Sunday, May 31, 2015

#PERSONS OF WHOM THE WORLD WAS NOT WORTHY / WATU AMBAO ULIMWENGU HAUKUSTAHILI KUWA NAO

     Persons of whom the world was not worthy; they inspired faith inside us, they made us believe Him. 
And all these, having gained approval through their faith, did not receive what was promised, because God had provided something better for us, so that apart from us they would not be made perfect. We have the hope of eternal inheritance in Christ because of God faithfulness to them, that made our faith in Jesus grow high. We are confident in Christ because of them, thanks Jesus for this grace and mercy in the mighty name of Jesus of Nazareth ("The Christ").
It is the truth, the world did not deserve to have those mighty men, they were light in this world to the way of life and beginning of our belief in the lord Jesus Christ of Nazareth, they caused us to believe that the LORD in Old Testament is the same JESUS in the New Testament, who is the Mighty God, Be blessed, Amen.

   Watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao; walifanyika chachu ya Imani ndani yetu; ile kumuaminisha Kristo kwetu. Watu ambao walishuhudiwa vema kwa sababu ya imani yao lakini hakuna hata mmoja wao aliyepokea ile ahadi, na Biblia inasema kabisa hii yote ni kwa sababu Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea kitu kilichobora zaidi ili tu kwamba wao wasikamilishwe pasipo sisi. Na sisi kwa sababu yao tunalo tumaini la urithi wa milele lililo katika Kristo Yesu lililo la hakika la kweli, ule uaminifu Mungu aliouonyesha kwao umetupa uhakika rohoni mwetu na kukuza imani zote kwa Bwana. Tunaoujasiri mkuu katika Bwana, kwa sababu ya wale watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao walifanyika wa kwanza kutuonyesha yaliyo ya Mungu yale matendo aliyoyatenda toka kale tuliyoshuhudiwa, tuliyayasikia na kuona ya kwamba Mungu ni mwema na wema wake ni wa milele, hivyo tunakushukuru Mungu kwa ajili ya neema hii kuu kwa maana wao ndio waliotuaminisha kuwa yule BWANA wa kwenye Agano la Kale ndiye yeye yule Yesu wa Nazareti aliye Kristo katika Agano Jipya na ni Mungu hakika, Amina.

Read more: Hebrews 11:32-40; Waebrania 11:32-40