Monday, July 6, 2020

#ROHO MTAKATIFU


Roho Mtakatifu (Swahili), Inumbula ja Nguluvi (Bena), Mumuyo Mwele (Chaga), Embeera z'obuntu bw'Omwoyo Omutukuvu (Luganda-Ungada), Umwuka wera (Rwanda), Mweya Mutsvene (Shona-Zimbabwe), Umoya Ongcwele (Zulu-S.Africa), Gbigbo Wiwe (Yoruba-Nigeria), Holy Spirit (English), Holy Ghost (English), Ruach HaKo'desh (Hebrew), Allos Parakletos (Koine Greek), Paraclete(Greek), Spiritus Sanctus (Latin), Heiliger Geist(German), esprit Saint(French), Spiorad Naomh(Irish), Svyatoy Dukh (Russian), Espíritu Santo(Spanish), vyovyote utakavyomuita kwa lugha yako.
    Roho Mtakatifu ndiye aliye ndani ya Yesu Kristo yaani Mungu Baba ndio huyo huyo mmoja hakuna watatu. Biblia (1 Yohana 5:7-9) inasema watatu wanashuhudia mbinguni; Mungu Baba, Neno na Roho Mtakatifu nao ni mmoja (MUNGU) na watatu duniani; Maji, Damu na Roho nao ni mmoja (Mwanadamu). Sasa kama ambavyo mwanadamu hawezi kugawanyika na kuwa zaidi ya mmoja yaani kama Recknald ni Baba, Mume na Mhasibu atakuwa ndiyo yuleyule Recknald mmoja daima, ndivyo ilivyo MUNGU ni mmoja regardless His manifestations to human beings. Hivyo kama basi ushuhuda wa mwanadamu unapokelewa kuwa ni kweli basi wa Mungu ni mkuu zaidi, ushuhuda wa Mungu ndio huu amemshuhudia mwanawe, yaani mwana wa Roho Mtakatifu, full stop. Amini leo kama bado.
Na hii ni hakika na kweli kwamba Roho Mtakatifu ndiye Mwalimu wetu, Mfariji wetu, Msaidizi wetu, huyu Mungu mmoja ndiye huyo huyo ndiye yeye kwetu na wa mfanano wetu wala si kitu, ama njiwa ama wa ishara yeyote unayodhani wewe kumlinganisha au kumfananisha kwayo, ni wa mfanano wetu wanadamu yaani Mungu.
   Huyo ndio habari njema ya dunia tangu kupaa kwa Yesu Kristo kwenda mbinguni na mbali, mbali zaidi ya mbingu, hakuna habari mpya zaidi ya hiyo ya Mungu pamoja nasi daily (yaani Roho Mtakatifu ndani yetu). Huyu yupo live duniani yupo nasi sasa hapa hapa duniani ndani yetu anatusaidia katika udhaifu wetu hatujui kusali vyema anatuwezesha tutiwe nguvu ya kushinda katika yote, kupitia yeye na kwa ajili yake ndani yetu tunasali, tunaomba, tunabarikiwa na kushinda yote, tuna huo uweza kwake na uwezo katika yote kwa maana ndiye yeye ayakamilishaye yote ndani yetu; yaani Roho Mtakatifu ndiye Mungu baba, ndiye Mungu mwana hapo, wala huwezi kabisa tofautisha watatu walio mmoja ndani yetu, ni ahadi na ilishatimia kwetu.
   Hivyo tembea kifua mbele sio kwa sababu ya nguvu za mwili wako, ama akili zako na utashi, ama uwezo wa kufanya kitu, ama utajiri wako na mali, bali kwa kuwa makao makuu (HQ) ya Roho Mtakatifu ni ndani ya wateule wake waliokombolewa kwa damu yake yaani Yesu Kristo.
  Kama umeamini katika hili na Yesu Kristo kafanyika Bwana na mwokozi wa maisha yako, yote haya ni yako, kwa kuwa ukombozi na uweza wa kukuunganisha katika neema hii una yeye Bwana, hivyo nasema barikiwa na Roho Mtakatifu siku zote katika jina la Yesu Kristo, amina.