Tuesday, October 15, 2024

#UFALME WAKE, UFALME WETU


Luka 12:29-32 inashangaza sana, Yesu anasema; "Msiogope! enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vyema kuwapa nyie huo Ufalme". He said; "It's your Father's good pleasure to give you the Kingdom."

Hata Daniel 7:27 alitabiri kwa habari ya wana wa Mungu akisema; "Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii".
Tena katika  Yohana 17:22 Yesu anasema; "Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo na umoja".  ona He said; "that  glory which  you gave me, i  have given them", this is  powerful!
Sikia hii; aliteswa tupate haki ya kuwa na kuitwa wana wa Mungu.
Iliyoitwa kufuru kuwa mwana wa Mungu  ikawa haki yetu.
Kwa uthubutu wake, akagharamia hata mauti yake, alitamka hivyo ikawa.
Na haki hiyo ilikuja na uweza uliotupa sisi ujasiri na nguvu katika ukiri wetu kuwa sisi ni wana wa Mungu hakika.

Ilimchukua yeye kuishi kama sisi ili tuupate ufalme wake (Wafilipi  2:6-8); yeye mwenye namna ya  Mungu  toka  mwanzo alichukua namna ya  mtumwa akawa na mfano wa  wanadamu halafu alijinyenyekeza sana akawa mtii mpaka mauti, naam, mauti ya msalaba (kwani ilikuwa laana mtu kuangikwa msalabani-Wagalatia 3:13-14), Yesu anasema jina lako Baba litukuzwe duniani (Yohana 12:28, 17:4,6), kwamba kuitwa kwetu sisi wana wa Mungu ni utukufu kwa Mungu Baba.
Fikiria jina lake la heshima; imeandikwa  ktk Wafilipi 2:9-11 kwa jina hilo kila goti lipigwe la vitu vyote vya mbinguni, duniani na kuzimu.
Halafu, alizaliwa nalo kikawaida kabisa, kipindi kingine alikimbizwa nalo kwenda kufichwa Misri, aliishi nalo mitaani, alicheza nalo na hakuna aliyejua, saa ilipofika akajifunua kwalo hakuna aliyemsadiki, alikataliwa nalo, akatukanwa nalo, akatengwa nalo, makanisa yakamuhukumu nalo, akateswa nalo, akasulubiwa nalo, kufa nalo msalabani na kuzikwa  nalo.
Hii yote kwa ajili yako wewe na mimi,   kwani hakuwa tayari kuona sisi tunanyanyaswa kwa kuwa gizani kuishi isivyotusitahili asili yetu, kwa hivyo siku ya tatu akafufuka nalo, halelujah! ili tu sisi tukamilishwe kwalo, tuitwe na tuishi kama wana wa Mungu, wana wa ufalme wa mbinguni  duniani. Bwana Yesu asifiwe!..
Chukua nafasi hiyo sasa, kaa hapo, angaza, barikiwa, occupy till when He come again. Indeed; you are the son/daughter of God, amen.