God's Way not mere talk, it's an empowered life; living by God's power.
Ndio!, Ufalme wa Mungu ni nguvu ktk matendo na sio maneno sana (power in action)~1Wakorintho4:20.
Matendo 19:1-20; Neno la Mungu la ufalme (kingly word of God) lilizidi kuenea Efeso na kushinda kwa nguvu, sababu ya nini? uthihirisho wa Roho Mtakatifu.
Sasa kama ni majivuno kwa mkristo yeyote, ni kwa sababu ya kumpata Roho Mtakatifu, ambayo ni neema kubwa sana. Waliomsikia Yohana mbatizaji Neno linasema waliamini neno la toba wakatubu na kubatizwa ikaishia hapo, ila ktk Yohana 1:12 kwa waamini wote wa Yesu kristo Mnazareti, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ule uwezo ndio nguvu iletwayo na Roho Mtakatifu.
Na je' sasa we ni mwamini wa Yohana Mbatizaji ama wa Yesu Kristo wa Nazareti? Jiulize!
Mwana wa Mungu kama kweli ndiye, son/daughter of God, omba uwe na Roho Mtakatifu, hapo inaleta maana ktk imani yako, na asiwe anaheri mpagani kukuzidi, naye huyo Roho akiwemo ndani yako atajithihirisha nawe utakiri kweli sasa ninaye.
Mfano mzuri ktk kizazi chetu mwanzoni mwa miaka ya 1900s, Mwafrika mweusi William J. Seymour, mtumishi wa Mungu huyu aliyekuwa kipofu jicho moja hakupendezewa na imani butu, alitamani matendo ya mitume yaendelee na aliamini kuwa kunena kwa lugha ni ishara mojawapo ya mtu kumpokea Roho Mtakatifu (Holy Spirit Baptism), akawa na shauku sana kila akisoma Matendo 2:4, shauku hiyo ikampelekea kuwa na mzigo kutaka kupokea na hata baada ya imani kujaa aliokuwa akiwahubiria wakaanza kupokea na kisha naye akajazwa Roho Mtakatifu miaka ya 1914, na ndio ulipozaliwa uamusho wa Roho mtakatifu kwenye mitaa ya Azusa ya Marekani, mpaka mitaani watu wakawa wanajazwa wanalewa Roho Mtakatifu na kuanza kunena kwa lugha mpya, na huo ukawa mwanzo mpya tena wa upentekoste kuenea kwa kasi baada ya kanisa kupoa kwa muda na huduma nyingi zikaanza utume duniani kama Assemblies of God iliyoenea duniani kwote, nawe unajua kama hapa Tanzania huwezi zungumzia mwanzo wa upentekoste bila kutaja Tanzania Assemblies of God (TAG), lakini jua ilianza na shauku ya mtu mmoja, hii ikithibitisha kuwa Mwana wa Mungu kweli akiwa na Roho Mtakatifu ni Kuhani wa Kifalme na Taifa teule🙏🏾.
so,
#Receive Holy Spirit
#Live like King, talk like Him
#Kingly virtues.
#Serve the Almighty God