule aliepata shida au kutenda kosa hali akiwa nje ya nafasi yake, sikuzote hupokea ya heri yule aliyekosea hali yu katika nafasi yake kuliko yule aliyekuwa ametoka kwenye nafasi yake. Mzazi humwambia yule aliekatika nafasi yake japo ni mkosaji, pole na kumuelekeza vizuri namna inavyotakiwa kuwa na kufanya, kwa maonyo laini, lakini, kwa yule aliyekosa huku akiwa ametoka nafasini pake huonekana kama muasi, laana na huchochea hasira ya mzazi na hata kuitwa majina au kutamkiwa maneno yasiyo na heri maishani mwake.
         Kwa mfano huo shauku ya Mungu ni sisi tuishi katika nafasi tuliyopewa ili tusitawi, tumiliki na kutawala, wingi wa matatizo yetu ni kwa sababu ya kutokuishi katika nafasi zetu kutokana na sisi wenyewe kutokujua vyema nafasi zetu na haki zetu katika Bwana. Mwanadamu ni wa thamani sana kwa Bwana Mungu kwa kiwango kikuu kuzidi viumbe wengine hadi ametupa sisi mwongozo wakuishi maisha ya ushindi kuanzia agano la Kale mpaka Jipya. Thamani tuliyopewa hata Mfalme Daudi alijishangaa Zaburi 8:4, yaani tumestahilishwa kwa namna ya ajabu ambapo huwezi hata linganisha na yale tuyatendaye, yeye Bwana Mungu hachoki, anatupenda kwa upendo mkuu siku zote, huku toka mwanzo akituahidi ukombozi na utu upya kupitia Kristo Yesu ambaye toka mwanzo alimdhihilisha kwetu na kutufunulia namna mwanadamu apasavyo kufanya ili awezeokoka na kuishi maisha huru pasipo dhambi, jambo ambalo kiuhalisia ni gumu kutekelezeka pasipo neema iliyo katika Kristo.
Lakini haya ni mafumbo makuu ambayo toka mwanzo, Mungu alikuwa anatufunulia kuelekea ule ukombozi mkuu wa Bwana Yesu Kristo, kwa yeye kufanyika kama sadaka ya upatanisho kati yetu sisi na Mungu (1 Wakorintho 5:7);
a] Mbuzi wawili wa upatanisho katika agano la kale:
Ukisoma Walawi 16:7-10 utapata uelewa kuwa mwanadamu alipaswa kupeleka mbuzi wawili kwa Kuhani mkuu ambao walipigiwa kura; moja kwa ajili ya Bwana kama atoning sacrifice ambapo damu yake ilifanyika patanisho la yule mwanadamu na Mungu na kura nyingine ni scapegoat kwa ajili ya Azazeli ambapo mwanadamu alipaswa kuweka mikono juu ya kichwa cha scapegoat nakukiri dhambi zake zote, kisha huyo mbuzi aliyejaa dhambi za mwanadamu huacha jangwani na maovu ya yule mtu hadi kufa kwake. Na hivyo kwa namna hiyohiyo Yesu amefanyika sadaka ya upatanisho kama ilivyokuwa mbuzi wa sadaka ya dhambi na pia aliamua kuwa matokeo ya dhambi zetu kama yule scapegoat kwa kubeba dhambi ya dunia (1 Yohana 2:2) ili sisi tuwe na uzima wa milele. Katika hili sasa unawezafunguka vizuri pale Yohana Mbatizaji  (Yohana 1:29) aliposema; tazama mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu na baada ya kufunuliwa kwake huku tu akachukuliwa jangwani kujaribuni huku mzigo wa dunia ukiwa mabegani mwake.
b] Nyoka wa shaba jangwani:
Katika Hesabu 21:4-9 ufunuo wa ukombozi kama wa Mwokozi wetu Yesu Kristo ulimjia Musa kwa kufanya nyoka wa shaba ilikwamba kila mwanaisraeli kwa mouvu yake juu ya Bwana kupata nafasi ya kujipatanisha upya na kuwa wazima, kwa kigezo kuwa kila muisraeli aking'atwa na nyoka wenye sumu maana walikuwa wakiwasababishia mauti, basi atapaswa kumwangalia nyoka wa shaba aliyeangikwa mtini na pindi afanyavyo hivyo ndipo sumu ya nyoka iliwatoka na umauti uliwaacha. Na hilo fumbo Yesu Kristo alilinena wenyewe katika Yohana 3:14-17 ya kwamba;"kama Musa alivyomuinua Nyoka wa Shaba kule Jangwani,Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye". Yesu alitufungua katika kuamini namna ukombozi unavyoweza kumjia mtu na kisha kupata uzima wa milele, kama mahesabu ama kanuni zinavyoweza kuthibitishwa na kuhakikishwa usahihi wake ndiyo ilvyo wokovu katika Kristo, kuna ukombozi na uzima katika kumtizama yeye maisha yako yote; kwa sababu vyote ni vya Bwana na vita ni vyake, hivyo amani yake iamue leo ndani yako, nafsi yako iwe huru milele.
c] Mauti ya Msalaba ya Yesu Kristo:
Kama nabii, Yesu alikuwa ni zaidi kwa maana yeye ndio neno la unabii wa biblia yote na yote ambayo hayakutoshea humo, na kama Kuhani mkuu, Yesu alikuwa zaidi maana yeye ndiyo sadaka kamili iliyothibitisha ukombozi wetu. Na ni zaidi ya mfalme kwa maana yeye ni zaidi ya vyote hana mwanzo wala mwisho, ni Alfa na Omega. Hata alipoangwika msalabani Wakolosai 2:14-15 inasema;"akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo."

Kufedheshwa huko msalabani hadharani kwa Yesu kulionyesha ushindi wa msalaba juu yake kwa ajili yetu sisi wanadamu na hakika nguvu na mamlaka za shetani (kuzimu na mauti) zilikomea hapo. Kama ilivyotukia kwa mbuzi wale wawili wakati wa agano la kale na kwa nyoka wa shaba wakati wa Musa, ndivyo ilivyotokea wakati wa mauti ya msalaba kuzimaliza nguvu za shetani, na hata aliposema ilikwisha alimaanisha hivyo aliona hivyo kuwa mzigo kwa azazeli alijitwishwa yeye na kwenda kubatilisha mauti na kuzimu  naye akashinda, ndio aliona hivyo kwamba sumu za nyoka ziliwatoka wote waliomtazama yeye nao wakapata uzima wa milele, hivyo ni jukumu lako kumtazama Yesu Kristo akomboe maisha yako na kukupa uzima wa milele. Kwa maana picha halisi ya yeye kuwa msalabani ilikuwa ya kwamba mwanadamu mdhambi mwenye mauti ndani, na yeye Yesu kufanyika dhambi na mauti ili kuvuta dhambi na mauti vilivyokuwa mwilini wa mwanadamu na kumfanya mpya pindi amtazamapo yeye, na yeye kufanyika hiyo sadaka ya dhambi ya upatanisho na Mungu. Amini leo ndugu okoka leo, ukiwa kwa Yesu Kristo ya kale yamepita tazama ni mwanzo mpya wa maisha yako.

No comments:

Post a Comment